Sheria inayombana mfanyabiashara kuuza bidhaa(Goods sale Act of …….)

tpaul

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
24,225
Reaction score
22,632
Ndugu wanajamvi,

Nimejitokeza hapa jukwaani kuuliza swali hili ili nipate ufafauzi wa kisheria. Je, kuna sheria yoyote iliyotungwa na Bunge la JMT inayombana mfanyabishara kuuza bidhaa? Na kama ipo, ilitungwa lini na ni adhabu gani inayotolewa (kifungo cha miaka kadhaa jela, kutaifisha bidhaa, au kupigwa faini) kwa yeyote anayeivunja?


Najua humu jukwaani kuna wanasheria waliobobea katika sheria watatusaidia kutoa ufafanuzi wa kisheria. Ninaamini pia baadhi ya wanaJF ambao ni mbumbumbu wa sheria kama kama mimi watanufaika na ufafanuzi huo. Mods tafadhali nilinde…wala msihamishe uzi huu kuupeleka kwingine. Uache hapa hapa hadi tupate majawabu mujarabu kuhusu mkanganyiko huu wa kisheria kutoka kwa wataalamu kabla nchi haijapata hasara kwa kushtakiwa na wafanyabiashara wanaolazimishwa kuuza bidhaa.
 

Kama watu wachache wananunua sukari nyingi na kuficha ili kutengeneza uhaba na kupanda bei juu ili wananchi wateseke na kuilaumu Serikali ya Magufuli ya kutetea wa TZ. Je hii inahitaji sheria? Watoto jana hawakupata chai leo, leo wanaficha sukari kesho madawa baadae peterole... inshi hii kweli itaenda mbele? Kwa hili hatuhitaji sheria bali maamuzi ya haraka sana
 
Mleta mada kaulizia kuhusu SHERIA inayo....
Nami nasubiri kufaidika na ufafanuzi wa Wanasheria wasomi...
 
mbona hii scarcity haikutokea kabla ya zuio la rais?

kama ishu ni watu kuhodhi sukari kwa nini Rais aagize sukari nje ya nchi?
 
Mkuu mbona unaomba Mods kukulinda? Au ulichopost kinamakosa? Kama unajua kimepostiwa sehemu siyo sahihi, kwanini usikipost mahala sahihi? Au JF nayo imekuwa ni sehemu ya kulindana?
 

Je mkifika mahakamani mnaweza define kwa ushahidi hiyo intention ya 'kuficha'?
 
Je mkifika mahakamani mnaweza define kwa ushahidi hiyo intention ya 'kuficha'?
Angalia sheria ya kuhujumu. Na tambua kuwa hali hii ilihitaji hatua ya haraka ya ku rescue Taifa kutoka kwa maadui wenye nia mbaya na wananchi. Sugar ili shoot hadi 3000 na kwingine haikuonekana kabisa. Nchi ilikuwa inatekwa na hawa wahujumu wenye pesa wachache wenye nia mbaya ,labda nawe humo??? Au unatetea waovu.
 
Usipende kunijibu huku ukifahamu fika Una kiwango finyu cha uelewa mithili ya kima....
Nimeuliza je huko mahakamani wanaweza kwenda thibitisha intention ya 'kuficha' jibu hilo Kama ulipata lishe bora utotoni Kama ni wale wa lishe mbovu pita kushoto.....
 
busara ingekuongoza kutokuchangia chochote hapa maana mleta mada ana-discuss sheria sio watu. (note: low minded discuss people, average discuss events, great discuss ideas).
Between; uzalishaji wa sukari nchini haukidhi mahitaji, ndo maana watawala waliotangulia walikuwa wanaagiza nje sehemu inayopungua kufidia gap. na ndo maana waliopo sasa hivi nao wamelazimika kutoa vibali vya kuagiza sukari nje tani 100 kufidia gap kama walivyofanya waliotangulia.
zingine ni porojo tu.
 
Hiyo sheria ya economic imenukuliwa mara kadhaa ktk mjadala huu wa waficha sukari hususani wa yule wa Mbagala aliyekuwa ameficha sukari takribani 5,000 ambayo thamani yake ni takribani sh trilion 12.5! yaani zaidi ya bajeti yetu ya maendeleo ya mwaka mzima.
Hapo ndipo nchi yetu ilikuwa imefikia - yaani kwa kufanya biashara tu na serikali ( siyo kuzalisha kiwandani kwake) mtu anakuwa na ukwasi wa kiwango hicho.
 
MKUU, HAPA HATUONGELEI SUKARI TU BALI BIDHAA ZOTE ZINAZOUZIKA. KWA MFANO, BAADA YA MAVUNO KUNA WAKULIMA WANAOHIFADHI (FICHA?) MAZAO KWENYE MAGHALA HADI MSIMU WA MAVUNO UNAPOPITA NA KUYAUZA KWA BEI YA JUU SANA. JE, HAWA WAKULIMA NAO NI MAJIPU?
 
mbona hii scarcity haikutokea kabla ya zuio la rais?

kama ishu ni watu kuhodhi sukari kwa nini Rais aagize sukari nje ya nchi?
KAMA KWELI KUNA SUKARI IMEFICHWA KWA NINI SERIKALI ISIRUHUSU WAFANYABIASHARA WAAGIZE SUKARI IWAACHE HAO WANAOFICHA WAENDELEE KUFICHA HADI IOZEE MAGHALANI?
 
Mkuu mbona unaomba Mods kukulinda? Au ulichopost kinamakosa? Kama unajua kimepostiwa sehemu siyo sahihi, kwanini usikipost mahala sahihi? Au JF nayo imekuwa ni sehemu ya kulindana?
MKUU NIMEJIHAMI KWA SABABU KUNA BAADHI YA MODS HUKURUPUKA KUHAMISHA NYUZI PASIPO SABABU YA MSINGI.
 
Duh sukari ya mbagala gharama yake zi zaidi ya trillion 12?? Kweli Tanzania tuna idadi kubwa ya wafu wanaotembea.... Kweli wewe daktari wa akili.
 
Huu mchezo hautaki mzuka bali ni kanuni za kiuchumi. Sukari ni kidogo ndani ya nchi siyo kuwadanganya Watanzania na waingize sukari kutoka nje kama viwanda vya ndani havikidhi uhitaji. Just increase supply umemaliza siyo kupambana na wafanyabiashara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…