Sheria ya fao la kujitoa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii ni ya kikatili sana

Sheria ya fao la kujitoa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii ni ya kikatili sana

Cashman

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2018
Posts
3,333
Reaction score
5,845
Unaambiwa ukishaajiriwa, ni sawa na kuwa umejisajili kuwa mtumwa, hata ukiacha kazi ili ujiajiri, huwezi kupata pesa yako iliyo mifuko ya hifadhi ya jamii. Itakubidi usubiri hadi miaka 55 ili uipate tena bila riba.

Mfano umeacha kazi ukiwa na miaka 40 itakubidi usubiri miaka 15 kama ni milioni 5, utaipata kama ilivyo bila kujali thamani ya shilingi imeshuka kwa kiasi gani.

Ukiachishwa kazi, utapewa 33% ya mshahara wako kwa miezi 6, ili uile kidogo kidogo ipungue, kisha kama hujapata kazi itabidi usubiri miezi 18 kisha unapata uhalali wa kulipwa pesa yako.

Sheria hii imewekwa kumkandamiza maskini azidi kuwa maskini. Sheria hii ni kandamizi sana na ya kikatili mno. Kwenye kampeni hizi sijaona wakiisemea kabisa.
 
Kiukweli nakaribia kuacha kazi ,nipo kwenye sekta ngumu ya ulinzi, nafanya kazi na kampuni ya SGA SECURITY na kuachishwa ni haraka sana kama itatokea shida kazini , sasa nachojiuliza je kama nina million 04 nitasubiri mpaka mwaka na nusu ?
 
Mbunge akimaliza miaka 5 ,anavuta 400m bila makato.Moja kati ya upumbavu umewahi pitishwa na bunge le kazakistan ni hii sheria.Leo hii waajiriwa wanashindwa kujiondoa kwenye kifungo cha ajira sababu ya sheria kandamizi
Pesa yako mwenyewe serikali inakutungia sheria namna ya kuitumia
 
Imeanza lini hii? Siku si nyingi kuna mtu nayemfahamu aliyepewa hela yake yote.
 
Back
Top Bottom