Principle inasema A non Muslim cannot inherit from a Muslim na vice Versa is true
Kama unajua jambo liseme, kama hujui, basi nyamaza kimya na usipotoshe jambo maana ninaamini kuwa ukifundisha watu hapa wanagroup, umefundisha wengi na ukidanganya, umedanganya wengi na hao hao huenda wakaendelea kudanganya wengine.
UFAFANUZI
kwa imani ya dini ya kiislam, inatambua ndoa baina ya muislam na muislam tu. Hivyo km mmojawapo si muislam basi kwanza ni shurti aweze kusilimu au kubadili dini na kuwa muislam.
HIVYO BASI
muislam yeyote atakaefunga ndoa na mtu asie muislam, ndoa hyo ni batili.
IWAPO KUTAFANYIKA NDOA YA NAMNA HYO
Basi haitahesabika kuwa ni ndoa ya kiislamu na haitafuata muktadha wowote km zilivyo ndoa za kiislam. Hapa nazungumzia kuhusu haki za kindoa, na urithi kama ambavyo Quaran tukufu imeweka vipengele mbalimbali vya mirathi.
JE IWAPO MUISLAM AMEOA AU KUWA NA UHUSIANO NA ASIE MUISLAM NA KUPATA WATOTO, JE HAKI ZAO ITAKUWAJE?
Quaran tukufu imeweza kutoa maelekezo ya jinsi ya kutoa urithi kwa walio waislam. Na ipo wazi kuwa 75% au 2/3 ya mali Ya muislam yeyote, itafuata urithi km ambavyo Quaran imeelekeza. 25% iliyobaki, mwenye mali anaweza kuigawa kwa yeyote kadri atakavyopenda. Na hapo ndo ataweza kutoa urithi kwa wale wasio waislam hasa mke na watoto wake km ataona inafaa. Hyo Mali anaweza kuigawa kwa njia ya "HUBA AU HIBA"(for love n affection)
NB: kwa mujibu wa dini ya kiislam, ni kosa kuandika wosia wa aina yoyote bila kufuata maandiko kwa mujibu wa Quran na wosia wowote ulioandikwa na muislam bila kufuata maandiko ni batili na wengi wao huenda mahakamani kwa ajili ya ku-challenge na mahakama ikijiridhisha, huweza kuubatilisha, isipokuwa tu ile 25% ambayo haipo kwa mujibu wa Quran, anaweza andika wosia na haiwezi kuwa -challenged mahakamani