Binafsi napenda kuchunguza mambo zaidi kwa kina sana kuliko wengi wanapoishia hivyo ingawa nasoma mitazamo tofauti nadhani ni budi kwa jukwaa kuchambua mitazamo kuliko kuiandika tu kama ilivyoandikwa pengine. Utaniwia radhi kwa kutaka ufafanuzi zaidi wa kina ambao utaweka wazi hizi zinazoitwa sheria au kanuni za mind and universe.
Kwa kuwa uko topic ya nne basi nami nitajikita hapa hapa katika vipengele hivi katika changamoto ili labda kuelewa zaidi au kuonesha udhaifu wa mitazamo hii.
Mfano umesema: "Maisha unayoishi hivi sasa hayajaachana na ulimwengu unaoendelea akilini. Ukiwa umefuatilia sheria ya kwanza utakuwa umejifunza kuwa kila tokeo lina chanzo chake, sheria ya pili ikasema mwanadamu ana uhuru wa kufikiria na ni yeye mwenyewe ndiye mwenye uwezo wa kutumia akili yake kufikiria na sio mwingine, kila mmoja ana uhuru wa kufikiria na kanuni ya tatu ikasema kuwa unapoelekeza umakini wako napo panakua.Sheria au kanuni hii ya nne inafuata baada ya kuelewa kanuni zile tatu zilizotangulia.
Kanuni zote zimeonyesha umuhimu wa akili na ufahamu wetu katika kutengeneza maisha yetu. Sheria hii ni kama imedhibitisha kabisa kwa kusema kuwa uhalisia wa kila mwanadamu unatokana na kinachoendelea kwenye akili yake."Labda kwa kuanzia, kwa kanuni hii ya nne una maana Mawazo yako ndiyo yajengayo uhalisia wako!?
In what extent?
Hii nadharia ina loop-holes nyingi na haipaswi kuitwa kanuni kwa maana halisi ya kanuni ambazo kamwe haziyumbi kwa namna yeyote mfano angalia fundamental laws of physics, zinapimika na kujaribika kwa kila namna na zimesimama kama zilivyo. Hizi tunaziita kanuni au sheria kwa kuwa hazina matundu wala waziyumbi na hivyo kama binadamu tumeweza kuunda vitu madhubuti ( machines, tools, buildings etc) na kwa mwendelezo kwa kutumia kanuni hizi.
Kwamba mawazo ya kiumbe jamii ya homo sapiens yanatengeneza na kuhalisi physical universe anayoitazama au kuifikiria! Hii kwa mtazamo wa kina concept hii kwanza inapendekeza kwamba ili ulimwengu uwepo lazima maisha haya tuyajuayo yawepo ili kuutazama. Na kutoka katika mada, observer wa ulimwengu amelengwa kuwa kiumbe mwenye conscious na bila huyu kuutazama ulimwengu basi uhalisia ulimwengu huu unakuwa haupo, so to say.
Kwa namna nyingine ambayo ni soft lakini iliyotolewa katika mzizi wa mtazamo huu ni kwamba mwanadamu yuko responsible kwa uhalisia wake mwenyewe kama ulivyoanisha na hivyo basi kwa kuwa walio nje yake wanaweza kuwa si halisi kama hawatokea katika akili yake. Nachelea kusema kwamba ingawa kuna mchango mdogo wa matokeo (performance) katika uhalisia wa mwanadamu kutokana na anachotaka kiwe sehemu kubwa haibebwi na "kinachoendelea katika akili yake" hivyo si sawa kusema hii ni kanuni.
Wanaokubaliana na mtazamo huu wa mada watapaswa kuamini kuwa mawazo yana uwezo wa kuumba, kuendesha na kuwa na nguvu juu ya uhalisia wa nje/unaotokea. Kwamba matendo, matukio, vitu na muda na space vinaweza kuendeshwa kwa mawazo ya mtu mwenyewe akili mwake na hivyo kuwa reality. Je ni kweli mawazo ya mtu yana uwezo huu as inevitable consequence of situation that cannot be altered of changed mpaka hali hii iitwe kanuni? Hapana hii ni wrong. Mawazo/fikra za kiumbe wa kibailojia mwenye asili ya carbon hayana nguvu ya kuumba uhalisia wa ulimwengu wake na kuwa na full control ya ulimwengu huo.
Human beings kama living observers wa physical universe na fundamental physical constants zake hatuwezi wala hatubebi uwezo wa kuwa creators wa ulimwengu na uhalisia tunaouona individually. We are simply observing. Impact inayotokana na interference yetu katika ulimwengu ni sehemu ndogo ambayo nayo ni chini ya physical fundamental laws of the universe lakini si kanuni ya akili. Nadhani ingekuwa vema kwa wewe kufafanua kwa extent gani thoughts zina-create someone's reality? Kama ni katika performance tu hii ni rahisi sana kuegemea katika kivuli hicho ambacho mifano yake haipaswi kuifanya concept hii iwe universal law.
Ukiamini kwamba utakuwa rais wa nchi siku moja hii itakusaidia katika kuelekeza nguvu zako kwenye matokeo hayo lakini si sheria kwamba kwa kuwa umeweka thoughts hizo kwa asilimia mia basi thoughts hizi zina nguvu ya kufanya hii iwe reality, na ni kanuni nope! Tunaweza kusema umejaribu kuinfluence matokeo kwa kuwa kuwaza hili basi unaweza jenga mazingira fulani ya kufanikisha matokeo lakini huna mamlaka ya mwisho ya matokeo haya. Hapo ndipo hii inakuwa si kanuni bali concept tu! Na hii ni katika performance tu kwingineko ni pagumu zaidi. Hakuna any fine tuned phenomena katika universe ambayo inamhitaji kiumbe kutoka duniani awepo ndio nayo iwepo katika uhalisia wake.
Rahisi zaidi ni kwamba kama mawazo yetu yana nguvu hii ya ku-influence reality katika phyisical world, nataka kujua kwa uhakika kama mtu aliyefuzu vizuri katika kuielewa concept hii amewahi kuwaza kupaa angani na akaweza kupaa huku watazamaji wakishuhudia nguvu ya mawazo katika fikra za mwanadamu?.
Naomba mwanga katika haya kwa kuanzia ili tuanze kujadili zaidi vipengele vingine.