Sheria ya kuzuia POLISI kufanya kazi yao

Sheria ya kuzuia POLISI kufanya kazi yao

deejaywillzz

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2014
Posts
637
Reaction score
224
Habari wakuu, weekend hii nilikuwa nimekaa na marafiki zangu tunapata vinywaji tukimuaga mwenzetu anarudi overseas. Polisi wakaja na gari lao wakimtafuta kaka yake na yule tuliyekuwa tunamuaga kwa kosa la kudaiwa laki mbili na mtu.

Kaka yake hakuwepo hapo kisha wakataka waingie ku search nyumba, kisha mdogo wake akauliza polisi kibali cha ku search nyumba, mabishano yakaanza baina ya Polisi na yule mdogo wake. Kilichofuatia wakamkamata mdogo wake kwa kosa la kuzuia polisi kufanya kazi yao.

Je ni kosa kuzuia polisi ku search nyumba yako hata kama hawana kibali cha ku search nyumba yako?
 
Sina hakika , lakini hii Angalia kwenye KATIBA MPYA hii inayopendekezwa.
 
Kama walikuwa na ile search warant ni kosa kwani polisi walikuwa kisheria.ila kama hawakuwa na search warant hawakupaswa kusearch hiyo nyumba na wamemkamata kibabe ila ndo hivo akifika huko kwao lazima zile taratibu azipitie.KUINGIA BURE KUTOKA..........MALIZIA MWENYEWE WE SI MTOTO MDOGO UTAFUNIWE KILA KITU.
 
Hii nchi inatumbukia kwenye shimo lenye kina kirefu
 
Habari wakuu, weekend hii nilikuwa nimekaa na marafiki zangu tunapata vinywaji tukimuaga mwenzetu anarudi overseas. Polisi wakaja na gari lao wakimtafuta kaka yake na yule tuliyekuwa tunamuaga kwa kosa la kudaiwa laki mbili na mtu.

Kaka yake hakuwepo hapo kisha wakataka waingie ku search nyumba, kisha mdogo wake akauliza polisi kibali cha ku search nyumba, mabishano yakaanza baina ya Polisi na yule mdogo wake. Kilichofuatia wakamkamata mdogo wake kwa kosa la kuzuia polisi kufanya kazi yao.

Je ni kosa kuzuia polisi ku search nyumba yako hata kama hawana kibali cha ku search nyumba yako?

Polisi anaruhusiwa tu kusearch nyumba ya mtu akiwa na kibali (search warrant) lakini kuna exceptional katika sheria hii katika mazingira ambapo polisi wana sababu ya msingi kusadiki/kuamini kuwa nyumba hiyo isiposachiwa haraka basi kuna uwezekano mkubwa wa hatari (kubwa kiasi cha kuaffect jamii) kutokea au ushahid katika kesi muhimu sana kupotea/kupotezwa.

Katika mazingira hayo polisi wanalazimika kumuita kiongozi yeyote wa serikali/jamii aliye karibu na utatakiwa uwepo pia ushahidi wa majirani kadhaa wenye akili timamu kushuhudia tendo zima la ukaguzi.

Katika ukosefu wa hayo yote mawili (warrant na ushahidi wa civilians) basi police hawana mamlaka ya kusearch na kwa kuwa ni haki ya kikatiba ya raia kulinda mali zao na kujilinda wenyewe raia mhusika ana haki ya kuzuia ukaguzi huo...nina hakika police wakikukamata katika mazingira ya kuwazuia kwa misingi hiyo charge hawataiandika hivyo..wataphrase kivingine ili kukutia hatiani
 
Back
Top Bottom