Sheria ndani ya dini ya Kikristo (Mahakama)

Kazi kwelikweli...Ndiyo maana wengine tunasema hata kama ni Dini basi mjaribu kwenda na wakati. Kuna sehemu imeandikwa na mwanaume naye lazima awe bikira au ni wanawake tu? Mbona wanawake wanakandamizwa sana kwenye mfumo wenu? Hebu niambie, utajuaje mwanamke ni bikira mara ya kwanza ukifinya naye tendo la ndoa? Najua utasema ni lazima anatoke damu kidogo anapopoteza ubikra wake. Lakini ubikira maana yake ni mara ya kwanza kuanza kufanya kile kitendo. Wasichana wengine wanapoteza ubikira hata kwenye michezo na wengine wamezaliwa bila hata ya kuwa na hymen.
Lijitu linaweza kuoa halafu likampa talaka mke wake mpya kwa sababu siyo bikira kumbe ni bikira kweli.
Hii kitu imewafanya dada zenu wengi kufanya tendo la ndoa kinyume na maumbile kuilinda hiyo bikira.
Badilikeni bana!

mkuu sikuhitaji longolongo nyingi sana,na majibu ya watu wa njiani,ila nimelenga suali katika sheria za dini ,zinasemaje ? sasa kama mtu kapanda baiskeli huko ni kwengine ,suali lipo palepale juu ya yale niliyoyahitajia ,sheria kwa upande wa dini zinasemaje .
 
Kadhi courts are special for brain dead idiot religion.

kama huna majibu ni bora ukajikalia kimya kuliko kujitanua kutukana wala haikusaidii kitu. muulizaji anataka kujifunza wewe kama una elimu mfundishe. ivi ukimjibu usahihi utaharibikiwa nini?
 
God wanted Israelite to maintain the best breed of animals they had.
My be because from the breed they were get more milk an meat.
crossing with the breed they dont know might have degenerated the best breeds of their animals.
Hapa si mahali pake thought.
Na kweli sheria hii sizo katika yale mambo niliohitajia ,ambayo yanaigusa jamii ,
 
Kazi kwelikweli...Ndiyo maana wengine tunasema hata kama ni Dini basi mjaribu kwenda na wakati. Kuna sehemu imeandikwa na mwanaume naye lazima awe bikira au ni wanawake tu? Mbona wanawake wanakandamizwa sana kwenye mfumo wenu? Hebu niambie, utajuaje mwanamke ni bikira mara ya kwanza ukifinya naye tendo la ndoa? Najua utasema ni lazima anatoke damu kidogo anapopoteza ubikra wake. Lakini ubikira maana yake ni mara ya kwanza kuanza kufanya kile kitendo. Wasichana wengine wanapoteza ubikira hata kwenye michezo na wengine wamezaliwa bila hata ya kuwa na hymen.
Lijitu linaweza kuoa halafu likampa talaka mke wake mpya kwa sababu siyo bikira kumbe ni bikira kweli.
Hii kitu imewafanya dada zenu wengi kufanya tendo la ndoa kinyume na maumbile kuilinda hiyo bikira.
Badilikeni bana!

sweke siamini kama umemuelewa mtoa mada. Naomba ninukuu alichotaka kujua

"Naulizia tu ,je ndani ya dini ya kikristo zimo sheria ,mfano sheria za kumhukumu mwizi endapo atakamatwa,sheria za mwanamke iwapo atazini au ataonekana sio bikira siku ya mwanzo ya kukutana na mumewe ikiwa hajawahipo kuolewa,sheria za mavazi kwa wanawake na hata waume ,sheria zinazohusiana na urithi.kama zipo mnaweza kuziorodhesha mbili tatu hapa,ili tupate muongozo au ufunuo.Na je hapa duniani ipo mahakama yeyote ya kikiristo."

Mie nilitegemea wewe kama mtaalam wa biblia unakuja kufundisha kwa mujibu wa kitabu chako. Mie naamini wewe ni mchungaji na ninavyojua mchungaji ni mwalimu sasa kwanini usifundishe wasiojua biblia nao wakapata kuijua? why?
 
