stephot
JF-Expert Member
- Mar 1, 2012
- 17,216
- 26,225
Wadau wa maswala ya sheria,mimi ilitokea kuzaa na dada mmoja,tulishirikiana kutunza mtoto mpaka ilipofikia kuanza shule yaani kindergaten na mpaka sasa yuko darasa la tatu,maswala yote ya kumlea tulishiriki pamoja ikiwemo ada,chakula na mavazi,ilifikia wakati tukakubaliana kuwa atanipa mtoto atakapotimiza umri wa miaka saba,ilipofika miaka saba akasema atanipa akifikisha miaka tisa,sasa amefikisha miaka tisa anakataa kunipa mtoto ana dai mpaka akimaliza standard seven,lengo langu ni kumchukua huyu mtoto na kumlea,lakini sijui haki yangu kufanya hili jambo ikoje kisheria,ukichukulia kuwa huyu mdada aliolewa mtoto alipofikisha umri wa miaka minne na amesha zaa na huyo jamaa mtoto mmoja,lakini huyo baba hachangii chochote kwenye kumlipia ada wala mavazi,ingawa mtoto wanaishi naye.