Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura Na. 343 "KUHUSU KUKAA MITA 200" Inasema .......

Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura Na. 343 "KUHUSU KUKAA MITA 200" Inasema .......

Mr Chin

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
4,625
Reaction score
1,024
[h=2]
kura.jpg
[/h][h=2]MAZOEA YA KUWEPO UMBALI WA MITA 200 AU 300 KUTOKAKITUO CHA KUPIGIA KURA[/h]

Kumekuwepo na mazoea kwamba, baada ya kupiga kura wafuasiwa vyama hubakia na kukaa kwenye maeneo ya kupigia kuraumbali wa mita 100 au 200 au 300.Jambo hili ni kinyume na Sheria za Uchaguzi. Kwani, katikakifungu cha 104 (1) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura Na. 343kinasema nanukuu

“Hakuna mtu atakayefanya Mkutano siku ya kupiga kura au;ndani ya jengo lolote ambamo upigaji kura katika uchaguziunaendelea, au mahali popote ndani ya eneo la mita miambili yajingo hilo, kuvaa au kuonyesha kadi ya picha yoyote, upendeleoau nembo nyingine inayoonesha kuunga mkono mgombea Fulanikatika uchaguzi”

Mwisho wa kunukuu.

Aidha, kifungu cha 103 (1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali zaMitaa, Sura ya 292 kinasema, Nanukuu:

“hakuna mtu atakayeruhusiwa, katika jengo lolote ambalo upigajikura katika uchaguzi unaendelea, au njia yoyote inayotumiwa naumma ndani ya umbali wa mita mia tatu ya mlango wowote wakuingilia katika jengo, atavaa au kuonyesha kadi, upendeleo au 4nembo yoyote inayoashiria kumuunga mkono mgombea Fulanikatika uchaguzi”Mwisho wa kunukuu.

Kifungu cha 5 cha Sheria ya Adhabu, Sura Na. 16 kinaelezamaana ya njia ya Umma.

Nanukuu:

“Public way includes any highway, market place, square, street,bridge or other way which is lawfully used by the public”

Mwisho wa kunukuu.

Vifungu vya Sheria zote kwa pamoja havisemi wala kutoa fursa aunafasi kwa wananchi kukusanyika bali zinapiga marufuku nakukataza uvaaji wa sare, au nembo au alama za Vyama vya Siasasiku ya kupiga kura kwa umbali kati ya mita 200 na 300.

Hivyo basi ieleweke kwamba umbali huo wa mita 200 mpaka 300sio umbali unaowaruhusu watu kukusanyika kwa kisingizio chakulinda kura.

Aidha, uzoefu unaonesha kwamba, katika kampenizinazoendelea, pale ambapo wafuasi wa vyama tofautiwanapokutana uwezekano wa kutokea vurugu ni mkubwa nasehemu nyingine vurugu zimetokea na kusababisha maafamajeruhi na uharibifu mali.


Source: http://www.nec.go.tz/uploads/documen...20UCHAGUZI.pdf

 
Ni nini mantiki ya hizo mita 200 kutamkwa, kwanini sheria isingetoa katazo la moja kwa moja kwamba kusanyiko lolote haliruhusiwi baada ya kupiga kura pasipo ku-point out radius distance ya 200m????
 
Tatizo mnatetemeka miaka mingine mlikuwa wapi kusema sheria ya uchaguz hairuhusu kulinda kura!?
Hakuna sheria inayo kuruhusu kulinda kura, lamba hiyo ipo kwenye UKAWA lakini sio Tanzania.
 
Ni nini mantiki ya hizo mita 200 kutamkwa, kwanini sheria isingetoa katazo la moja kwa moja kwamba kusanyiko lolote haliruhusiwi baada ya kupiga kura pasipo ku-point out radius distance ya 200m????
Nini huelewi kwenye hiyo sheria? Be more specific.
 
Hizo sheria zote mbili yaani sura Na. 343 na Na. 292
Naziona zipo silence na sijui position ya law inakuaje pale ambapo sheria yenyewe imekuwa silence?

Kifungu cha 104(1) sura Na 343 naona kimebeba sharti linalo kataza kufanyika kwa MKUTANO ndani ya mita 200.

Nataka kujua uhusiano uliopo kati ya mkutano na watu kubaki nj'e ya mita miambili kwa nia ya kurinda kura na kusubili matokeo ya kura?
 
Mleta mada umepotosha kwa makusudi. Sheria inaruhusu kuendelea na mambo mengine yote nje ya mita 200. Sheria iko wazi kabisa, nje ya mita200 wote tuko huru na maisha yetu ya kila siku, iwe kula, kunywa, kulinda au kusubiria matokeo.
 
Mr Chin, Unajitekenya Na Kucheka Peke Yako, Sheria Imeeleza Wazi Halihitajiki Kusanyiko Lolote Ndani Ya Mita 200, Kuanzia Mita 201 Ni Ruksa Kusubiri Matokeo, Kawapotoshe Wenye Akili Finyu Kama Zako! Mabadiliko Hayaepukiki
 
Hakuna mtu atakaye vaa sare, wala kufanya kampeni siku hiyo! Kitakachofanyika ni kusubiri matokeo, tukiwa na mazungumzo ya kawaida, yawezakuwa mpira au biashara.
 
mleta mada wewe ni miongoni mwa wapuuzi wengi sana waliojaa katika nchi hii.
hivi kwa akili yako ndogo kifungu cha 104 kinatoa tafsiri absurd kiasi hicho?
 
Wakuu kisheria ni kwamba case ama jarada linapokwenda mahakamani na uamuzi haujatolewa haitakiwi kujadili ama kutoa maoni! Subirini decision ya mahakama kuu! Main registry dar es salaam! Wakili peter kibatala amefungua case pale! Baada ya hapo yu can give opinions
 
Wakuu kisheria ni kwamba case ama jarada linapokwenda mahakamani na uamuzi haujatolewa haitakiwi kujadili ama kutoa maoni! Subirini decision ya mahakama kuu! Main registry dar es salaam! Wakili peter kibatala amefungua case pale! Baada ya hapo yu can give opinions
Je, hayo maamuzi yamesha toka/
 
Ni nini mantiki ya hizo mita 200 kutamkwa, kwanini sheria isingetoa katazo la moja kwa moja kwamba kusanyiko lolote haliruhusiwi baada ya kupiga kura pasipo ku-point out radius distance ya 200m????

Wewe nakuona kama mbabaishaji.Nadhani sherıa haikutungwa wakati huu.Sheria hıi ninavyoiona nı nzuri kwa wapinzani kwani vurugu ndizo ambazo zimekuwa zıkıtumika kuiba kura.
 
Back
Top Bottom