Kwa mjibu wa Biblia, Mkristo anafuata amri alizopewa na Mungu. Na anakuwa amekosea pale anapokuwa ameenda kinyume na maagizo aliyopewa na Mungu wake. Pia suala la huku si la kibinadamu bali Mungu kwa maana ni sheria za rohoni ambazo Mungu anaziona kuliko binadamu.

Hivyo, Mkristo anafanya vile kwa kumpendeza Mungu si binadamu.

Yafaa nini tuhukumu kama bado hataona mbingu na sheria za Mungu zi wazi kwa wale wampendao?
 
Naulizia tu ,je ndani ya dini ya kikristo zimo sheria ,mfano sheria za kumhukumu mwizi endapo atakamatwa,sheria za mwanamke iwapo atazini au ataonekana sio bikira siku ya mwanzo ya kukutana na mumewe ikiwa hajawahipo kuolewa,sheria za mavazi kwa wanawake na hata waume ,sheria zinazohusiana na urithi.kama zipo mnaweza kuziorodhesha mbili tatu hapa,ili tupate muongozo au ufunuo.Na je hapa duniani ipo mahakama yeyote ya kikiristo.

Naona kuna msukumo wa kujadili kisiasa ndani maamuzi ya dini ya kiislamu kutaka iwepo mahakama ya kadhi ,je na wenzetu ndugu zetu wa karibu kabisa wa dini ya kikristu ,nao iwapo wanazo sheria wanaweza kuanzisha mahakama ambayo itaweza kushughulikia misingi ya sheria za dini yao.
Naomba kuwakilisha hoja na natanguliza samahani ikiwa itaonekana nimemgusa mtu.

Bwana wetu YESU KRISTU alisema, Ya Mungu mpe/muachie Mungu na ya Kaisari mpe kaisari.
Mtume wetu Paulo alisema, asiyefanya kazi asile, siyo aombewe.
Hivo basi, ni kweli tuna mahamaka, lakini ni ya kiroho ambayo Hakimu ni Mungu mwenyewe maana yeye ndio huona na hujua kila kitu tufikiriacho.
Tafakari mkuu: And Jesus told them "....He that is without sin among you, let him first cast a stone at her" John 8:7
So, what for hiyo kadhi?
 
Naulizia tu ,je ndani ya dini ya kikristo zimo sheria ,mfano sheria za kumhukumu mwizi endapo atakamatwa,sheria za mwanamke iwapo atazini au ataonekana sio bikira siku ya mwanzo ya kukutana na mumewe ikiwa hajawahipo kuolewa,sheria za mavazi kwa wanawake na hata waume ,sheria zinazohusiana na urithi.kama zipo mnaweza kuziorodhesha mbili tatu hapa,ili tupate muongozo au ufunuo.Na je hapa duniani ipo mahakama yeyote ya kikiristo.

Naona kuna msukumo wa kujadili kisiasa ndani maamuzi ya dini ya kiislamu kutaka iwepo mahakama ya kadhi ,je na wenzetu ndugu zetu wa karibu kabisa wa dini ya kikristu ,nao iwapo wanazo sheria wanaweza kuanzisha mahakama ambayo itaweza kushughulikia misingi ya sheria za dini yao.
Naomba kuwakilisha hoja na natanguliza samahani ikiwa itaonekana nimemgusa mtu.

Mwiba,

Bahati mbaya sana huwa ni vigumu kupata michango "sane" unapouliza swali lolote la kidini kwani watu wanakuwa "emotional" inapokuja kwenye masuala haya ya kidini.

Kimsingi katika ukristo kuna mifumo ya kutatua matatizo kwa usuluhishi. Ukifuatilia sana historia ya ukristo utagundua kuwa huko nyuma sana kuna wakati dini na utawala viliunganika, kama wanavyounganisha dini na utawala waislam. Katika enzi hizo, papa ndo alikuwa anakuwa emperor. Hata hivyo mfumo huo ulileta mikanganyiko mikubwa sana kwani migogoro ya kisiasa na kijamii iliingia sana katika kazi za kanisa kiasi kuwa viongozi wa kanisa walipoteza kabisa mwelekeo kwenye mambo ya kiimani na kuzama zaidi kwenye siasa na jamii. Matokeo yake hayakuwa mazuri sana kwani mapapa wengi walipoteza heshima yao mbele ya jamii na upinzani ukawa mkubwa.

