Sheria yetu ya Uhamiaji ni kweli iko hivi?

PascalFlx

Member
Joined
Feb 11, 2009
Posts
68
Reaction score
5
Wiki iliyopita, niliwasili katika uwanja wetu wa kimataifa JK Nyerere, katika moja ya safari zangu nje ya nchi., Kwa bahati mbaya ticket yangu ilikuwa na matatizo nikaambiwa nikae katika madawati upande wa kulia kama unaingia katika sehemu ya kukabidhi mizigo wakati wanashughulikia tatizo langu.

Wakati nasiubiri utatuzi wa suala langu hapo ndipo niliposikia vilio ya wageni waliokuja kuitembelea nchi yetu, wakiwa wameketishwa katika madawati hayo bila kujua hatima ya masuala yao.

kati ya hao kuna watu watatu waliokuwa na tatizo moja, wawili wakitoe nchi ya Cameroon na mmoja Nigeria. Raia hao wa nchi za Africa walikuwa wamezuiwa na maafisa wa Uhamiaji kurejea nchini kwao kwa kigezo cha kwamba wanarejea nchini mwao kwa kutumia Shirika la Ndege TOFAUTI na lile waliloingilia nchini, jamani ni kweli sheria yetu ya uhamiaji iko hivi?, kama ni kweli basi tuna tatizo kubwa ambalo linahitaji kufanyiwa marekebisho.

Vijana hao walikuwa wanalalamika sana kwani walikuwa hawajui what to do next kwani ndege zao zilikuwa zimeshaondoka na hawajui wamuone nani au wafanye nini. Kusema kama mtanzania imenisikitisha kuona mtu anazuiliwa kurudi nchini kwake kwa kigezo kama hicho. ningeelewa kama wangemzui kuingia kwa kigezo cha kutokuwa na return ticket, Lakini kama aliruhusiwa kuingia na one way ticket ni kwanini alazimishwe kurejea kwao kwa shirika hilo hilo?.

Hata katika nchi zenye sheria kali za uhamiaji hawana sera kama hizi wakati unapotaka kuondoka katika nchi hiyo. Sheria kama hii kama ni kweli ipo inaharibu mazuri yote ambayo mgeni aliyafurahia alipokuwa nchini. Hebu naomba mnisaidie ni kweli mgeni anapoondoka nchini anatakiwa kutumia shirika la ndege hilo hilo aliloingilia nchini hata kama aliingia na one way ticket?. na kama shirika hilo limesitisha kutoa huduma Tanzania sheria hii inatumikaje?

Tatizo langu lilipotatuliwa niliondoka na kuwaacha hapo sijui hatima yako ilikuwaje, ila ilinisikitisha
 
dah mkuu habari yako imenisikitisha na kunihuzunisha sana kiukweli siijui sana sheria ya uhamiaji ila nafikiri kuna mapungufu mengi hapo
 

Unauhakika kuwa walikuwa wanarudi nchini mwao?
 
yes uhakika nilikuwa nao, but who cares so long as they leave the country, hata Marekani ukitaka kuondoka nchini mwao hawakuzuii. what's the point kumzuia mtu kuondoka nchini?. hapa tunazungumzia Sheria ya uhamiaji je ni kweli iko hivi?
 
hakuna uhusiano kati ya usafiri na sheria ya uhamiaji ya mwaka 1995 hivi vitu viwili vinajieleza vyenyewe (res ipsa loguitur). naona mtoa mada aitha hukuwaelewa au ulidanganywa.ili upate uhakika zaidi ungehakikisha na upande wa pili wanasemaje ( kwa nini watu hao waliwazuia ) ndio ungepata jibu kamili.na nna iman kutakuwa na sababu nyingine tu.hvyo mtoa mada umeleta habari isiyokamilika ambayo inawek mianya mingi.humbly submitted
 
hakuna uhusiano kati ya usafiri na sheria ya uhamiaji ya mwaka 1995 hivi vitu viwili vinajieleza vyenyewe (res ipsa loguitur). naona mtoa mada aitha hukuwaelewa au ulidanganywa.ili upate uhakika zaidi ungehakikisha na upande wa pili wanasemaje ( kwa nini watu hao waliwazuia ) ndio ungepata jibu kamili.na nna iman kutakuwa na sababu nyingine tu.hvyo mtoa mada umeleta habari isiyokamilika ambayo inawek mianya mingi.humbly submitted
 
Hadithi yako hii nahisi haina ukweli wa kutosha. Hata siku moja Uhamiaji hawawezi kufanya hilo. Criminal Psychology inaniambia inawezekana uliyoyasikia ni malalamiko yao 'pembeni' ku-pre-empty tatizo la msingi. Nabaki na labda!
 
Kazi ya uhamiaji ni kuwakaribisha, kuwasafirisha na kulinda mipaka yetu. Jukumu la pili na kuwapa wananchi hati za kusafiri nchi jirani na zile za ng'ambo. Wala hawaangalii ulikuja na nini ila wanaangalia hati zako zipo safi? Huu wimbo unapatikana TBC swahili.
 
Kwa uzoefu nilionao, raia wa cameroon na nigeria yawezekana walizuiwa kutokana na aidha kumiliki pasipoti bandia au viza zao kuisha muda bila ya kuripoti uhamiaji kupata extension, sasa walitaka kusafiri wakati muda ushakwisha lazima wang'ang'aniwe ili kulipia muda walioutumia kuvuta hewa ya Tanzania burebure...! Nawasilisha
 

Chukua mia.
 

Hao si ndo kila siku wanatutumia email za kitapeli? Kifungu cha sheria ya uhamiaji kinamruhusu afisa uhamiaji kumhoji, kumkagua na kumtia nguvuni mtu yeyote yule anayetaka kuingia au kutoka nchini ikiwa ataonekana kutaka au kuvunja kifungu chochote cha sheria hiyo....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…