Unaambiwa ukishaajiriwa, ni sawa na kuwa umejisajili kuwa mtumwa, hata ukiacha kazi ili ujiajiri, huwezi kupata pesa yako iliyo mifuko ya hifadhi ya jamii. Itakubidi usubiri hadi miaka 55 ili uipate tena bila riba.
Mfano umeacha kazi ukiwa na miaka 40 itakubidi usubiri miaka 15 kama ni milioni 5, utaipata kama ilivyo bila kujali thamani ya shilingi imeshuka kwa kiasi gani.
Ukiachishwa kazi, utapewa 33% ya mshahara wako kwa miezi 6, ili uile kidogo kidogo ipungue, kisha kama hujapata kazi itabidi usubiri miezi 18 kisha unapata uhalali wa kulipwa pesa yako.
Sheria hii imewekwa kumkandamiza maskini azidi kuwa maskini. Sheria hii ni kandamizi sana na ya kikatili mno. Kwenye kampeni hizi sijaona wakiisemea kabisa.