Sheria za kijeshi.

Sheria za kijeshi.

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,497
Reaction score
4,775
Naomba kujuzwa yafuatayo kwa wajuzi wa masuala ya jeshi.
1-je raia anaruhusiwa kuipigia bendera ya nchi saluti ?
2-iwapo askari alievaa sare atagoma kutoa kitambulisho,raia anaruhusiwa kupambana nae ili asipelekwe kokote ?
*ikitokea raia amefanya hivyo je sheria inamlinda vipi ?
3-je raia wa kawaida anaruhusiwa kumkamata askari ambae ametenda uhalifu hata kama amevaa sare ?
wajuzi wa sheria karibuni kwa msaada.
 
kwa uelewa wangu khs salute ni heshima anayotoa askari ambaye kavaa gwanda, askari anapokuwa hajavaa gwanda hukaza mikono miguu ikiwa mguu sawa na kunyanyua mwili hivyo basi raia anavyo simama kwa ukakamavu wakati wa kupandisha na kushusha bendera ni heshima ambayo ni sawa na saluti kwa askari mwenye uniform
 
Sheria mama za jeshi ni mbili tu.

1; The general is always right

2; If you think the general is not right refers to the rule number one.

Hizo zingine ni utaratibu wa kijeshi.
 
namba 2 katika sare nyingi za majeshi kuna nametag kwa askari polisi huwa kunakuwa na namba za askari hvyo basi kama hajatoa kitambulisho unaweza kumripoti kituo cha karibu ambapo atashughulikiwa kutokana na sheria za jeshi husika... na kisheria askari anayekuja kukamata kama hakuja na viongozi wa serikali inambidi aoneshe kitambulisho
 
no 3 raia haruhusiwi kumkamata askari aliyevaa uniform bali kutoa taarifa kituoni pamoja na details zake pia kijeshi hata askari polisi kumkamata askari jeshi aliyevaa gwanda hairuhusiwi bali kutoa taarifa kambini haf MPs watakuja kumkamata
 
Naomba kujuzwa yafuatayo kwa wajuzi wa masuala ya jeshi.
1-je raia anaruhusiwa kuipigia bendera ya nchi saluti ?
2-iwapo askari alievaa sare atagoma kutoa kitambulisho,raia anaruhusiwa kupambana nae ili asipelekwe kokote ?
*ikitokea raia amefanya hivyo je sheria inamlinda vipi ?
3-je raia wa kawaida anaruhusiwa kumkamata askari ambae ametenda uhalifu hata kama amevaa sare ?
wajuzi wa sheria karibuni kwa msaada.
note: hii na kwa uelewa wangu sina uhakika kisheria
 
Back
Top Bottom