Sheria za makazi mahala popote pale ndani ya Tanzania

Blue Bahari

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2016
Posts
1,851
Reaction score
2,171
Wakuu habarini!
Samahani leo nataka mnitoe tongotongo kuhusu sheria na utaratibu wa kupata makazi kwa yeyote ndani ya Tanzania.

Ni hivi, nimeshangaa kusikia katika kijiji kimoja mkoa fulani, ambapo kuna jamaa analamika kwamba viongozi wa kijiji wanamtaka alipe pesa (Tzs 150,000) kama kiingilio katika kijiji hicho kwa kuwa yeye "Si mzawa wa kijiji hicho". Jamaa alikuwa ameanza kujenga nyumba yake, sasa kwa kuwa PESA hana, viongozi wa kijiji wampiga marufuku kutoendelea na ujenzi mpaka pale atakapolipa hiyo PESA ( Tzs 150,000). Na jamaa kapigwa mkwara kwamba akikaidi agizo la kutoendelea na ujenzi, basi wao viongozi watakuja kubomoa.

Na ukiangalia huyo jamaa ni muuza Maji ya kwenye madumu kutembeza mitaani ,ambayo ndo PESA anayoitegemea kwa kila kitu. Aiesee nilishangaa kwa kuwa katika kuishi kwangu maeneo mbali mbali ya Tanzania sijawahi kumbana na kitu kama hicho na wala sijawahi sikia kuna vijiji ambavyo vina utaratibu kama huo, ndo ilikuwa Mara yangu ya kwanza kusikia kwake.

Lakini vile vile Mimi binafsi nikasoma katiba ya nchi (1977) nijiridhishe kama imeruhusu kuwekwa utaratibu kama huo, nimesoma lakini bado nafungwa na uelewa wangu mdogo wa masuala ya katiba na sheria.







Je ; kwa mnaofahamu ni kweli mamlaka za miji au vijiji vina ruhusa ya kufanya hivyo?
Karibuni kwa mjadala.


Utu ni mwema.
 
Kichwa cha habari, nimekosea. Badala ya kuandika "Ndani" nimeandika "nfani". Kuedit nimeshindwa.

Utu ni mwema.
 
Mimi siijui vyema sheria wala sijaisomea lakini ktk hili nahisi wanamuonea sana tena sana.nchi yetu ni huru kwa raia wake juu ya makazi,ndiyo maana unaweza kuta Msukuma anaishi kwa wapogolo,mchaga anaishi kwa waruli na mambo kama hayo.huyu ndugu atoe taarifa kituo cha police kimpe msaada w kunyanyaswa kwake.

JAH RASTAFARI MORNING AFRICA
 
Ndio maaana hata Mimi nimeshangaa kitendo kama hicho cha kumtaka alipie ada ya kuingilia kijijini. Kitu ambacho sikuwai kusikia mahala popote pale.

Utu ni mwema.
 
Kama Kiwanja alinunua kwao yaani kwa mwanakijiji basis ana haki ya kuendeleza ujenzi
. Vinginevyo aangalie na mila. Nyumba inaweza bomolewa na watu wasiojulikana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katiba ya inchi inasema kama mtanzania anaweza akaenda ....au akaishi popote TANZANIA mradi tu asivunje sheria.....hao wakuu wa KIJIJI NI WAPUUZI TU..ninachojuwa mm ukitaka kujenga huwa kunakuwa na KIBALI CHA UJENZI TU....ndy unapaswa kulipa tena HALMASHAURI YA MJI HUSIKA....na sio umpe MJUMBE AU MWENYEKITI WA MTAA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio hata Mimi nielewavyo..... Lakini hii ya kusema kulipia kiingilio mhhhhhh??????

Utu ni mwema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…