Sheria ya Finantial fair player

Sheria ya Finantial fair player

astranaut

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2018
Posts
1,276
Reaction score
1,024
Kwa ulaya kuna sheria ya finantial fair player,sheria hiyo imeanzishwa ili kuvilinda vilabu vidogo vidogo visibemendwe na vilabu vikubwa kwenye soko la usajili japokua bado ni ngumu kucompete kwenye soko la usajili kutokana na changamoto za kiuchumi. hivyo basi team inaruhusiwa kutumia kiasi ambacho ni ndani ya maingizo yake sio kinyume chake na kilabu inayoonekana kukiuka tumeshuhudia zikiadhibiwa kwa kufungiwa usajili n.k

Kwa mantiki hiyo mpira wa Tanzania sasa unakua na vilabu vinaenda kwenye ukisasa zaidi tofauti na zamani,hivyo basi katika kuelekea huko kwenye ukisasa pia nashauri chama chetu cha mpira wa miguu(TFF) na CAF kwa ujumla katika kuiga mazuri ya ulaya pamoja na sheria zao ni muda mwafaka sasa wa kuingiza sheria hiyo ili kuvilinda vilabu vidogo vidogo kuliko sasa kila team inatumia inavyotaka wala hakuna anae hoji.karibuni kwa kujazia nyama zaidi ili kuwafikishia walengwa huko waliko.
 
team inaruhusiwa kutumia kiasi ambacho ni ndani ya maingizo yake sio kinyume chake na kilabu inayoonekana kukiuka tumeshuhudia zikiadhibiwa kwa kufungiwa usajili n.k
Ufadhili pia ni maingizo. Kwa hiyo sidhani kama timu unazoziita ndogo, kwa mfano Temeke Squad inaweza kupambana na Young Africans ambayo ni timu tajiri zaidi Afrika Mashariki na kati.
 
Ufadhili pia ni maingizo. Kwa hiyo sidhani kama timu unazoziita ndogo, kwa mfano Temeke Squad inaweza kupambana na Young Africans ambayo ni timu tajiri zaidi Afrika Mashariki na kati.
lengo sio kuzipambanisha bali kuvipunguza kasi vilabu vikubwa kwenye matumizi ya usajili
 
Acha kwanza timu kubwa na pendwa zaidi hapa nchini Young Africans Sports Club ifanye usajili kisha ndipo ushauri. Matumizi mengine ya pesa toka kwa wananchi ni haya!
IMG-20210731-WA0054.jpg
 

Finantial fair player .....​

tuanzie hapo kwanza,huko kwenu Katavi ni kitu gani hii??
 

Finantial fair player .....​

tuanzie hapo kwanza,huko kwenu Katavi ni kitu gani hii??
makosa ya kiuandishi lakini yote lengo ni kufikisha ujumbe,mods nisaidieni kurekebisha heading
 
Back
Top Bottom