Hapo ndo kukazaliwa mfumo wa usekulari, kuwa dini na uongozi wa mambo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa vitenganishwe. Mfumo wa mahakama ukaonekana si suala la kiimani kwa hivyo mahakama zikaondoka. Ndani ya madhehebu mengi ulibaki mfumo wa utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi; si kimahakama. Mahakama za kanisa zinazozungumziwa kwa mfano katika ukatoliki ni kwa ajili ya kushughulikia matatizo ya viongozi na watendaji ndani ya kanisa "clergy" na si matatizo ya waumini. Matatizo ya waumini yameachwa kushughulikiwa na mfumo wa mahakama za kawaida ambazo katika usekulari zinakuwa ndani ya mifumo ya utawala ambayo ni nje ya kanisa.

Hivyo, katika ukristo, kuna usuluhishi na mabaraza ya usuluhishi, si mahakama kwa maana ya mahakama kwa sababu maamuzi yake hubaki kuwa wazi kwa wale wanaosuluhishwa kuyakubali au kuyakataa.
 
Uislam na Ukristo je ni kama vyama vya siasa? Dini ya kristo haina haja kushindana na dini ya Kiislam kwa kua utaratibu wa mafunzo na imani ni tofauti pia.

Waislam wana uhuru wote chini ya TZ huru hivyo wafanye ya kwao, nao wasiingilie imani ya watu wengine. Lakini hua nashindwa kuelewa chombo hasa kinachowaongoza waislam TZ ni kipi? Hicho chombo kama kipo ndio kichukue jukumu la kuendesha MAHAKAMA YA KADHI kwa michango toka kwa waislam ama miradi yao ama misaada.

Foreign policy ya China haitofautiani sana na matamanio ya kiislam kwa watu wasio waislam - and you can not trust any of them.
 
Kazi kwelikweli...Ndiyo maana wengine tunasema hata kama ni Dini basi mjaribu kwenda na wakati. Kuna sehemu imeandikwa na mwanaume naye lazima awe bikira au ni wanawake tu? Mbona wanawake wanakandamizwa sana kwenye mfumo wenu? Hebu niambie, utajuaje mwanamke ni bikira mara ya kwanza ukifinya naye tendo la ndoa? Najua utasema ni lazima anatoke damu kidogo anapopoteza ubikra wake. Lakini ubikira maana yake ni mara ya kwanza kuanza kufanya kile kitendo. Wasichana wengine wanapoteza ubikira hata kwenye michezo na wengine wamezaliwa bila hata ya kuwa na hymen.
Lijitu linaweza kuoa halafu likampa talaka mke wake mpya kwa sababu siyo bikira kumbe ni bikira kweli.
Hii kitu imewafanya dada zenu wengi kufanya tendo la ndoa kinyume na maumbile kuilinda hiyo bikira.
Badilikeni bana!

Wewe hujui chochote kuhusu Uislam haya uliyoandika sijui umeyapata wapi...wewe jibu mleta mada kauliza sheria ndani ya dini ya Kikristo.
 
Mwiba,

Bahati mbaya sana huwa ni vigumu kupata michango "sane" unapouliza swali lolote la kidini kwani watu wanakuwa "emotional" inapokuja kwenye masuala haya ya kidini.

Kimsingi katika ukristo kuna mifumo ya kutatua matatizo kwa usuluhishi. Ukifuatilia sana historia ya ukristo utagundua kuwa huko nyuma sana kuna wakati dini na utawala viliunganika, kama wanavyounganisha dini na utawala waislam. Katika enzi hizo, papa ndo alikuwa anakuwa emperor. Hata hivyo mfumo huo ulileta mikanganyiko mikubwa sana kwani migogoro ya kisiasa na kijamii iliingia sana katika kazi za kanisa kiasi kuwa viongozi wa kanisa walipoteza kabisa mwelekeo kwenye mambo ya kiimani na kuzama zaidi kwenye siasa na jamii. Matokeo yake hayakuwa mazuri sana kwani mapapa wengi walipoteza heshima yao mbele ya jamii na upinzani ukawa mkubwa.

Hapo ndo kukazaliwa mfumo wa usekulari, kuwa dini na uongozi wa mambo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa vitenganishwe. Mfumo wa mahakama ukaonekana si suala la kiimani kwa hivyo mahakama zikaondoka. Ndani ya madhehebu mengi ulibaki mfumo wa utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi; si kimahakama. Mahakama za kanisa zinazozungumziwa kwa mfano katika ukatoliki ni kwa ajili ya kushughulikia matatizo ya viongozi na watendaji ndani ya kanisa "clergy" na si matatizo ya waumini. Matatizo ya waumini yameachwa kushughulikiwa na mfumo wa mahakama za kawaida ambazo katika usekulari zinakuwa ndani ya mifumo ya utawala ambayo ni nje ya kanisa.

Hivyo, katika ukristo, kuna usuluhishi na mabaraza ya usuluhishi, si mahakama kwa maana ya mahakama kwa sababu maamuzi yake hubaki kuwa wazi kwa wale wanaosuluhishwa kuyakubali au kuyakataa.

Nimekufahamu vizuri sana na umenipa muongozo ambao ni mzuri na upo wazi,sijui nimekuelewa ndivyo kuwa waumini huwa mnafanya mnayotaka na kanisa halina nguvu ya kukuingilia au kukuhukumu ,hii namaanisha pale nilipohitajia yale mambo ambayo nilitaka maelezo kuhusiana na sheria za dini kwa upande wa ukiristo.

Kwa mfano wanawake wa kiislamu wanatakiwa kujihifadhi sehemu za mwili wao kinyume atakuwa au anahesabika anakenda uchi na hawezi kufanya ibada akiwa hivyo ,ila wanakwenda na wanavaa vimini na nguo zinazoonyesha sehemu na nguo za kubana mwili,ndani ya nchi inayofuata sgeria za kiislamu mwananmke huyo haruhusiki na akionekana atafikishwa mahakamani ,kwa sababu ni kosa ,jingine haruhusiwi kufanya ibada au kuingia sehemu za ibada akiwa katika hali hiyo.

Suali ni vipi katika ukiristo tuseme hili vazi lina sehemu yake au sheria zake na hata kufanya ibada au kuingia katika sehemu za ibada ,mapdre na waendesha ibada wa kikristo wanawaelimisha waumini wao au ni free mtu kuingia katika sehemu ya ibada labda kanisani akiwa na amevalia mini ,makwapa wazi V ya kutenganisha matiti inaonekana and something like that ambayo kwayo inaweza kumsababishia padre asiweze kurudisha macho upande ulioko vituko hivyo.
 
Kwa mjibu wa Biblia, Mkristo anafuata amri alizopewa na Mungu. Na anakuwa amekosea pale anapokuwa ameenda kinyume na maagizo aliyopewa na Mungu wake. Pia suala la huku si la kibinadamu bali Mungu kwa maana ni sheria za rohoni ambazo Mungu anaziona kuliko binadamu.

Hivyo, Mkristo anafanya vile kwa kumpendeza Mungu si binadamu.

Yafaa nini tuhukumu kama bado hataona mbingu na sheria za Mungu zi wazi kwa wale wampendao?

Kwahiyo kaka kwa mtizamo huo, haitupasi sisi watanzania kuwahukumu mafisadi, wauza madawa la kulevya, wauaji wa aribino,etc? kama siyo hivyo basi mtoa mada anataka kujua mfano nini hukumu iliyoelezwa kwa mujibu wa mafundisho ya kikristo kuwa mtu akiiba nini afanywe?
 
imeandikwa
"basi ukipeleka sadaka yako mbele ya madhabahu na hapo ukakumbuka kwamba ndugu yako ana ugomvi nawe, iache sadaka yako mbele ya madhabahu, nenda kwanza ukapatane na ndugu yako, ndipo urudi utolee sadaka yako" matayo 5:23-24

mat5:38-39
"mmesikia kwamba imesemwa: "jicho kwa jicho, jino kwa jino" Lakini mimi nawaambieni, usimlipize kisasi mtu mbaya. Mtu akikupiga kofi shavu la kulia, mgeuzie pia la pili."

mat 5:44
lakini mimi nawaambieni, wapendeni adui zenu na kuwaombea wale wanaowadhulumu nyinyi, ili mpate kuwa watoto wa Baba yenu aliye mbinguni. Maana yeye huwaangazia jua lake watu wabaya na wema, na kuwanyeshea mvua watu wanyofu na waovu.

mat 6:1-2
jihadaharini msije mkafanya matendo yenu mema mbele ya watu kusudi muonekane nao. Basi unapomsaidia masikini usijitangaze. Usifanye kama wanafiki wafanyavyo kwenye masunagogi na njiani ili watu wawas
ifu.

mathayo 6:6
lakini wewe unaposali, ingia chumbani mwako, funga mlango, kisha umwombe Baba yako asiyeonekana. Naye Baba yako aonae yaliyofichika, atakutuza.

mnapofunga, msiwe na huzuni kama wanafiki. wao hukunja nyuso zao wapate kuonekana na watu kuwa wanafunga mat 6:16

mat 7:1
msiwahukumu wengine msije nanyi mkahukumiwa na Mungu;kwa maana jinsi mnavyowahukumu wengine ndivyo nanyi mtakavyohukumiwa; na kipimo kile kile mnachotumia kwa wengine ndicho Mungu atakachotumia kwenu.

ndiyo maana nawaambieni, msiwe na wasiwasi juu ya chakula na kinywaji mmnavyovihitaji ili kuishi, wala juu ya mavazi mnayohitaji kwa ajili ya miili yenu. Je maisha ni zaidi ya chakula tu au zaidi? na mwili je si zaidi ya mavazi?

Yesu akawajibu, "Mose aliwaruhusu kuwaacha wake zenu kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu. Lakini haikuwa hivyo tangu mwanzo mat 19:7

"basi, ya Kisari mpeni Kaisari, na ya Mungu mpeni Mungu ....mat 22:21

mathayo 22:37-40
"mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote" hii ndiyo amri kuu ya kwanza. Ya pili inafanana na hiyo "mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe. sheria yote ya Mose na manabii vinategemea amri hizi.

Naulizia tu ,je ndani ya dini ya kikristo zimo sheria ,mfano sheria za kumhukumu mwizi endapo atakamatwa,sheria za mwanamke iwapo atazini au ataonekana sio bikira siku ya mwanzo ya kukutana na mumewe ikiwa hajawahipo kuolewa,sheria za mavazi kwa wanawake na hata waume ,sheria zinazohusiana na urithi.kama zipo mnaweza kuziorodhesha mbili tatu hapa,ili tupate muongozo au ufunuo.Na je hapa duniani ipo mahakama yeyote ya kikiristo.

Naona kuna msukumo wa kujadili kisiasa ndani maamuzi ya dini ya kiislamu kutaka iwepo mahakama ya kadhi ,je na wenzetu ndugu zetu wa karibu kabisa wa dini ya kikristu ,nao iwapo wanazo sheria wanaweza kuanzisha mahakama ambayo itaweza kushughulikia misingi ya sheria za dini yao.
Naomba kuwakilisha hoja na natanguliza samahani ikiwa itaonekana nimemgusa mtu.

ndugu,
ukristo hauchangamani na siasa, ukristo ni kufuata neno la Mungu....kuliishi na kulifuata....kufuata maandiko.....

ya utawala wa dunia hii yanaachiwa utawala wa dunia hii,
hakuna sheria, kuna amri 10 zinazobase katika amri kuu... na amri kuu ni upendo.....
kukiwa na upendo hakutakuwa na mifarakano, choyo, vita nk nk nk

hatuhukumu, jukumu la kuhukumu ni la Mungu pekee.....
ila kila mmoja ana wajibu wa kumfundisha neno mwenzie.....
kila mmoja ana wajibu wa kuishi kwa kufuata maandiko......si rahisi ni kazi ngumu kutokana na udhaifu wa binadamu lakini kwa imani na matumaini yanawezekana
 
Naulizia tu ,je ndani ya dini ya kikristo zimo sheria ,mfano sheria za kumhukumu mwizi endapo atakamatwa,sheria za mwanamke iwapo atazini au ataonekana sio bikira siku ya mwanzo ya kukutana na mumewe ikiwa hajawahipo kuolewa,sheria za mavazi kwa wanawake na hata waume ,sheria zinazohusiana na urithi.kama zipo mnaweza kuziorodhesha mbili tatu hapa,ili tupate muongozo au ufunuo.Na je hapa duniani ipo mahakama yeyote ya kikiristo.

