kelvin bayona
Member
- Jul 18, 2022
- 16
- 8
1. Acha iende
Usije ukaharibu siku yako njema ya leo, siku yenye furaha, siku yenye nuru njema kwa sababu ya siku mbaya ya jana. Jambo linalorudisha sana watu nyuma pengine kimaendeleo, kimasomo, hama kufanya maamuzi ni kuruhusu kukumbuka siku ya jana iliyopita ambayo pengine ilikuwa mbaya kwake kwahiyo anakuwa anawaza nikurudia kosa la jana itakuwaje? Hakuna mtu ambae hakosei au kupitia wakati mbaya na mgumu hayupo katika dunia hii lakini tatizo linakuja utafanyeje hili usikumbuke mambo yaliyotokea jana? Utafanyeje hili lililotokea jana liwe funzo katika maisha na mihangaiko yako au katika kufanya maamuzi yako. Hapo watu wengi hasa vijana ndipo tunapokuja kuharibu kila kitu na kuvuruga maisha yetu ya badae kwa sababu tunaogopa kukosea, tunaogopa kilichotokea jan kisije tokea tena leo, na hii ni kwa sababu ya aibu. Kwahiyo iache jana ipite yaache makosa ya jana yawe funzo kwako.
2. Wapuuze
Usipende sana kusikiliza watu wanasema nini kuhusu wewe, ishi maisha ambayo unaona yanakupendeza wewe na yanampendeza Mungu wako hapo utaishi maisha ya amni na hutaona kama maisha ni magumu, kikubwa unachapa kazi bili kujari watu wa pembeni yako hama jirani zako hama rafiki zako wanasemaje. Kwanini usikilize maneno au watu ambao hawakuletei chakula nyumbani kwako?, kwanini usikilize maneno ya watu ambao unakutana nao mchana tu lakini usiku hawajui unalala wapi au unakula nini? Maisha ya kila mwanadamu yanategemea maisha ya mwanadamu mwingine lakini sio maisha ya mwanadamu yanategemea maneno ya mwanadamu mwingine. Mfano unakuta mtu anashindwa kujiingiza kwenye furasa ambayo anajua kabisa kuna njia ya kutokea lakini kwa sababu anasikia marafiki zake wanamsema na sababu ya kumsema wao hawajapata nafasi kwenye hiyo furusa, nakwambia kijana ukiendelea kusikiliza hayo mambo hatofika sehemu yoyote ile.
3. Toa muda
Muda huponya kilakitu. Kila kitu utakachokifanya kiwekee muda wake, toa muda kwa kila jambo unalolipanga, toa mda kwa ambalo lipo mkononi mwako unalifanya kwa sasa. Kama ilivyo kanuni ya maisha kwamba kuna muda wa kuzaliwa kuna muda wa kuishi kuna muda wa kufa pia, hapa kwenye swala la muda wa kuishi ndipo unapaswa kutumia muda wako vizuri kwasababu ukizaliwa utakua utaanza kujiusisha na shughuli hapa kwenye shughuli za maisha ndipo unapopaswa kuweka muda wako sawa hili mambo yako yote yaende vizuri. Hapa haimaanishi muda wote ufanye tu kazi au shughuli kila wakati lazima utenge muda wa kufurahia kwa kucheza kwenda ufukweni kupunga upepo, pumzisha akili yako wewe sio mashine kwamba masaa yote wiki nzima unafanya tu kazi, ukishikiria hilo la kufanya kazi mapema ndipo mda wako wa kufa unakaribia maana kuwa watu wengi wametumia muda mwingi kufanya mambo yao bila kupumzika mpaka wanakufa bado walikuwa hawajapata kile walichokuwa wanakutafuta na wamekufa kwa sababu ya kufanya kazi kupitiliza na kutokugawa muda vizuri kwa ajili ya majukumu.
4. Usijilinganishe
Kutokujilinganisha na mtu yeyote itakufanya uwe mwenye ujasiri na amani, usijaribu kujilinganisha wewe na watu wengine, wewe ni wewe na unathamani zaidi ya mtu unaejilinganisha nae. Hii tabia hasa mabinti wanaipenda sana kujilinganisha kuwa kama yule dada, utasikia mmh kule mdada anaumbo zuri natamani ningekuwq mimi, mpaka hapo unakuwa umevunjia wewe heshima umemdharau Muumba wako aliyekuumba akakupa wewe umbo hilo. Mwingine akiona mtu ana maisha fulani nayeye anatamani kuwa hivyo hivyo hata kam hana uwezo, sisemi ni vibaya kutamani kuwa na maisha kama ya mtu aliyefanikiwa lakini tamaa yako iwe ndani ya uwezo wako usitake kununua gari kwa sababu umeona mtu fulani analo wakati unapokaa pengine unadaiwa kodi au biashara yako inayumba wewe unawaza kununua tu vitu vya kifahari kwa sababu rafiki yako uliyesoma nae kanunua. Ukiacha kujilinganisha na watu wengine utajithamini na kuwa na ujasiri juu yako kuanzia kwenye maisha yako na maamuzi yako.
5. Tulia
Ni sawa tu kutokuwa na kila kitu unachokitamani kwa wakati huu, lakini niamini mimi hilo jambo kama umeandikiwa au kama ni riziki yako lazima itakuja tu hata kama itachelewa vipi, hata kama utapitia changamoto kupata hilo jambo lakini kama lakwako ni lakwako tu kikubwa ni kuweka bidii kulitafuta jambo hilo huku ukiwa unamkumbuka na Muumba wako. Vijana wengi tumekuwa watu tunaopenda mikato sana, yaani tukiona kuna sehemu ya kufanikiwa kwa mkato bila kupambana ndipo tunawekeza akili zetu na nguvu zetu zote huko kwa sababu hatutaki kujituma, lakini kama tutatulia na kufanya kazi kwa bidii ninaamini kila jambo litakaa sawa kwa wakati wake tu kikubwa tufanye kazi kwa uhalali bila dhuruma, wizi, wivu, ufisadi. Swahili upenda kusema kam hipo hipo tu kikubwa ni kuliweka akilini na kulifanyia kazi hitaji lako lifikrie kila mda ukitembea lifkrie ukiwa kwenye usafiri pengine unaenda kazini rifkrie lazima utapata tu njia ya kufanikiwa pale mda utakapokuwa umefika.
6. Ni juu yako
Wewe mwenyewe ndio mwenye uwezo wa kujipatia ama kujinyima furaha. Wewe binafsi moyoni mwako ndiye Mwenye kujipangia maisha yangu utaishi yatakayokupatia furaha na amani ya moyo wako. Usitegemee mtu atoke nje akupatie furahaa bila wewe kuamua kucheka, huwezi kwenda kwenye matamasha ya vichekesho ukataka kucheka kama hujaamua moyoni mwako kwamba leo nipo tayari kwenda huko kucheka na kufurahi. Ndio furahaa yako pengine itategemea watu waliokaribu nawewe au wanaokugunzuka, labda wanakuhudhi sana na kukukera lakini wanadamu tumeumbiwa kusahau na kusamehee vijana tunasema kupotezea, mambo kama hayo unaachana nayo kwa sababu umekwisha kujiwekea kwamba unahitaji furahaa moyoni mwako.

Upvote
7