Sheria ya Wachezaji Watano tu wa Kigeni kwa kila mechi inaenda kuua soka Tanzania


Hao wa ndani mmewatengeneza au mnaokoteza. tutaendelea kuwa kichwa cha wendawazimu tu hamna namna
 
Kama hujui kitu ni vyema ukakaa kimya, unaifahamu EPL ile ligi ya taifa la malkia?

Ka unaifahamu Top 8 teams zote za EPL zinawachezaji wangapi wazawa wa malkia? England national team unaifahamu ni timu ya daraja gani?
Unaijua La liga Santander?
Unafahamu top 4 teams za La liga zina foreign players wangapi?

Ama kweli ukiwa mwana CCM unakuwa huna akili leo nimeamini.
 
Akina Samata, msuva, ulimwengu, faridi,nk wajiandae nao kukaa benchi maana wameenda kuua vipaji vya nchi walikokwenda kucheza
Yani wadau wa michezo tunaangaika kuhamasisha wachezaji kwenda nje wao wanazuia wale wa nje kuja nchini kwetu.

Hivi Jupiter league ya Belgium ingekuwa ina sheria za kidada kama hizi za mwakyembe Samatta ambaye anamuhusudu kama Mungu mtu hadi anaacha kulala anakwenda kumpokea JKNIA usiku wa manane angekuwa wapi?

Mwakyembe pombe kali acha!
 
Tz tuna vipaji sana,tatizo wachezaji wetu hawajitambui,msimu huu yupo vizuri baada ya muda mfupi unamkataa,wachezaji wa kigeni wanaleta ushindani Kiasi,na waamuzi ni vilabu na bodi ya ligi,Mwakyembe ni maoni yake tu
 
Kanuni isiyo na faida
 
Unaleta ubaguzi kwa wachezaji wa mataifa mengine wakati hapo hapo na wewe unataka wachezaji wa taifa lako wacheze mataifa mengine na wapate namba...

Unafki wa namna hii ndo unafanya tuchelewe kupata maendeleo
 
Kwa karne hii ya soka la ushindani likitawaliwa na nguvu ya fedha hilo suala halitawezekanaaa
 
Hivi hawa watu mbona hawana kumbukumbu hata miaka kumi haijapita kulikua na sheria ya kua na wachezaji wa kigeni watano, Je timu ya taifa ilikua inafanya nini?
Ni bora kua na wachezaji wengi wa kigeni ili kama tutapata wachezaji wadhawa wanapata namba wawe ni wazr zaidi ili pia kuisaidia timu ya taifa. Kuliko kuja michezaji midhawa afu wote wakawa vipofu.
Ili mjinga umtoe ujinga muweke kati kati ya werevu wengi, sio unaenda kuweka kati kati ya wajinga tena.
 
Wachezaji wetu hawajitumi kabisa wanategemea hizo nafasi maalumu wagombanie nafasi za kucheza sio mbeleko... Kama bocco alivyofanya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…