Sheria inayombana wakili anapoboronga

Sheria inayombana wakili anapoboronga

Aloysius

Member
Joined
Mar 1, 2011
Posts
80
Reaction score
9
Je wajua kuwa una haki ya Kumshtaki Wakili wako Mzembe
Ni bahati mbaya kuwa wanasheria ndiyo waelimishaji washeria, hivyo basi nivigumu kukuta wanatoa elimu inayowanyooshea vidole.

Kupitia mwanya huu, baadhi ya Mawakili, ambao bila shaka ni wachache wamekua Mamwinyi dhidi ya wateja wao, wakifahamu wazi kuwa wateja hawajui haki zao dhidi yao.

Mambo ambayo yanalalamikiwa haswa na wananchi wengi dhidi ya baadhi ya wanasheria wasiyo heshimu miko ya sheria ni pamoja na:-

1. Uzembe na au kupuuza kesi za wateja hasa pale ambapo wamekwisha bugia pesa za mteja

2. Kuwazunguka wateja na kuwa kitu kimoja na upande mwingine kwa namna ambayo ina muumiza mteja

3. Kutokuwa makini katika kuandaa kesi ya mteja jambo ambalo linapelekea kesi kuwekewa pingamizi na kumuumiza mteja

Katika hili, sheria haiko kimya, Kuna sheria inayoongoza shughuli za wanasheria maarufu kama, The Advocates Act, R.E 2002. Sheria hii inainisha miiko kadha wa kadha ambayo Mwanasheria ni sharti aifate katika kuendesha kesi ya mteja.

Miiko hiyo ikivunjwa kipo chombo ambacho mwananchi anapaswa kumlalamikia wakili ambacho kwa bahati nzuri ni cha haki mno, kinaitwa Tanganyika Law Society ama kwa kifupi TLS.

Mwananchi usikubali kupoteza haki yako kwa kuwa hujui ni hatua gani uchukue dhidi ya wakili wako, kimbilia TLS, kwani TLS ni kimbilio la haki. Chukua hatua.

Angalizo: Usiwe mwepesi kufikia uamuzi kuwa wakili wako anastahili kulalamikiwa katika chombo hicho, subira huvuta heri.

Makala hii imeandaliwa na:
Aloys Rugazia
Afisa Sheria
MARS Legal Consultants
P.O Box 6445, Dar es Salaam
Kinondoni, Email: marslegalconsultants@outlook.com
Ujumbe Mfupi: +255 654323268
 
Je wajua kuwa una haki ya Kumshtaki Wakili wako Mzembe
Ni bahati mbaya kuwa wanasheria ndiyo waelimishaji washeria, hivyo basi nivigumu kukuta wanatoa elimu inayowanyooshea vidole. Kupitia mwanya huu, baadhi ya Mawakili, ambao bila shaka ni wachache wamekua Mamwinyi dhidi ya wateja wao, wakifahamu wazi kuwa wateja hawajui haki zao dhidi yao. Mambo ambayo yanalalamikiwa haswa na wananchi wengi dhidi ya baadhi ya wanasheria wasiyo heshimu miko ya sheria ni pamoja na:-
1. Uzembe na au kupuuza kesi za wateja hasa pale ambapo wamekwisha bugia pesa za mteja
2. Kuwazunguka wateja na kuwa kitu kimoja na upande mwingine kwa namna ambayo ina muumiza mteja
3. Kutokuwa makini katika kuandaa kesi ya mteja jambo ambalo linapelekea kesi kuwekewa pingamizi na kumuumiza mteja
Katika hili, sheria haiko kimya, Kunasheria inayoongoza shughuli za wanashesheria maarufu kama, The Advocates Act, R.E 2002. Sheria hii inainisha miiko kadha wa kadha ambayo Mwanesheria ni sharti aifate katika kuendesha kesi ya mteja. Na miiko hiyo ikivunjwa kipo chombo ambacho mwananchi anapaswa kumlalamikia Wakili ambacho kwa bahati nzuri ni cha haki mno, kinaitwa Tanganyika Law Society ama kwa kifupi TLS. Mwananchi husikubali kupoteza haki yako kwakua hujui ni hatua gani uchukue dhidi ya Wakili wako, kimbilia TLS, kwani TLS ni kimbilio la haki. Chukua hatua.
Angalizo: Husiwe mwepesi kufikia uamuzi kuwa Wakili wako anastahili kulalamikiwa katika chombo hicho, subira huvuta heri!

Makala hii imeandaliwa na:
Aloys Rugazia
Afisa Sheria
MARS Legal Consultants
P.O Box 6445, Dar es Salaam
Kinondoni, Email: marslegalconsultants@outlook.com
Ujumbe Mfupi: +255 654323268

Wanasheria katika nchi hii wamepoteza mwelekeo. Hawazingatii kabisa code of ethics. Wanawazunguka wateja wao wakitaka kujineemesha.

Kwa upande wa Tanganyika Law Society ndio zero kabisa. Chama hiki kimepoteza mwelekeo. Hatusikii makeke yake kama zamani. Juzi kilishambuliwa na Tundu Lissu kwenye mdahalo mmoja hivi kuhusu jinsi ambavyo kimekaa kimya kuhusu mchakato wa Katiba mpya. Kiongozi wake mmoja akasema wanashughulikia suala la kutaka kwenda mahakamani kupata tafsiri ya vifungu kadhaa vya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Alienda mbali zaidi na kusema kwamba angetoa mlishonyuma baada ya siku mbili lakini sasa ni mwezi hakuna kitu.

Kile kitengo cha msaada wa kisheria cha chuo kikuu cha Dar es Salaam sijui nacho kilifilia wapi!!

 
Mr Aloysius sidhani kama mamlaka ya nidhamu iko tanganyika law society tu, kuna Advocates Discplinary Committee ambayo inakuwa presided na jaji wa mahakama kuu na huwa inakuwa na wajumbe watatu i think,hii husikiliza mashauri yote yanayohusu misconduct ya mawakili,kama wakili hajaridhika sheria imeelekeza ngazi ya rufaa,vilevile unaweza kufungua civil case kwenye aspect ya proffessional negligence{tort} kudai fidia,hii iliwahi kumkuta lamwai alipoacha kuhudhuria mahakamani kesi ya mteja wake ikafutwa, na vile vile jaji wa mahakama kuu ana uwezo wa kum~suspend wakili pale anapoona clear fraud, just do your homework and advise the proper way for your client to pursue
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom