Maudhi katika ndoa yanaweza kuwa mazito sana na
ndipo mlalamikaji mume au mke anapokwenda
mahakamani kudai amri ya kuvunja ndoa kabisa
ambayo inaitwa amri ya talaka.
Sheria ya ndoa ya mwaka 1971 inasema ya kuwa
mashauri ya kudai talaka ambavo lazima yatolewe
na mahakama yanapaswa kwanza kupitia kwenye
baraza Ia usuluhishi. Mabaraza ya usuluhishi yapo
mengi na yameundwa kwa shughuli hiyo kwenye
vijiji na mijini. Jukumu Ia mabaraza hayo ni
kuwasuluhisha mlalamikaji na mlalamikiwa ili
waweze kusameheana. Baraza hilo linaposhindwa
kusuluhisha, hawana budi kutoa shahada kwa
mume na mke wanaohusika. Shahada
hiyo itamwezesha mlalamikaji kufungua
madai ya talaka kwenye mahakama. Bila
shahada hiyo madai hayawezi kupokele-
wa mahakamani. Sababu zinazoweza kuf-
anya ndoa ivunjike.
(a) Maasi au utoro wa makusudi
usiopungua miaka mitatu.
(b) Mlalamikiwa kufungwa jela kwa
muda wa miaka mitano mfululizo au
maisha.
(c) Kutengana kwa hiari au kwa amri ya
mahakama kusikopungua miaka
mitatu.
(d) Ukatili wa mwili au akili kwa watoto
wa ndoa au kwa mlalamikaji.
(e) Kichaa kinachothibishwa na
madaktari wawili kwamba hakiponi.
(f) Mlalamikaji kubadili dini ikiwa wote
walikuwa na dini moja wakati wa
kuoana.
Kwa mujibu wa dini hiyo kubadili dini
kunavunja ndoa au kunakuwa na sababu
za kuvunja ndoa