Naona kuna msukumo wa kujadili kisiasa ndani maamuzi ya dini ya kiislamu kutaka iwepo mahakama ya kadhi ,je na wenzetu ndugu zetu wa karibu kabisa wa dini ya kikristu ,nao iwapo wanazo sheria wanaweza kuanzisha mahakama ambayo itaweza kushughulikia misingi ya sheria za dini yao.
Naomba kuwakilisha hoja na natanguliza samahani ikiwa itaonekana nimemgusa mtu.

KRISTO alituachia sheria, sheria zinazojali utu wa mtu. alitoa amri kuu mbili, yaani kumpenda Mungu na kumpenda jirani yako kama nafsi yako. Ukizichambua amri hizi, yote uliyoyataja hapo juu ymeguswa.

Kuhusu mahakama, kama sehemu ya utawala, INJILI inatuagiza tuheshimu mamlaka kwani imetoka kwa MUNGU. RUM 13 FF. Hivyo kidunia katika utumishi wa haki, tuzitii mamlaka, lakini waenda mbinguni hatujishughulishi na mambo hayo.

Mfano, aliletewa mzinzi ili asimamie adhabu ya mtu aliyezini, alicho waambia, alisema yeyote asiye na dhambi na awe wa kwanza kumrushia jiwe, hakuna laiyejitokeza kwani wote walikuwa na makosa. Fundisho lile linataka tumwachie MUNGU pekee kazi ya kuhukum, binadam hatuna sababu ya kuhukum binadam wengine, kwani hata sisi ni wadhambi kila siku.

kwa mfano, nani ambaye hajawahi kuiba? nani hajawahi kuzini? nani hajawahi kusema uongo? na mengine mengi.

Ukristo ni utumishi wa rohoni siyo wa mwilini, kwani kinachotafutwa ni kuiponya roho na si mwili hata kidogo
 
Kwahiyo kaka kwa mtizamo huo, haitupasi sisi watanzania kuwahukumu mafisadi, wauza madawa la kulevya, wauaji wa aribino,etc? kama siyo hivyo basi mtoa mada anataka kujua mfano nini hukumu iliyoelezwa kwa mujibu wa mafundisho ya kikristo kuwa mtu akiiba nini afanywe?

mr mak,
kanisa halina wajibu wa kuhukumu....
amri inasema usiue... kwa hiyo litakemea mauaji....
kuhukumu ni kazi ya serikali......kumbuka ya kaisari muachie kaisari, serikali itakapoona ufisadi ni kosa kisheria, watachukua tararibu za kisheria.........

na mkosaji akija kanisani kumuomba msamaha Mungu wake, hatutomrushia mawe, maana yaliyofichika ni Mungu pekee ndiye aonae...
 
mkuu naona unatuwacha ! Nani atupiwe jiwe kwa kosa gani ? Usione shida kumwaga ukweli ni dhahiri kuwa unajua mengi lakini unabania.

hii imeandikwa kwenye bible mkuu kuwa "' Wanaume walimfumania mwanamke akizini wakamshika wakampeleka kwa Yesu ili atoe hukumu juu ya huyo mwanamke lakini Yesu baada ya kuwasikiliza akawaambia wale wanaume na asiye na dhambi awe wa kwanza kumtupia jiwe huyu mwanamke wale wanaume hiyo kauli wakaitafakari wakajiona ni wadhambi hivyo wakaondoka ,Yesu alikuwa akiandika chini "je yule mwanaume uliyekuwa nae yu wapi" yesu alipoinuka hakukuta wale wanaume hata mmoja , akamwuliza yule mwanamke je wako wapi waliokuwa wanakuhukumu ?yule mwanamke akasema wameondoka basi Yesu akamwambia nami pia sikuhukumu nenda umesamehewa dhambi zako ila usitende dhambi tena , yule mwanamke akaondoka
 
Naulizia tu ,

(1) je ndani ya dini ya kikristo zimo sheria ,mfano sheria za kumhukumu mwizi endapo atakamatwa,sheria za mwanamke iwapo atazini au ataonekana sio bikira siku ya mwanzo ya kukutana na mumewe ikiwa hajawahipo kuolewa,sheria za mavazi kwa wanawake na hata waume ,sheria zinazohusiana na urithi.kama zipo mnaweza kuziorodhesha mbili tatu hapa,ili tupate muongozo au ufunuo.

