Sheria ya Ardhi sasa imebadilika, kwa sasa huwezi kupewa hati miliki kama hakuna plan (mipango miji)
pole kwa hiyoissue ambayo hata mimi imenikuta
wanachofanya sasa watu wa Ardhi: wanaweka stop order na kuanza kupita kuonyesha mipaka ya mipango miji iko wapi,mathalani shamba langu lilitoa viwanja viwili na njia kubwa mbili, na kwa gharama za kila kiwanja ilikuwa 3200000Tsh, kwa hiyo kwa viwanja viwili ilinipasa kulipia 6400000Tsh.
sasa katika fidia kulikuwa na Mihembe na mazao mengine pamoja na miti, na Ardhi yenyewe (serikali siku hizi imeanza kulipia Ardhi japo ni kidogo sana) kwa shamba langu lote niliwekewa hesabu ya 3154000Tsh kama fidia, na nikapewa option ya kuchukua kiwanja kimoja kwa 46000Tsh, kingine kwa bei ileile ya 3,200,000Tsh na hizo hela zinatakiwa ndani ya siku nane uwe umezilipa,
nilifika mpaka kwa mkurugenzi na mwanasheria wa Ardhi lakini jibu likawa ni lilelile, niliporudi kuja kulipia nikakuta sehemu yangu keshauziwa mtu na yuko kwenye process ya kupewa hati, ninavyokwambia shamba langu nililonunua 1999 nimeamishwa na nipo sehemu nyingine kabisa na hakuna kesi
na hili inatupasa tuwe makini sana unaweza kukunua shamba wa million zaidi ya kumi, lakini mipango miji ikija hilo hawalitambuhi unaweza kulipishwa kumi nyingine hivihivi