Sheria ya kuchukua Mtoto

Sheria ya kuchukua Mtoto

stephot

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2012
Posts
17,216
Reaction score
26,225
Wadau wa maswala ya sheria,mimi ilitokea kuzaa na dada mmoja,tulishirikiana kutunza mtoto mpaka ilipofikia kuanza shule yaani kindergaten na mpaka sasa yuko darasa la tatu,maswala yote ya kumlea tulishiriki pamoja ikiwemo ada,chakula na mavazi,ilifikia wakati tukakubaliana kuwa atanipa mtoto atakapotimiza umri wa miaka saba,ilipofika miaka saba akasema atanipa akifikisha miaka tisa,sasa amefikisha miaka tisa anakataa kunipa mtoto ana dai mpaka akimaliza standard seven,lengo langu ni kumchukua huyu mtoto na kumlea,lakini sijui haki yangu kufanya hili jambo ikoje kisheria,ukichukulia kuwa huyu mdada aliolewa mtoto alipofikisha umri wa miaka minne na amesha zaa na huyo jamaa mtoto mmoja,lakini huyo baba hachangii chochote kwenye kumlipia ada wala mavazi,ingawa mtoto wanaishi naye.
 
Kwani tatizo lako ni nini, mtoto ni wako na wala 'mdada' hajakataa kama mtoto si wako, yuko kwa mama yake anaendelea vizuri. Waweza kupeleka matumizi huko. Usikalili kwamba mzazi wa kike hawezi kutunza mtoto.
 
Peleka maombi mahakama ya wilaya wataangalia status ya kudai hiyo custody lakini ujue sheria inampa priviledge pia mama wa mtoto kuishi nae hasa katika tender age
 
Kama mtoto kafikisha umri wa miaka 7,kisheria unawezakumchukua.
Tumia njia ya kifamilia kudai mtoto, ikashindikana nenda mahakamani utapewa mtoto wako.
 
Peleka maombi mahakama ya wilaya wataangalia status ya kudai hiyo custody lakini ujue sheria inampa priviledge pia mama wa mtoto kuishi nae hasa katika tender age

tender age max ni miaka mingapi maana ana miaka 9 na ameanza mwaka wa 10 october last year.
 
Back
Top Bottom