Sheria ya kifungo cha nje ikoje tanzania?

Sheria ya kifungo cha nje ikoje tanzania?

Mgumu04

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2011
Posts
1,940
Reaction score
1,055
Tafadhari ndugu yangu mimi nina rafiki yangu amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja na ametumikia kama mwezi sasa na siku chache .Ndugu zake wamefuatilia kwenye ofisi za ustawi wa jamii ili apewe kifungo cha nje ila imeonekana kuna mlolongo mrefu kila wakienda wanaambiwa atatoka kesho mara baada ya wiki sasa juzi wameenda tena ofisini wakaambiwa barua ilikosewa baada ya kuandikiwa kifungo cha mwaka wakawa wamemwandikia miezi 6 wakaseme (ustawi) kwamba wasubili (ndugu) warekebishe na atatoka jumatatu ambayo ni leo wameenda wakaambiwa hakimu aliye mhukumu hayuto ili atie saini ili atumikie kifungo cha nje swali langu ni kwamba kwa mtu yeyote anayeomba kifungo cha nje ni lazima atiliwe saini na yule hakimu aliye mhukumu au sheria ina sems nini katika ili naomba msaada wetu wana jf
 
..Wizara ya mambo ya ndani kuna kitengo kinaitwa " PROBATION AND COMMUNITY SERVICES-OFISI YA HUDUMA KWA JAMII"; Itategemea upo wilaya au mkoa gani maana ofisi hizo hazipo mikoa au wilaya zote za Tanzania. Uwepo wa huduma hiyo au la utapata MAHAKAMANI kwani wanafanya nao kazi kwa karibi sana. Ikibahatika kuwepo katika eneo ulipo nadhani usumbufu utapungua ukiwaona hao. Pia hakimu aliyemhukumu ndiye hasa mhusika; lakini pia hakimu Mfawidhi anaweza kuhusika endapo alyehukumu hatakuwepo.....WNEINGINE WATAKUONGEZEA!!!!! POLE SANA, HAYA ILA USICHOKE MPAKA UPATE HAKI YAKO.
 
Back
Top Bottom