sheria mpya ya mafao yazidi kuleta balaa uzalishaji wasimama kabisa KMCL

kwa wafanya kazi wengine inakula kwao, make wafanya kazi wengine ni kama hawana uchungu na hizo pesa na wanabakia kulalamikia mitaani tu,

Penye wengi pana mengi sasa kama mnafanya kazi yenye watu wanne hata mkipiga kelele nani atasikia, kwenye sekta ya madini kuna kundi kubwa ambalo lina nguvu ya kusikika pia kwa wafanyakazi wengine tatizo namna ya kuji-organize ndio changamoto maana ofisi zingine huwa hazipo katika vyama vya wafanyakazi vyovyote hasda watu wanaofanya kwenye NGO kelele zao ni humuhumu JF
 

Yaani hii issue inaniumiza kichwa maana wengine tumeshazoea ajira zetu za mikataba unapiga kazi kama wataongeza mkataba ukafikisha miaka 5 wakikutosa unatafuta nyingine ukikosa unaingia NSSF unavuta chako unakuwa mjasiamali. Kiukweli hawajatenda haki na hakuna mtu asiependa kuchangia hela ila lazima uwepo utaratibu in case kama mtu hajapata kazi kwa miezi kadhaa achukue chake. Ile hoja ya kutumia fedha zetu tulizochangia kama dhamana ya mkopo nilipenda lakini walipogusa huu upande wa ukomo nikachoka kabisa. MBONA WABUNGE HAWAJAWABANA AU WAO SIO WATANZANIA, HAPA NDIPO KWA KUWASHINDIA
 
Mimi nasubiri wabadilishe nikachukue changu na kazi yao sitaki tena!nataka changu!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…