(2) je hapa duniani ipo mahakama yeyote ya kikiristo.

Naona kuna msukumo wa kujadili kisiasa ndani maamuzi ya dini ya kiislamu kutaka iwepo mahakama ya kadhi ,je na wenzetu ndugu zetu wa karibu kabisa wa dini ya kikristu ,nao iwapo wanazo sheria wanaweza kuanzisha mahakama ambayo itaweza kushughulikia misingi ya sheria za dini yao.
Naomba kuwakilisha hoja na natanguliza samahani ikiwa itaonekana nimemgusa mtu.

Ufafanuzi,

(1) Ndiyo Sheria zipo, lakini si kwa masuala kama uliyoyataja, ya hukumu za bikira, hukumu za mavazi, hukumu za urithi kama ndugu zetu waislamu walivyo na Sharia. Sheria zilizopo mfano za Roman Catholic zinajulikana kwa jina la Canon Law, hizi ni mahususi kwa ajili ya uendeshaji wa kanisa na usimamizi wa kile ambacho kanisa limejenga misingi yake, zinashughulikia masuala ya ndoa (uhalali wa ndoa, maana ya ndoa, wakati gani ndoa inaweza kubatilishwa, utaratibu wa kubatilisha ndoa na nani anabatilisha), utaratibu wa kuchagua watumishi wote wa kanisa kuanzia wa chini hadi Papa pamoja na wajibu na majukumu yao. kwa kifupi ni sheria zinazolinda imani ya kanisa Catholic na kuweka misingi ya makubaliano ya nini cha kufanya. Kwa misingi ya mada yako sheria za kuhukumu watu ziko kwenye Mamlaka za Tawala husika (Kaisari), na mambo yanayohusu kanisa yanashughulikiwa na Canon Laws

(2) Niongelee Roman Catholic - Ndiyo, hapa duniani ipo Mahakama, na inashughulikia masuala yanayohusu Kanisa, ni vyema nikasisitiza hapa kuwa Mahakama ya Kanisa haikai na kujadili nani anabikira au hana bikira wakati wa kuolewa, au nani kavaa kimini au kafunika kichwa.

Unaweza kuuliza zaidi.
 
Nimekufahamu vizuri sana na umenipa muongozo ambao ni mzuri na upo wazi,sijui nimekuelewa ndivyo kuwa waumini huwa mnafanya mnayotaka na kanisa halina nguvu ya kukuingilia au kukuhukumu ,hii namaanisha pale nilipohitajia yale mambo ambayo nilitaka maelezo kuhusiana na sheria za dini kwa upande wa ukiristo.

Kwa mfano wanawake wa kiislamu wanatakiwa kujihifadhi sehemu za mwili wao kinyume atakuwa au anahesabika anakenda uchi na hawezi kufanya ibada akiwa hivyo ,ila wanakwenda na wanavaa vimini na nguo zinazoonyesha sehemu na nguo za kubana mwili,ndani ya nchi inayofuata sgeria za kiislamu mwananmke huyo haruhusiki na akionekana atafikishwa mahakamani ,kwa sababu ni kosa ,jingine haruhusiwi kufanya ibada au kuingia sehemu za ibada akiwa katika hali hiyo.

Suali ni vipi katika ukiristo tuseme hili vazi lina sehemu yake au sheria zake na hata kufanya ibada au kuingia katika sehemu za ibada ,mapdre na waendesha ibada wa kikristo wanawaelimisha waumini wao au ni free mtu kuingia katika sehemu ya ibada labda kanisani akiwa na amevalia mini ,makwapa wazi V ya kutenganisha matiti inaonekana and something like that ambayo kwayo inaweza kumsababishia padre asiweze kurudisha macho upande ulioko vituko hivyo.

