EINSTEIN112
JF-Expert Member
- Oct 26, 2018
- 21,711
- 35,644
Rais Vladimir Putin ameweka sheria ya kijeshi - kwa mara ya kwanza katika historia ya Urusi ya sasa, kwa sasa sheria hiyo inatekelezwa katika eneo pekee lililotwaliwa na Moscow.
Baraza la shirikisho liliidhinisha kwa kauli moja uamuzi wa Bw Putin. Rais mara moja alianzisha ''hatua'' mbali mbali za kiutawala katika majimbo ya Urusi yaliyosalia.
Magavana walipewa uwezo wa kuweka sheria mbali mbali katika maeneo yao. Kwa mfano, matembezi ya wakazi katika maeneo yaliyo karibu na mipaka yanaweza kuzuiwa, magavana waliahidi kwamba marufuku ya aina hiyo haitawekwa kwa sasa.
Putin alitangaza kuanzishwa kwa sheria ya utawala wa kijeshi katika majimbo manne yaliyonyakuliwa na Urusi kutoka kwa Ukraine katika mwanzo wa mkutano wa baraza la usalama.
Kremlin imekuwa ikizungumzia kuhusu hatua ya aina hiyo tangu Urusi ilipoishambulia Ukraine. Hatahivyo, maafisa wa Urusi wamekuwa wakisema kwa miezi mingi kwamba hakuna mpango wa kuweka sheria ya kijeshi katika majimbo fulani au katika nchi nzima.
"Ngoja niwakumbushe kuwa Jamuhuri ya watu ya Donetsk, Jamuhuri ya watu wa Luhansk, pamoja na majimbo ya Kherson na Zaporozhye zilikuwa chini ya sheria ya jeshi kabla ziwe shemu ya Urusi.
Sasa tunahitaji kuanzisha utawala huu katika mfumo wa sheria ya Urusi. Hiyo ndio maana tulisaini sheria juu ya kuanzishwa kwa sheria ya kijeshi katika maneo haya manne . Ninaiweka," alisema Putin.
Katika hotua yake, Rais huyo alizungumzia kuhusu "kura za maoni" ambapo kutokana na matokeo ya kura hizo, maeneo ya Ukraine "yalijiunga na Urusi " ambazo na iwe Ukraine wala jamii ya kimataifa hawazitambui kuwa halali.
Sheria ya kijeshi nchini Urusi inadhibitiwa na sheria ya Urusi ya shirikisho iliyopitishwa katika mwaka 2002.
Usimamizi wa jeshi.
CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES
Putin aliweka utawala wa kijeshi katika majimbo yaliyonyakuliwa Kipengele cha 7 cha sheria ya shirikisho "kuhusu Sheria ya Kijeshi’’ inaelezea hatua zinazochukuliwa.
Miongoni mwa "hatua nyingine" zilizoainishwa katika kipengele nambari ni haki ya mamlaka ya kuweka masharti kuhusu ‘’shughuli za kiuchumi na ", ununuzi wa mali, uhuru wa mauzo ya bidhaa na huduma, ukusanyaji na usambazaji wa habari.
Sheria pia inasema kwamba "hatua nyingine" inaweza kutumiwa sio katika majimbo ambako kumewekwa sheria ya kijeshi, lakini pia katika maeneo mengine ya nchi.