Sheria za Kazi: Uliza Ujibiwe

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,307
Reaction score
25,932
Salamu zenu waungwana,

Nawakaribisha kwenye bandiko hili ili tuweze kuulizana na kujibiana kuhusu Sheria za kazi hapa nchini Tanzania. Mimi pamoja na wasomi wenzangu wa sheria wenye nia kama yangu ya kutoa elimu, ingawa ni kwa ufupi, tutajibu maswali yenu wadau.

Tujitahidi kuuliza maswali yanayoeleweka na ya uhalisia.Karibuni sana!
 
sheria inatamka vipi mimi kupanda cheo katika kampuni binafsi? Nilazima kampuni inipandishe cheo?
 
hatutaki sheria za kazi hapa tunataka mafao yetu tu. hatuna muda wa kusubiri 55 yrs. Kama hakuna jibu katika hili hata hizo sheria hazina maana.
 
hatutaki sheria za kazi hapa tunataka mafao yetu tu. hatuna muda wa kusubiri 55 yrs. Kama hakuna jibu katika hili hata hizo sheria hazina maana.
Kama ungejua kuwa hata hiyo 55 ni kwa mujibu wa sheria ungenyamaza tu
 
hatutaki sheria za kazi hapa tunataka mafao yetu tu. hatuna muda wa kusubiri 55 yrs. Kama hakuna jibu katika hili hata hizo sheria hazina maana.
Ulimpigia nani kura? Jibu hapo halafu tujadili kujitoa
 
kwa hiyo tukimaliza mkataba na 30yrs tuendelee kusubiri tu mpaka 55yrs kwa maana ni sheria?
Unachanganya mada.
Hilo ni fao la kujitoa ambalo kwa mapendekezo ya mabadiliko ya sheria ambayo bado haijapita linataka kufutwa.
Kukasirika haisaidii. Dawa ni kupaza sauti kupitia mikutano ya wadau hata kumwandikia spika wa bunge barua rasmi ukionyesha hoja zako. Usimsahau mbunge wako.
Haya mambo hayataki hasira.
 
Nimestaafu nadai mafao yangu ambayo yko kwenye staff regulation za shirika kama kupewa benefit fulani fulani. Kwa ajili ya kukosa fedha wamenipa barua kuwa tukipata tutakulipa. Now it is two years. limitation period inasemaje katika situation kama hii.
 
Hii sheria itatufanya tufe napema kwa kigezo cha kusubiri pesheni

Let's say mtu unapiga kazi hadi 40 years, unataka uachane na kazi etu usubirie miaka 15 mbele!!!!!! Ili upate pensheni yako

Ccm imefikia ukomo bora iondoke tu

Yaani ha

hatutaki sheria za kazi hapa tunataka mafao yetu tu. hatuna muda wa kusubiri 55 yrs. Kama hakuna jibu katika hili hata hizo sheria hazina maana.
 
Kuhusu retrenchment na re employment inasemaje? Kuna kampuni ilini retrench kisa kazi hamna sasa imepata kazi ya muda inataka kuleta wageni Hali mimi nipo sina kazi
 
hatutaki sheria za kazi hapa tunataka mafao yetu tu. hatuna muda wa kusubiri 55 yrs. Kama hakuna jibu katika hili hata hizo sheria hazina maana.
Yap!....Umenena mkuu...nasubiri jibu na mimi

mafao yetu...kwa nini tunyimwe?
 
Pole. Nina swali la kutaka kujua maana yapo mafao ya aina kama mna mkataba wa hiari au staff regulations zilizoidhinishwa na mamlaka husika.
1. Yapo mafao yanayolipwa na mwajiri.Hapa inabidi pamoja na barua ya kustaafu akokotoe kila kipengele ujue unadai shilingi ngapi.
2. Yapo mafao ambayo unalipwa na mifuko ya hifadhi za jamii baada ya mwajiri wako kuwasilisha michango kwa wakati. Ilibidi uwe umechukua statement kwenye mfuko kuona kama michango yako imewasilishwa na hakuna mapengo.

Swali unasubiri na.1 au 2 au vyote?
 
Hii sheria itatufanya tufe napema kwa kigezo cha kusubiri pesheni

Let's say mtu unapiga kazi hadi 40 years, unataka uachane na kazi etu usubirie miaka 15 mbele!!!!!! Ili upate pensheni yako

Ccm imefikia ukomo bora iondoke tu

Yaani ha
Hii sheria sio ya ccm na haina siasa. Ili uweze kulipwa pensheni ni lazima uchangie si chini ya miezi 180 au miaka 15. Ndio maana unaambiwa huwezi ajiriwa kwa masharti ya pensheni kama una zaidi ya miaka 45. Wanataka kutimiza masharti ya sheria.
Ziko hesabu zake siwezi kuzimwaga hapa.
 
Kuhusu retrenchment na re employment inasemaje? Kuna kampuni ilini retrench kisa kazi hamna sasa imepata kazi ya muda inataka kuleta wageni Hali mimi nipo sina kazi
Sheria haimlazimishi mwajiri kumwajiri mtu. Swala la msingi ni je ulipopunguzwa kazi taratibu zilifuatwa? Ukilipwa stahiki zako?
Kama kazi zimepatikana una haki ya kuomba tena ila ujue utafikiriwa kama wengine na kama utendaji wako ulikuwa mzuri hawawezi kukuacha kama unakidhi vigezo.
 
Kama ninafanya kazi na sina mkataba, yaana nilikua na mkataba na uliisha lkn kampuni ilinipa mkataba mwingine na mm sikuukubali kwa ajir ya maslai, lkn wakanipa ahad kuwa endelea kufanya kaz tuu, baada ya miez mitatu tutakurekebishia mkataba wako, sasa mm nataka kuacha kaz, naandika barua ya kuacha kaz ili nipate stahiki zangu, je..!? kwa mujibu wa sheria ni haki kuandika hiyo barua na je sheria itanitaka nitumikie kampun kwa mda gani ili niweze kupata stahiki zangu, ikiwa pamoja na chet..!?

ahsante
 
Namba moja. Ni mafao ya kwenye shirika =staff regulations zilizoidhinishwa na mamlaka husika..
 
Huu unaitwa uzalendo....nami na offer architectural consultation kwa wana JF ambao project wanazotaka kuanzisha zina nufaisha jamii kwa namna moja ama nyingine!
 
Mkuu hii kazi ni nyeti na kwani sheria inasemaje kuhusu mwajiri kuleta mgeni kwa kazi ile ambayo wewe mzawa umepigwa chini ilhali umekuwa trained for more than 3yrs kufanya hiyo kazi na huwezi kuajirika kwingineko kwakuwa uko trained to work in that specific technology. Wanaleta watu wa nje kisa ni kazi ya miezi minne but what about me? Sina kazi na siajiriki kwingine:
 
Hivi mkienda CMA ukaambiwa Subiri uamuzi maana yake nini...!?
Yaani njoo siku Fulani uchukue uamuzi..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…