Wiki iliyopita, niliwasili katika uwanja wetu wa kimataifa JK Nyerere, katika moja ya safari zangu nje ya nchi., Kwa bahati mbaya ticket yangu ilikuwa na matatizo nikaambiwa nikae katika madawati upande wa kulia kama unaingia katika sehemu ya kukabidhi mizigo wakati wanashughulikia tatizo langu.
Wakati nasiubiri utatuzi wa suala langu hapo ndipo niliposikia vilio ya wageni waliokuja kuitembelea nchi yetu, wakiwa wameketishwa katika madawati hayo bila kujua hatima ya masuala yao.
kati ya hao kuna watu watatu waliokuwa na tatizo moja, wawili wakitoe nchi ya Cameroon na mmoja Nigeria. Raia hao wa nchi za Africa walikuwa wamezuiwa na maafisa wa Uhamiaji kurejea nchini kwao kwa kigezo cha kwamba wanarejea nchini mwao kwa kutumia Shirika la Ndege TOFAUTI na lile waliloingilia nchini, jamani ni kweli sheria yetu ya uhamiaji iko hivi?, kama ni kweli basi tuna tatizo kubwa ambalo linahitaji kufanyiwa marekebisho.
Vijana hao walikuwa wanalalamika sana kwani walikuwa hawajui what to do next kwani ndege zao zilikuwa zimeshaondoka na hawajui wamuone nani au wafanye nini. Kusema kama mtanzania imenisikitisha kuona mtu anazuiliwa kurudi nchini kwake kwa kigezo kama hicho. ningeelewa kama wangemzui kuingia kwa kigezo cha kutokuwa na return ticket, Lakini kama aliruhusiwa kuingia na one way ticket ni kwanini alazimishwe kurejea kwao kwa shirika hilo hilo?.
Hata katika nchi zenye sheria kali za uhamiaji hawana sera kama hizi wakati unapotaka kuondoka katika nchi hiyo. Sheria kama hii kama ni kweli ipo inaharibu mazuri yote ambayo mgeni aliyafurahia alipokuwa nchini. Hebu naomba mnisaidie ni kweli mgeni anapoondoka nchini anatakiwa kutumia shirika la ndege hilo hilo aliloingilia nchini hata kama aliingia na one way ticket?. na kama shirika hilo limesitisha kutoa huduma Tanzania sheria hii inatumikaje?
Tatizo langu lilipotatuliwa niliondoka na kuwaacha hapo sijui hatima yako ilikuwaje, ila ilinisikitisha