Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015: Kwa mkakati huu wa Serikali, Watumiaji wa Mitandao tutapona?

Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015: Kwa mkakati huu wa Serikali, Watumiaji wa Mitandao tutapona?

Ambae anaona hizi sheria ziko sawa kichwani ana matope (kusema hivi tayari nishavunja kipengele kimoja na naweza kwenda jela mwaka au kulipa fine isiyopungua three million).Unaona ilivyo rahisi kumfunga mtu. Siamini walikaa wabunge na wao kwa akili zao kabisa wakapitisha haya madudu. Hii ni dictatorship kabisa, sijaona HATA KIMOJA ambacho ni right kuhusu hiyo sheria, em aliyeona kipengele ambacho kinasaidia bila kukandamiza aniambie isije kua nimeruka mambo ya msingi.

Naona ni muda sasa inabidi watu tuungane kuipinga hii ifutwe kabisa au ifanyiwe marekebisho.

Ukisoma vizuri hiki kimeseji tu tayari mtu anaweza jipanga akanifunga maana hata identity tu nayotumia sio jina langu halisi.
 
MSIJALI HII SHERIA ILIPANGA KULINDA UHUNI NA UHALIFU WA WATU FULANI FULANI WA CCM NA INAPIGWA VITA NA DUNIA NZIMA, IKO KINYUME NA UHURU WA KUNENA, NA ITAFUTWA
 
Wakati nchi za wenzetu wakitunga sheria za kudhibiti uhalifu unaoligharimu Taiga mamilioni ya fedha na damu za watu, Tanzania inatunga sheria ya kusaidia kupatikana kwa " goli LA mkono"
 
Ambae anaona hizi sheria ziko sawa kichwani ana matope (kusema hivi tayari nishavunja kipengele kimoja na naweza kwenda jela mwaka au kulipa fine isiyopungua three million).Unaona ilivyo rahisi kumfunga mtu. Siamini walikaa wabunge na wao kwa akili zao kabisa wakapitisha haya madudu. Hii ni dictatorship kabisa, sijaona HATA KIMOJA ambacho ni right kuhusu hiyo sheria, em aliyeona kipengele ambacho kinasaidia bila kukandamiza aniambie isije kua nimeruka mambo ya msingi.

Naona ni muda sasa inabidi watu tuungane kuipinga hii ifutwe kabisa au ifanyiwe marekebisho.

Ukisoma vizuri hiki kimeseji tu tayari mtu anaweza jipanga akanifunga maana hata identity tu nayotumia sio jina langu halisi.
MSIJALI HII SHERIA ILIPANGA KULINDA UHUNI NA UHALIFU WA WATU FULANI FULANI WA CCM NA INAPIGWA VITA NA DUNIA NZIMA, IKO KINYUME NA UHURU WA KUNENA, NA ITAFUTWA
Hii ilikuwa muhimu kwa ccm ili kuzuwia watu wasiseme tunaibiwa kura.
 
Hii ilikuwa muhimu kwa ccm ili kuzuwia watu wasiseme tunaibiwa kura.

Iwe muhimu isiwe muhimu swala ni kwamba bado haijafutwa, hilo ndilo la msingi maana yake siku yoyote ile mtu anaweza bambikiwa kesi na akafungwa hivihivi tunaangalia
 
Sheria hiyo haikutungwa na wabunge bali ililetwa kama mswaada na flani flani katika bunge kisha kupitishwa haraka haraka kwa kigezo cha ifanye kazi mapema uchaguzi unakaribia, kisha wakadai wataifanyia marekebisho.
 
Hakuna mjadala ulio kubali hiyo sheria bali mawaziri fulani walitumika kuipamba sheria hiyo kwa wananchi kupitia tbc1
 
Mmmmh serkal hii ina less kbao
Lakn anyway
Leng lao tutaljua
Na kma baadh itafungiw
Wataona athar kubw then
Watajua nn cha kufanya hao macrazer
 
Wakuu salaam,

Tuendelee kukumbushana, Sheria mpya ya makosa ya mtandao inafanya kazi nchini Tanzania.

Ni vizuri kuifahamu sheria hii vizuri ili kujiepusha na adhabu mbalimbali zitakazotokana na ukiukwaji wa sheria hiyo.

Ikimbukwe kwamba kutokujua sheria si sababu itakayokufanya usichukuliwe hatua.

kwanza swali la muhimu kujiuliza ni kwamba sheria hii ya makosa ya mtandao inamuhusu nani?

Sheria hii kwa kifupi inamuhusu mtu yoyote anayetumia mtandao wa intaneti kupitia kifaa chochote ikiwemo kompyuta, simu za mikononi, luninga na vingine vya namna hivyo.

Watumiaji wa mitandao kama Facebook, WhatsApp, Instagram, Twitter, barua pepe (emails), blogu na nyinginezo za aina hiyo wanapaswa kuwa makini sana na sheria hii ya makosa ya mtandao.

Kwa leo nitaorodhesha makosa machache ambayo ni muhimu ukayaepuka pindi tu sheria hii itakapoanza kufanya kazi mnano mwezi septemba.

Epuka kusambaza picha/video za ngono ama zinazoashiria vitendo vya ngono- adhabu ya kosa hili ni pamoja na faini isiyopungua shilingi milioni ishirini au kifungo kisichopungua miaka saba ama vyote kwa pamoja.

Epuka kutengeneza na kusambaza ujumbe, picha zenye taarifa za uongo- adhabu ya kosa hili ni pamoja na faini isiyopungua shilingi milioni tatu au kifungo cha miezi sita ama vyote kwa pamoja.

Epuka kumtusi/kumkebehi mtu kutokana na utaifa wake, rangi yake, kabila ama dini yake- adhabu ya kosa hili ni pamoja na faini isiyopungua shilingi milioni tatu au kifungo kisichopungua mwaka mmoja ama vyote kwa pamoja.

Epuka kutengeneza na kusambaza taarifa za ubaguzi wa rangi/utaifa- adhabu ya kosa hili ni pamoja na faini isiyopungua kiasi cha shilingi milioni tatu au kifungo kisichopungua mwaka mmoja ama vyote kwa pamoja.

Epuka kuchapisha taarifa ambazo zinaweza kusababisha umwagaji damu ama vitendo vingine visivyo vya kibinadamu- adhabu ya kosa hili ni pamoja na faini isiyopungua kiasi cha shilingi milioni kumi au kifungo kisichopungua miaka mitatu ama vyote kwa pamoja.

Epuka kutumia taarifa/jina la mtu mwingine huku ukijifanya wewe ni yeye- adhabu ya kosa hili ni pamoja na faini isiyopungua kiasi cha shilingi milioni tano au kifungo kisichopungua miaka mitano ama vyote kwa pamoja.

Hayo ni baadhi tu ya makosa ambayo tunapaswa kujiepusha nayo wakati huu ambapo sheria ya makasa ya mtandao imeanza kufanya kazi rasmi.

Kwa kifupi jiepushe na kutengeneza ama kusambaza ujumbe/picha ambazo ni kinyume cha maadili pamoja na zile zinazoweza kusababisha uvunjifu wa amani ama kuleta madhara/karaha kwa watu wengine.
 
Back
Top Bottom