Mwiba,

Ni kweli kuna matatizo ya uvaaji kwa wanawake na wanaume pia; nguo za kubana au vimini kwa wanawake, suruali za milegezo kwa wanaume na mambo kama hayo. Lakini haya ni mambo ya kimaadili zaidi kuliko mambo ya kushughulikiwa na sheria. Makanisa mbali mbali huwa wanazo taratibu zao za kushughulika na mambo haya na hizo taratibu hutofautiana kutoka kanisa moja hadi jingine. Haya mambo ya uvaaji hayahusiani moja kwa moja na imani bali ni mambo ambayo yanaonekana kuathiriwa na mila na desturi mbali mbali.

Ni kweli kabisa kuna maeneo kuingia kanisani na mini-skirt si issue kubwa na kutokana na mila na desturi za maeneo yale kama hakuna mtu anayekuwa "offended" wanawake huwa huru kujimwaga vile wapendavyo! Hata wanaume vile vile. Kwa ninavyojua, mafundisho mengi ya ukristo huangalia mambo ya ndani zaidi kuliko mambo ya nje kama mavazi anayovaa mtu au chakula anachokula; ambayo mara nyingi hubadirika kutokana na mila, desturi na mazingira ya mahali husika. Haya si mambo ya kushughulikiwa kisheria sana. Hata jamii zinazokaa uchi kabisa wanaweza kuwa wakristo na wakaendelea kusali bila matatizo ikiwa kukaa uchi kwenye jamii husika si tatizo!! Ukristo husisitiza zaidi mambo ya upendo na ukiangalia katika amri kumi za mungu ambazo wakristo huzifuata hadi leo, uvaaji halimo katika amri hizo kumi! Hata wakatoliki ambao wanazo amri sita za kanisa bado katika zile amri sita uvaaji si mojawapo ya amri hizo!

Mambo ya kuhukumu mwizi katika ukristo si masuala ya kiimani hivyo hukumu juu ya wizi (au mambo yote ya kijinai) huchukuliwa kuwa ni mambo ya kushughulikiwa na serikali; wezi hata wakiiba sadaka au mali ya kanisa hushitakiwa katika vyombo vya sheria vya kiserikali.
 
Kuna kitu kinaitwa MORAL LAW, ambayo msingi wake ni Amri kumi za Mungu zilizoko katika TORATI: Usiibe, usizini, usiseme uwongo, Waheshimu baba na mama, nk. Yesu amezijumlisha katika Amri kuu ya Upendo. Mtu akiiba, kwa mfano, amemkosea Mungu, amemkosea huyo aliyemwibia, kaikosea jamii, na kajikosea mwenyewe katika dhamiri yake. anatakiwa kujipatanisha na nafsi yake kwa toba (kujuta na kubadilika), ajipatanishe na huyo aliyemwibia (kurejesha mali ya wizi, au kama haiwezekani kumpa huyo aliyemwibia, aitoe kwa wengine. akitoa na faini ni vizuri zaidi). pia anatakiwa kujipatanisha na jamii na Mwisho anatakiwa kujipatanisha na Mungu wake. kwa wakatoliki, mtu anapoungama kwa Padre, anajipatanisha kwa Mungu na Jamii kwa uwakilishi wa Padre. Kwa ujumla Ukristu unahimiza mabadiliko ya kiroho ya mtu, hauna vyombo vya dola vya kumshugulikia mtu anayevunja amri za Mungu. mtu akiiba, akakamatwa, anashughulikiwa na vyombo vya kiserikali. akienda kanisani akatubu, anapatanishwa na Mungu na jamii. akitubu kwa yule aliyemwibia, anajipatanisha naye.

Katika Kanisa Katoliki kuna pia sheria za Kanisa, Canon Law. hizi husimamia mambo kama ya ndoa, nk. kuna mahakama ya kanisa ambayo inasikiliza watu wanapokuwa wametofautiana, mfano katika ndoa, na kuagiza kinachotakiwa kufanyika, kwa kuangalia msimamo wa Imani. mahakama hii inaendeshwa na kanisa, inagharimiwa na kanisa, na ni kwaa ajili ya wanakanisa
 
Back
Top Bottom