Sheria inasemaje kwa watumishi wa umma kushindwa kesi mahakamani

Kuchasoni Kuchawangu

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2012
Posts
620
Reaction score
370
Wakuu salam
Naomba ufafanuzi wa sheria hasa kuhusu Kesi ya madai ambayo inamhusisha mtumishi wa umma baada ya kushindwa Kesi na kuamuriwa kulipa gharama na mahakama. Je anaweza akahatarisha ama kupoteza ajira yake pindi akishindwa kulipa gharama za kesi? ama kuna madhara gani anaweza yapata kutokana na kesi ya madai hususani ajira yake?
Karibuni kwa mawazo na ushauri wa kisheria.
 
...kesi ya madai haina athari ya moja kwa moja na ajira yako, labda kama mwajiri wako alihusika moja kwa moja kwenye hiyo kesi, na sheria za kazi hazimruhusu kukuachisha kazi kutokana na madai hayo
ingekuwa vizuri ukaeleza ni madai ya namna gani, na ni kwanini umekuwa na hofu ya ajira yako.

maana hata ugomvi wa kifamilia ni madai pia

Fahamu kwamba madai ni mambo binafsi ya mtu
 
Mtumishi wa umma unafanya biashara ya pesa kwa maana ya kukopesha kwa riba, ikatokea uliyemkopesha akashindwa kukulipa ukampeleka mahakamani ukamshinda na mahakama ikaamua kumfilisi, akafilisiwa lakini akakata rufaa high court akakushinda na mahakama ikaagiza ulipe gharama za kesi. Jamaa akaja na gharama kubwa kushinda kiasi ulichokuwa unamdai. Je ukishindwa kulipa nini madahara yake kwenye kibarua
 
mkuu samahani nimecheka sana kibao kilipogeuka ya dunia mengi ngoja waje wataalamu wafafanue
 
Mtumishi wa umma unafanya biashara ya pesa kwa maana ya kukopesha kwa riba, ikatokea uliyemkopesha akashindwa kukulipa ukampeleka mahakamani ukamshinda na mahakama ikaamua kumfilisi, akafilisiwa lakini akakata rufaa high court akakushinda na mahakama ikaagiza ulipe gharama za kesi. Jamaa akaja na gharama kubwa kushinda kiasi ulichokuwa unamdai. Je ukishindwa kulipa nini madahara yake kwenye kibarua
Hakuna madhara mkuu. Wewe dunda tu, mwajiri wako hahusiki kwa lolote kwa kuwa hiyo kesi haina uhusiano na ajira yako
 
Mtumishi wa umma unafanya biashara ya pesa kwa maana ya kukopesha kwa riba, ikatokea uliyemkopesha akashindwa kukulipa ukampeleka mahakamani ukamshinda na mahakama ikaamua kumfilisi, akafilisiwa lakini akakata rufaa high court akakushinda na mahakama ikaagiza ulipe gharama za kesi. Jamaa akaja na gharama kubwa kushinda kiasi ulichokuwa unamdai. Je ukishindwa kulipa nini madahara yake kwenye kibarua
Kama Kuna uwezekano ningependa kujua hiyo rufaa huyo alishindaje

lakinj poa bado unanafasi ya kukata rufaa mahakama ya rufani Kama bado upo ndani ya muda.

zaidi Ni kuwa hakina athari za moja kwa moja kwenye ajira yako hata Kama umeshindwa kesi kwakuwa hiyo siyo kesi ya jinai Na haina effect kwa ajira yako au kampuni iliyokuajiri.

katika sababu za sheria za kazi Na mahusiano kazini, hakuna sababu inayofaulu katika hizk Ili kuachishwa kazi
 
Back
Top Bottom