DSN
JF-Expert Member
- Feb 2, 2011
- 2,837
- 1,679
Naaamini daima mlinzi wa mwisho wa nchi yoyote dunia ni USALAMA WA TAIFA wa TAIFA LOLOTE DUNIANI.
USALAMA WA TAIFA ndio roho ya mwisho ya TAIFA kujua MAADUI WA TAIFA na NDIO washauri wa muhimu kutoa MIKAKATI ya njia gani zitumike kupambana na adui awe ni wa ndani ya nchi ama nje ya nchi.
Kwa mujibu wa sheria ya USALAMA WA TAIFA ya mwaka 1996 Ibara ya 5:2(1), kipengele hiki kinatamka HAITAKUA KAZI YA USALAMA WA TAIFA KUHAKIKISHA KUWA HATUA ZA KIUSALAMA ZINATEKELEZWA[kwa mujibu wa Kisima cha Mjadala]
Jamani kama kifungu hiki ndio sheria halali, basi kumbe hapa tulipofika USALAMA WA TAIFA SIO waliotufikisha hapa tulipo bali WATAWALA WETU NA BUNGE HILO LILOKAA NA KUTUNGA SHERIA HIYO.
Ni jukumu sasa la wao kama Walinzi wa MWISHO WA UHAI WA TAIFA wawe tayari kuivunja sheria hiyo,aiwezekana anaelinda nchi amjue adui yake [naamanisha adui wa USALAMA WA TAIFA] kisha azuiwe kujua ni jukumu la nani, njia zipi na wakati gani adui yake atashughulikiwa kumuepusha kumuua yeye kama TAIFA.
Manake hapa tulipofika sasa bila busara za walinzi wa nchi kutumika ipasavyo, nchi hii iko kwenye hatua ambayo ni bomu wakati wowote likipata mlipuaji linalipuka manake, wananchi wanaitaji majibu ya mafumbo mengi sana na ambayo wenye majibu hayo wapo bado na hawawatosherezi kwa majibu wanayotoa.
Kwa kuwa wapo na ni jukumu na wajibu wao kuwajua na kupambana [Wajibu wa walionyanganya na bunge mwaka 1996]na maadui zetu. Waludishe wajibu wao wa KUPAMBANA na maadui zetu wa ndani na nje ya nchi.
TAIFA litakapoingia kwenye matatizo wao pia ni watanzania nao watakuwa ni sehemu ya waathiliwa wa tatizo,mbaya zaidi ni DHAMBI MBAYA kwao na kwa vizazi vyao kwa KUISALITI MAMA NCHI NA WANA WA NCHI kwa kushindwa kutekeleza jukumu la kuilinda na kusimamia USTAWI WA TAIFA ambao kwao ni dhamana waliyokabidhiwa na WATANZANIA.
Wanaitajika kulingana na nyakati za sasa kuwa mabadiliko kutoka kuwa IDARAna hadi TAASISI [INSTITUTE] yenye IDARA toshelezi na yenye kujitegemea kwa kila jambo hata kama watatumia mabilioni ya shilingi kwani ghalama ya kujenga Taifa jipya na kuludisha uhai wa watakao potea kwa Taifa kuingia matatani, nini kulinganisha na mabilioni hayo. Watanzania wanalipa kodi ili Serikali iwatumikie wapate ustawi binafsi na hatimae ustawi wa Taifa zima na kwa ujumla wake. Na USALAMA WA TAIFA ndio walinzi wakuu kusimamia UHAI HUO WA WANANCHI KAMA TAIFA.
Sio vyema na sio sahihi leo wananchi wanajadiliana kuwa amani ya Taifa iko hatiani wakati wowote amani inaweza kutoweka, kisa UFISADI na tofauti kubwa ya kipato kati ya Matajiri na Maskini.
Jibu lipatikane ili gumzo la maisha ya kila siku ya watanzania wajadiliane jinsi gani Taifa lao kipato chake kimeongezeka na wajadiliane mambo ya msingi juu ya mafanikio mema ya utawala uliopo au utakao kuja. Wajadiliane dhidi ya sera zipi za Chama Tawala [Ruling Party] ama Upinzani [Opposition] ni bora kwao na kama zinastahiki kupewa nafsi ya kupewa nafsi ya kutekelezwa ili zilete ustawi.
Tufike sehemu watanzania wawe gumzo duniani kuwa AFRICA kuna Taifa limeingia kwenye DEVELOP NATION, Why Not?
Nampenda Mwl JK pamoja na msimamo wake ambao ni udikteta kwa Maslahi ya wengi ulijenga picha ya Tanzania kuwa Taifa la aina yake [Unique] ambayo ni heshima.
Mimi ni mfuasi wa IMANI Kuwa kila jambo linaloendeshwa na binadamu yoyote duniani linawezekana kwa mwingine pia. Naamini watanzania wanaweza kuwa TAIFA la kupigiwa mfano. Tunakila kitu kutufikisha hapo kuwa Taifa lenye maendeleo, tuna madini, maliasili, ardhi safi na bora, na hata maliasili watu.
Tunaitaji silaha moja USALAMA WA TAIFA kuwa na nguzo BORA na IMARA pekee kuliokoa TAIFA na kusimamia mikakati yote kwa jicho Chanya [Positive] la Ujenzi wa Taifa na kupambana na wahujumu chanya [Negative] dhidi ya Taifa.
Katika dhama hizi za leo kuendelea kuamini lolote linalohusu Usalama ni SIRI,jamani nikupoteza Taifa linaloitwa Tanzania. Ndio ni kweli Lazima yanayoendelea Ndani ya Idara [ambayo napenda kuona siku moja soon ikibidi inakua TAASISI] yanaendelea kuwa SIRI, na hata ikibidi baadae miaka Ishirini lilokuwa SIRI linaachiwa kuwa sio siri tena,kwani inasaidia kuleta tafakari baadae ni kwanini uamuzi huo ulichukuliwa, kwa faida ya Taifa. Kwani kama idara [Taasisi] nao ni watu wanaitaji kupumua kwani kikombe kikijaa maji ama chai umwagika.
Je tumefika hapa tulipo kwa Sheria za kibabe kama hiyo hapo juu ya Usalama wa Taifa 1996 ibara ya5:2(1) ili kuua nchi ama kujenga nchi?