PostGE2025 Sheria Kandamizi zilivyominya Uhuru wa Habari na Wanahabari wakati wa Uchaguzi Mkuu 2025

PostGE2025 Sheria Kandamizi zilivyominya Uhuru wa Habari na Wanahabari wakati wa Uchaguzi Mkuu 2025

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Ghwema

Member
Joined
Dec 6, 2025
Posts
7
Reaction score
7
Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 nchini Tanzania uliingia kwenye vitabu vya historia si kwa wingi wa Wapiga Kura bali kwa mazingira magumu yaliyozunguka uhuru habari na uhuru wa maoni.

Ibara za 18 na 19 za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinatoa uhuru wa wa maoni na habari, lakini kilichotokea Oktoba 29, 2025 ni kinyume chake, kwani vyombo vya habari na wananchi kwa jumla walijikuta katika mtego wa kutumia uhuru huo kutekeleza majukumu yao.
fetty 2(2).jpg
Kuminywa huko kulitokana na hatua ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuzima intaneti baada ya kuibuka kwa maandamano ya kupinga uchaguzi huo.

Hapo ndipo waandishi wa habari waliposhindwa kutuma habari na hata ucjhakataji wa habari kwenye vyumba vya habari ulishindikana.

TCRA pia ilitoa maelekezo kwa radio na televisheni kuhusu habari za kutangaza na zipi zisitangazwe. Huko ni kuwanyima haki wananchi kupata taarifa.

Sheria kandamizi
Kudorora kwa uhuru wa habari kumechochewa na mfumo wa kisheria uliowekwa kimkakati ili kudhibiti ukweli, mfano sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016 na Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Maudhui ya Mtandaoni) za Mwaka 2020 (zinazojulikana kama EPOCA).

Kifungu cha 7 cha Sheria ya Huduma za Habari (2016) kinatoa mamlaka makubwa kwa Serikali kuzuia uchapishaji wa habari zinazoonekana kuhatarisha usalama wa Taifa au maslahi ya umma maneno ambayo yamekuwa yakitumiwa kwa tafsiri pana sana ili kufungia magazeti yanayochokonoa siri za serikali wakati wa uchaguzi.

Aidha, Kifungu cha 50 na 54 cha sheria hiyo hiyo vinatoa adhabu kali za jinai kwa Waandishi wa Habari, jambo linalowafanya Wahariri kuishi kwa hofu ya kufungwa gerezani au kutekwa na kupotezwa kwa kosa la kutoa taarifa za ukweli zisizoipendeza mamlaka.

Vilevile, kupitia Kanuni za Maudhui ya Mtandaoni (EPOCA), Serikali imetumia Kifungu cha 16 kinacholazimisha watoa huduma za Mtandaoni kama JamiiForums.com kuhifadhi na kutoa taarifa za watumiaji wao pindi zinapohitajika na vyombo vya usalama.

Wakati wa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025, Jukwaa la JamiiForums.com lilikuwa ni mhanga wa Sheria na Kanuni hizo, jukwaa hilo likikabiliwa na shinikizo la kisheria la kuwafichua watu wanaotumia majina ya bandia kutoa siri za ubadhirifu wa fedha za umma au njama za kuvuruga uchaguzi.

Kutokana na msimamo wao JF wa kulinda faragha ya mtoa habari kulingana na misingi ya uandishi, jukwaa limejikuta likipambana na vitisho vya kufungiwa na faini kubwa, jambo ambalo limezifanya kurasa nyingine nyingi za habari Mtandaoni kuingia kwenye nidhamu ya woga na kuacha kuandika habari za uchunguzi.

Licha ya kupambana na vitisho vya kufungiwa waliendelea kutoa taarifa kupitia jukwaa lao, taarifa zao hazikuwapendeza mamlaka na watawala kitendo kilichochangia kufungiwa kwa miezi mitatu kuanzia Septemba 6 hadi Disemba 6, 2025.

Adhabu hiyo kwa JamiiForums.com ilitoka kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), hali hii ilizua uwoga kwa majukwaa mengine na kufanya kuripoti habari za upande mmoja ili kuepuka adhabu hii zaidi kufungiwa kwa majukwaa yao, kitendo hiki kilisababisha kudidimizwa kwa uhuru wa habari na Vyombo vya Habari wakati wa Uchaguzi wa Mwaka 2025.
FETTY PICS(1).png
Ukatili
Huwezi kuzungumzia Uchaguzi wa 2025 bila kugusa vitendo vya kikatili vilivyolenga kuzima sauti za watu. Tofauti na miaka ya nyuma ambapo watu walikamatwa na kufikishwa mahakamani, safari hii mbinu imekuwa ni watu kupotea, kutekwa na kuuwawa.

