Aloysius
Member
- Mar 1, 2011
- 80
- 9
Je wajua kuwa una haki ya Kumshtaki Wakili wako Mzembe
Ni bahati mbaya kuwa wanasheria ndiyo waelimishaji washeria, hivyo basi nivigumu kukuta wanatoa elimu inayowanyooshea vidole.
Kupitia mwanya huu, baadhi ya Mawakili, ambao bila shaka ni wachache wamekua Mamwinyi dhidi ya wateja wao, wakifahamu wazi kuwa wateja hawajui haki zao dhidi yao.
Mambo ambayo yanalalamikiwa haswa na wananchi wengi dhidi ya baadhi ya wanasheria wasiyo heshimu miko ya sheria ni pamoja na:-
1. Uzembe na au kupuuza kesi za wateja hasa pale ambapo wamekwisha bugia pesa za mteja
2. Kuwazunguka wateja na kuwa kitu kimoja na upande mwingine kwa namna ambayo ina muumiza mteja
3. Kutokuwa makini katika kuandaa kesi ya mteja jambo ambalo linapelekea kesi kuwekewa pingamizi na kumuumiza mteja
Katika hili, sheria haiko kimya, Kuna sheria inayoongoza shughuli za wanasheria maarufu kama, The Advocates Act, R.E 2002. Sheria hii inainisha miiko kadha wa kadha ambayo Mwanasheria ni sharti aifate katika kuendesha kesi ya mteja.
Miiko hiyo ikivunjwa kipo chombo ambacho mwananchi anapaswa kumlalamikia wakili ambacho kwa bahati nzuri ni cha haki mno, kinaitwa Tanganyika Law Society ama kwa kifupi TLS.
Mwananchi usikubali kupoteza haki yako kwa kuwa hujui ni hatua gani uchukue dhidi ya wakili wako, kimbilia TLS, kwani TLS ni kimbilio la haki. Chukua hatua.
Angalizo: Usiwe mwepesi kufikia uamuzi kuwa wakili wako anastahili kulalamikiwa katika chombo hicho, subira huvuta heri.
Makala hii imeandaliwa na:
Aloys Rugazia
Afisa Sheria
MARS Legal Consultants
P.O Box 6445, Dar es Salaam
Kinondoni, Email: marslegalconsultants@outlook.com
Ujumbe Mfupi: +255 654323268