Sheria ya kukamata ugoni ina kasoro, irekebishwe

Sheria ya kukamata ugoni ina kasoro, irekebishwe

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Sheria ya Ugoni inaeleza ukidakwa na mke au mume wa mtu ni kosa la madai na unaweza kulipishwa fidia kulingana na mahakama itakavyoona.

Sasa najiuliza umepata mwanamke katika mazingira ambayo hujui au hajakueleza au ameficha utambulisho wa ndoa. Wewe kosa lako ni lipi?

Mwanamke ametongozwa, akauliza kama jamaa ameona, jamaa akakana mke wake wa ndoa. Kosa la mwanamke hapo liko wapi? Au angeanza kuulizia mitaani kwanza jamaa ana ndoa?

Hii sheria ina makosa, irekebishwe iangalie mazingira ya mtu kutokuwa na taarifa ya hali ya ndoa
 
Mkuu, sheria ya Ugoni mbona inaeleza hivyo? Basi tu ni uoga wa kutotaka kufanyiwa ubaya. Ila sheria inataka mahakama ndiyo ipange kiasi cha wewe kulipa.

Kama mahakama itathibitisha kuwa hukuwa unafahamu kwa namna yeyote kwamba ni mke au mume wa mtu basi hutalipa kitu.
 
Sheria ya Ugoni inaeleza ukidakwa na mke au mume wa mtu ni kosa la madai na unaweza kulipishwa fidia kulingana na mahakama itakavyoona...
Kwa muktadha huo ndio maana ikawa ni madai kuliko kuwa ni jinai!!kwani ingekuwa ni kuoneana tu,Na hata hiyo kesi kwenye madai huko kuidhibitishia mahakama ili mtu atiwe hatiani ni ngumu mno!!kuna mambo mengi sana huangaliwa.
 
Sasa najiuliza umepata mwanamke katika mazingira ambayo hujui au hajakueleza au ameficha utambulisho wa ndoa. Wewe kosa lako ni lipi?
Inabidi ufanye utafiti wa kutsha kuhakikisha uko within the law, siyo kuambiwa. Kuna case law ya hivyo. nikiipata nitakuwekea
 
Nikibahatika kukufuma kuna adhabu mbili tu nje ya ile ya mahakama 1. Ni kifo 2. Malinda au vyote kwa pamoja hii sitanii wala simutishi mtu
 
Sheria ya Ugoni inaeleza ukidakwa na mke au mume wa mtu ni kosa la madai na unaweza kulipishwa fidia kulingana na mahakama itakavyoona.

Sasa najiuliza umepata mwanamke katika mazingira ambayo hujui au hajakueleza au ameficha utambulisho wa ndoa. Wewe kosa lako ni lipi?

Mwanamke ametongozwa, akauliza kama jamaa ameona, jamaa akakana mke wake wa ndoa. Kosa la mwanamke hapo liko wapi? Au angeanza kuulizia mitaani kwanza jamaa ana ndoa?

Hii sheria ina makosa, irekebishwe iangalie mazingira ya mtu kutokuwa na taarifa ya hali ya ndoa
Sheria inasema hivyo lakini hukumu inategemea mambo mengi. Ukiweza kuiridhisha mahakama bila shaka kuwa yule mke wa mtu alikulaghai na hukujua kabisa kuwa ni mke wa mtu na ulifanya juhudi zote kujihakikishia basi unaweza kupona.
 
Back
Top Bottom