Sheria ya Malezi: Ukitelekeza Mtoto Jela Miezi 6 au Faini Milioni 5

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
Moja kwa Moja kwenye mada.

Kwa wale ambao Huwa mnazaa na kutelekeza Watoto mjiandae vizuri maana Sheria ya Malezi imeboreshwa..

Ikibainika umetelekeza mtoto awe wa Nje ya ndoa au ndani basi adhabu yake ni jela Miezi 6 au Faini ya sh.Milioni 5 au vyote Kwa pamoja..

Ila Kwa mtizamo wangu mbona faini ni kubwa kuliko kifungo? Hicho kifungo kingekuwa mwaka 1.

Usije kusema hujaambiwa

========

Afisa Ustawi wa Jamii katika Halmashauri ya jiji la Dar es salaam Rosemary Wilfred amesema sheria ya sasa kwa mwanaume anayetelekeza mtoto baada ya kuzaa na mwanamke inamtaka mwanaume husika kulipa faini ya shilingi milioni tano ama kufungwa jela miezi sita au kutumika adhabu zote kwa pamoja.

Amesema wao kama maafisa wa ustawi wa jamii wanaendelea kuelimisha jamii juu ya kuzifahamu sheria za makuzi na malezi ya mtoto ili kulinda haki za mtoto za kupata malezi kutoka pande zote mbili za wazazi.

Chanzo: EastAfrica Radio
 
Kutakuwa na ithibati gani kuwa mtoto ni wangu endapo nitakuwa na shaka ikizingatiwa siku hizi kina dada wanafanya mimba/watoto kuwa mtaji kwa kupewa uhusika mtu zaidi ya mmoja.

Mamlaka zilishawahi kukiri kuwa huwa zina 'manipulate' matokeo ya DNA kuepusha watoto kukosa malezi ya baba.
 
Mtanyooka tu
 
Kuna ex wangu alinambia mtoto wangu nikawa poa tu na mtoto, mpaka pale mtoto wake mkubwa ex wangu. Aliponambia umefanana na sana na Boyfriend mpya wa mama yake. Alisema haya mbele ya mama yake, mama alijaribu kumminyia macho lakini imetoka hio. Msela nilikula kona mpaka leo sijui hii sheria itanihusu au yule boyfriend wake ex wangu🤣🤣
 
Ukiwa na shaka lipia DNA
 
Ili uishi na mwanao lazima apite miaka 5
 
Wanaokataa watoto waje tuyamalize kisheria mtu mzima nibebe majukumu Yao. Nitawaachia watoto wao watakapofikisha miaka 18 ila Kwa muda huu waseme Kama hawawezi kuwahudumia Kwa sasa ili tusiharibu kizazi. Wataendelea kuishi na mama zao ila gharama zote zitatolewa nami without physical means.
The lost
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…