Sheria ya 15:- Mponde adui yako kisawa sawa

RIGHT MARKER

Senior Member
Joined
Apr 30, 2018
Posts
129
Reaction score
473
Hii ni Sheria ya 15 kati ya Sheria 48 za mamlaka zilizoandikwa na mwandishi ROBERT GREENE katika kitabu chake kiitwacho THE 48 LAWS OF POWER. Sheria hii imesema; CRUSH YOUR ENEMY TOTALLY, yaani mponde adui yako ipasavyo.

Bila shaka mtu anayejitafuta kwenye maisha ni lazima awe na maadui. Kama wewe huna maadui anza kuwatengeneza. Mwanadamu asiyekuwa na adui ni yule ambaye hafanyi chochote kwenye maisha, kwani hata muuza Ice Cream pia ana maadui. Hata hivyo nafasi ya uadui ina uzito wake; uzito wa uadui haupawi kuzidi mizani yako, itavunjika. Ni kama chumvi kwenye mboga ikizidi sana mboga haitolika, au sukari kwenye chai ikizidi sana chai haitokuwa tamu licha ya kuwa sukari ni tamu. Hivyo adui akifikia hatua ya kuwa adui hatarishi hupaswi kucheka nae ni maumivu kwako.

Katika Sheria ya 15 kati ya Sheria 48 za kitabu cha ROBERT GREENE inasema; waponde adui zako kisawa sawa. Usiende nao nusu nusu au kuwapa chaguo lolote. Kumbuka ukiacha hata makaa moja yakifuka, hatimaye yatawaka. Historia imejaa mifano ya viongozi waliokuwa na uwezo wa kuwashinda maadui zao lakini wakawaacha hai kwa sababu ya huruma. Hata hivyo huruma yao ikawaponza, adui kila mara walikusanya nguvu zao wakizidi kuchukizwa na kuamua, hadi walipokuwa na nguvu za kutosha kulipiza kisasi.

Mara nyingi adui zako hawahisi chochote ila uadui kwako, na wanataka kukuondoa. Kwa mujibu wa sheria hii ya 15 kati ya sheria 48 za mamlaka, inafafanua kuwa njia pekee ya kuwa na usalama na amani ni kuwafanyia adui zako kile ambacho wangekufanyia wewe. Unapopata mamlaka au nguvu usisite kutoa pigo la mwisho, hii haimaanishi kuwaua, lakini angalau kuwatenganisha kwa kuondoa kabisa uwezo wao wa kupigana na wewe.

MFANO HAI: Katika miaka ya 1930, CHIANG KAI-SHEK alikuwa na uwezo wa kuwaangamiza wakomunisti wa MAO TSE-TUNG, kwa hivyo alielekeza mawazo yake kwa wavamizi wa kijapani akaacha kupambana na wakomunisti. Lakini kwa zaidi ya miaka kumi baadae, Wakomunisti walipata ahueni (nguvu) na hatimaye waliweza kulitimua jeshi la CHIANG KAI-SHEK, na kumlazimisha CHIANG KAI-SHEK kukimbilia TAIWAN. Hakujifunza kufuata sheria hii ya 15 ya kumponda adui yako kisawa sawa pindi unapokuwa na nguvu au mamlaka, hivyo ilimgharimu uwezo wake.

BY: RIGHT MARKER-TZ
Mbezi Louis, Dar es salaam.
Septemba 20, 2024.
 
Katika Sheria ya 15 kati ya Sheria 48 za kitabu cha ROBERT GREENE inasema; waponde adui zako kisawa sawa. Usiende nao nusu nusu au kuwapa chaguo lolote. Kumbuka ukiacha hata makaa moja yakifuka, hatimaye yatawaka. Historia imejaa mifano ya viongozi waliokuwa na uwezo wa kuwashinda maadui zao lakini wakawaacha hai kwa sababu ya huruma. Hata hivyo huruma yao ikawaponza, adui kila mara walikusanya nguvu zao wakizidi kuchukizwa na kuamua, hadi walipokuwa na nguvu za kutosha kulipiza kisasi.🥺🥺🙇🏿‍♂🙇🏿‍♂🤔🙇🏿‍♂
IMG-20240919-WA0042.jpg
 
Back
Top Bottom