Tumeshuhudia kupotea kwa watu akiwemo aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Temeke, Deusdedith Soka na kada mwingine wa chama hicho, Mdude Mpaluka Nyagali aliyekuwa akiishi jijini Mbeya, ambao kwa nyakati tofauti walitekwa na kupotezwa, hali iliyozua hofu kwa wananchi.


Kudorora kwa uhuru wa habari na uanaharakati wakati wa uchaguzi wa mwaka 2025

Kuelekea na wakati wa mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025, kuta za uhuru wa habari zimeonyesha nyufa za wazi kupitia matukio ambayo hayajawahi kushuhudiwa kwa kiwango hiki huko nyuma.

Kwanza kumekuwa na kujidhibiti na nidhamu ya woga, ambapo vyombo vya habari vimeacha kufanya kazi ya uchunguzi na badala yake vimegeuka kuwa vipaza sauti vya kuripoti matukio ya upande mmoja.

Waandishi wa kawaida pamoja na Wahariri wengi, kwa hofu ya kufungiwa au kufutiwa leseni kupitia Sheria kandamizi, wameamua kunyamazia habari zenye ukosoaji.

Kumekuwa pia na matumizi ya faini na vitisho vya kisheria kupitia Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) na Idara ya Habari Maelezo kutoa adhabu ambazo zina lengo la kudhoofisha vyombo vya habari kiuchumi na kisaikolojia.

Mfano, Majukwaa ya habari mtandaoni na vituo vya redio vimejikuta vikipewa barua za onyo kali au faini kwa kosa la kuruhusu msikilizaji au mchangiaji kutoa maoni yanayokosoa utendaji wa viongozi wa juu wakati wa kampeni.

Kumekuwa pia na udhibiti wa teknolojia na mawasiliano ya Kidijitali katika kilele cha uchaguzi wa 2025.

Hii inahusisha kupunguza kasi ya mtandao na kuingilia kurasa za wanaharakati maarufu mitandaoni na kuzifungia ili wasiendelee kutoa habari ambazo vyombo vya habari vinazuiwa kutoa na viongozi wa nchi.

Mazingira ya hatari kwa usalama wa waandishi na wanaharakati kwa kuwateka na kuwapoteza ikiwa wataonekana kuwa na msimamo mkali dhidi ya mfumo uliopo.

Nini Kifanyike?
Serikali lazima iunde Tume Huru ya Uchunguzi na iongozwe na majaji wasiokuwa na upande, jukumu lao kubwa mojawapo iwe ni kujua walipo wote waliotekwa au kupotea katika mazingira tata.

Kufuta Kanuni Kandamizi za Maudhui ya Mtandaoni, Serikali iache kutumia TCRA kama chombo cha Polisi. Pia, Vyombo vya Habari vya Mtandaoni na majukwaa kama JamiiForums.com yaachwe yafanye kazi kwa uhuru. Sheria ilinde faragha za watu badala ya kumlazimisha mtoa huduma kutoa siri za mteja wake.

Waandishi wa Habari lazima wakatae kuwa wasemaji wa Wanasiasa, taaluma yao inapaswa kuwa daraja kati ya kiongozi na Mwananchi. Ikiwa mwananchi anaumia kwa gharama kubwa za maisha, mwandishi asisite kuandika ukweli huo kwa hofu
Kudorora kwa uhuru wa habari na uanaharakati nchini Tanzania wakati wa uchaguzi wa 2025 ni donda ambalo lisipotibiwa litaoza.

Taifa linaloongozwa kwa hofu haliwezi kupata maendeleo ya kweli. Maendeleo si barabara na madaraja pekee, bali ni utu na uhuru wa mwananchi kusema kile kilicho moyoni mwake bila kuwaza kama atafika nyumbani salama.

Ni lazima turudi kwenye misingi ya katiba yetu na kuheshimu utu wa kila mmoja, bila kujali itikadi za kisiasa. Huu ndio wakati wa viongozi kuonyesha ukomavu na kuruhusu nuru ya ukweli iangaze taifa letu.

TUNASISITIZA WATANZANIA WANASTAHILI CHAGUZI HURU, SALAMA NA ZENYE KUHESHIMU HAKI ZA BINADAMU. SAUTI ZET
 
Back
Top Bottom