Sheria inasemaje kuhusu watu kuwa na plate number za kubandika na kubadili watakavyo?

Sheria inasemaje kuhusu watu kuwa na plate number za kubandika na kubadili watakavyo?

Cute Wife

Platinum Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
3,054
Reaction score
8,449
Wakuu,

1000367256 (1).jpeg
1000367257 (1).jpeg

Kwenye picha hiyo gari imewekewa pini zinazotumika kubania karatasi, ambapo kwa nilivyoelezwa inamuwezesha mhusika kubadili plate number haraka sana. Anachofanya ni kubetua hizo pini na kuweka plate number nyingine kwa juu!

Hii inamaanisha unaweza kugongwa, kutekwa, na kufanyiwa vitendo vingine vya ukatili na usiweze kumpata muhusika, sababu kubadili hiyo namba ni kitendo cha dk 0 tu.

Hapo unapata maswali, huyu mtu ameshabadili hiyo plate mara ngapi mpaka amepata ujasirj wa kutembea na hiyo plate ikiwa hivyo mchana kweupe? Ameshatekeleza matukio mangapi huko barabarani ambayo mpaka leo hayana majibu juu ya nani alifanya matukio hayo?

Sheria inasemaje watu hawa ambao wakati wowote wanaweza kubadili namba na kufanya matukio? Ndio watu wasiojulikana au wahuni tu wa mjini? Dr. Mwigulu Nchemba
 
Sheria inasemaje watu hawa ambao wakati wowote wanaweza kubadili namba na kufanya matukio? Ndio watu wasiojulikana au wahuni tu wa mjini?
Tanzania ni Taifa la Kambale, kila mmoja ana ndevu asaivi.

Watekaji mostly ndio hutumia hizo gari.

Anyways, acha inyeshe tutajua tu wapi panavuja.

Yule jamaa wa Land cruiser hard top waliomkamata wakasema alitishia Toy la Bunduki, gari yake pia ilikuwa na namba fake, fuatilia ile habari utaelewa ni kina nani hasa wana hio tabia ya kishenzi.
 
Naikumbuka! Kwanini umtishie mtu na toi in the first place?! Majambazi yameshika Power!
 
Back
Top Bottom