Ndugu kwanza nashindwa nianzie wapi ila fanya haya yatakusaidia humu jamvini!
_ Weka uzi wako kwa aya/paragraphs, itafanya ulichoandika kivutie na pia kueleweka mapema.
_Jiepushe na utumiaji wa wingi katika nyuzi za namna hii,mfano umetumia sana wingi "tumemchagua Mbunge" hapa mbunge hachaguliwi na wote,avoid generalization , mfano nikuulize swali WEWE ULIMPIGIA KURA MB NDUGAI? KAMA NDIO JE UNADHANI WOTE ULIOSEMA TULIMPIGIA KURA WOTE NI WA JIMBO LA KWA NDUGAI?
_epuka kuleta mijadala isiyo na ushahidi, sheria zipo na ignorance of law haikulindi chochote, avoid such fallacious statement, umesema WATANZANIA "tunauana kisa madaraka" Wewe umeshaua wangapi mkuu?
_Jikite kwenye hoja moja, be specific,mfano hoja yako mwanzoni unahoji na unataka kujua sheria zinasemaje pale mbunge anapofariki, mara kati kati tena unaleta habari mara sijui za mbunge kuwa mbunge alihali ashafukuzwa uanachama ,,humo humo tena umelalamika kuhusu speaker NDUGAI yaani hueleweki
Sent using
Jamii Forums mobile app