Naomba ufafanuzi, Mfano mtu alinunua kiwanja ambacho kimejengwa nyumba baadaye anakuja kaka wa muuzaji na kusema apewe percent kwani alihusika katika vifaa baadhi vya ujenzi kama milango na tofali kadhaa, hapo nani anakua na haki?.
Mimi nadhani vitu vingine hata kisheria ni kusumbua watu tu, kama umenunua kiwanja na kina nyumba maana yake amekuuzia vitu vyote vilivyomo kwenye kiwanja. Huyo anaedai alihusika katika milango nadhani amfate aliepewa pesa ya mauziano kulikoa kuanza kumsumbua mnunuaji.