Sheria ya ndoa lazima ibadilike


Hakuna mahali pamekataza talaka ktk mistari yote hiyo.
1wakorinto 7:11 "...mke asiachane na mumewe; LAKINI, IKIWA AMEACHANA NAYE..."
Huo mstari unajua kuna kuachana
 
Suala ni kwamba mke anaachwa.
Sasa hembu mtu aseme ni wapi kanisa linapata mstari wa kukataa talaka 100%!!
 

Ndugu jicho tai! Hili andiko liko wazi kabisa! Hata kama mke au mume anatabia mbaya kiasi gani! Kama SIO MZINIFU BASI NI MARUFUKU KUMUACHA!
Sasa kama sio kulazimishwa kukaa na mlevi. Mwizi. Mpenda matusi. Mbadhilifu wa mali. Na uchafu mwengine ni nini??

Halafu hebu fikiri kama mke au mume juu ya uchafu woote huo kukufanyia! Pia umkute ni TASA(Hawezi kuzaa).!!
Kwa mujibu wa andiko huwezi kumuacha MPAKA MMOJA WENU AFE!!

Kwa maisha tunayoishi sasa hili andiko halitufai kabisa! La si hivyo utakuta wanandoa wanatoana roho.mbona tunayaona tayari hayo!
Mtu anamfanyia mpango wa kumuondoa mwenzake kwa sababu akimpa talaka jamii itamsuta!!

Mi na imani kubwa kabisa hili andiko sidhani kama litakuwa la Mungu!!

Mungu Mkuu hawezi kuwafanyia viumbe wake ugumu kiasi hiki!! Haiingi akilini hata kidogo.
 
Hakuna mahali pamekataza talaka ktk mistari yote hiyo.
1wakorinto 7:11 "...mke asiachane na mumewe; LAKINI, IKIWA AMEACHANA NAYE..."
Huo mstari unajua kuna kuachana

Na sababu ya kuacha au kutoa talaka kwa mujibu wa andiko ni ZINAA PEKE YAKE!!

sasa wewe unakubali kweli kuwa MUNGU MWENYE HEKIMA ZOTE!
Atuwekee sisi viumbe wake masharti ambayo ni mabaya namna hii??

Yaani hata baba hawezi muwekea mwanae masharti kama hayo!

Sembuse Mungu??

Mi na imani kubwa kuna mtu kaingiza haya maneno kwenye andiko!!
Na kama tunavyojua kuwa bibloa imechakachuliwa saana!

Haiingi akili kuwa Mungu akulazimishe kukaa na mke au mume mlevi, mwizi, tapeli, mtumiaji wa madawa ya kulevya, na mgomvi wa kila siku! Eti tu kwa sababu sio mzinzi. Basi lzm ukae nae!!

Huyo Mungu hawezi kuwa muonevu kiasi hicho!! Hapa kuna mkono wa mtu!! Na mchakachuo!! Mi ndo nakwambia.
Na kama unabisha muulize mtu yyt kama hii ni haki!?
 

Hakuna divorce ama talaka kwenye ndoa za kikristo bali ni separation ambayo haivunji ndoa
 
Hakuna divorce ama talaka kwenye ndoa za kikristo bali ni separation ambayo haivunji ndoa

Kwa hiyo nikishafanya hio separation naruhusiwa kuoa tena?
Au ndio imekula kwangu!
 
Utaoa ama kuolewa pale mmoja atakapo fariki

Ndio maaaana kesi za mpenzi kufa kifo cha utatanishi haziiiiiishi!

Kumbe mpaka mmoja afe!?? Aiseeee! Duhhhh!
Mi na ukristo mbali mbali! Nisije wekewa sumu ya panya bure. Kisa? Mama watoto kanichoka!
Bora wale wanaoruhusu talaka.!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…