Blue Bahari
JF-Expert Member
- Aug 21, 2016
- 1,851
- 2,171
Wakuu habarini!
Samahani leo nataka mnitoe tongotongo kuhusu sheria na utaratibu wa kupata makazi kwa yeyote ndani ya Tanzania.
Ni hivi, nimeshangaa kusikia katika kijiji kimoja mkoa fulani, ambapo kuna jamaa analamika kwamba viongozi wa kijiji wanamtaka alipe pesa (Tzs 150,000) kama kiingilio katika kijiji hicho kwa kuwa yeye "Si mzawa wa kijiji hicho". Jamaa alikuwa ameanza kujenga nyumba yake, sasa kwa kuwa PESA hana, viongozi wa kijiji wampiga marufuku kutoendelea na ujenzi mpaka pale atakapolipa hiyo PESA ( Tzs 150,000). Na jamaa kapigwa mkwara kwamba akikaidi agizo la kutoendelea na ujenzi, basi wao viongozi watakuja kubomoa.
Na ukiangalia huyo jamaa ni muuza Maji ya kwenye madumu kutembeza mitaani ,ambayo ndo PESA anayoitegemea kwa kila kitu. Aiesee nilishangaa kwa kuwa katika kuishi kwangu maeneo mbali mbali ya Tanzania sijawahi kumbana na kitu kama hicho na wala sijawahi sikia kuna vijiji ambavyo vina utaratibu kama huo, ndo ilikuwa Mara yangu ya kwanza kusikia kwake.
Lakini vile vile Mimi binafsi nikasoma katiba ya nchi (1977) nijiridhishe kama imeruhusu kuwekwa utaratibu kama huo, nimesoma lakini bado nafungwa na uelewa wangu mdogo wa masuala ya katiba na sheria.
Je ; kwa mnaofahamu ni kweli mamlaka za miji au vijiji vina ruhusa ya kufanya hivyo?
Karibuni kwa mjadala.
Utu ni mwema.