Sheria ya Upigaji Kelele ni balaa.

Sheria ya Upigaji Kelele ni balaa.

KakaJambazi

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2009
Posts
18,804
Reaction score
12,227
Nchi ya Kenya imepitisha sheria ya kutokutoa sauti au kupiga kelele isiyozidi umbali wa 30km, itakayoanza kutumika baada ya miezi sita ijayo.

Mpaka sasa makonda wa matatu, wenye kumbi za disko, wenye misikikiti na wagonga kengele makanisani wako kwenye wakati mgumu, huku wakijiuliza ni jinsi gani wanaweza kukwepa mkondo wa sheria.

Huko majumbani nako hali ni tete, kwani kucheka na kulia nazo ni kelele.
 
Ee bana ee, hata mimi niliisikia hiyo kitambo kidogo. Ninavyoona ni kwamba kwa jinsi jamii za kiafrika zilivyo, sheria hii ikianza jela naona zitajaa..
 
kuna mtu awezaye kucheka na sauti ikasambaa 30km?
 
Itakua 30 Meters hakuna konda anayeweze kupiga kelele 30 Km.
 
kuna mtu awezaye kucheka na sauti ikasambaa 30km?


Point of correction,, ni 30M na si km.

Faini kwa mtu atakayekamatwa ni Ksh 5million au jela miaka 2. Itaanza kutumila Januari mwaka ujao.
 
Back
Top Bottom