Ndoa ya kanisani ni ndoa ya mke mmoja. Hivyobasi,ikifungwa hairuhusiwi kwa mume au mke kufunga nyingine tena isipokuwa kama mke au mume amefariki au ndoa husika imevunjwa na mahakama
Hautaruhusiwa Mkuu hadi:Asante mkuu,so kwa maana hiyo nikiwa tayari nina ndoa ya kanisa na nikataka kwenda kufunga nyingine ya bomani na mwanamke mwingine kisheria sitaruhusiwa kufanya hvyo?
Hautaruhusiwa Mkuu hadi:
(a) Kitokee kifo cha mmoja wa wanandoa
(b) Ndoa husika imevunjwa rasmi na Mahakama
Ndoa ya kiserikali yaweza kuwa kuwa ima ya mke mmoja au ya wake wengi. Hii yategemea makubaliano kati ya wanandoa na aina ya ndoa itakayoandikwa katika cheti husika cha ndoa hiyo. Ndoa ya Bomani yaweza kuwa ya wake wengi wanaoolewa siku moja au wengi wa siku tofauti.Au ya mke mmoja kama wanandoa walivyokubaliana.Asante sana mkuu,sasa unanipa mwanga,na je kama ndoa yangu ya awali ilifungwa kiserikali/bomani na si kanisani,je itakua ni kikwazo pia kufunga ndoa ya pili,kwa maana ya je ndoa ya kiserikali/bomani inaruhusiwa wake wangapi?asante mkuu
Ndoa ya kiserikali yaweza kuwa kuwa ima ya mke mmoja au ya wake wengi. Hii yategemea makubaliano kati ya wanandoa na aina ya ndoa itakayoandikwa katika cheti husika cha ndoa hiyo. Ndoa ya Bomani yaweza kuwa ya wake wengi wanaoolewa siku moja au wengi wa siku tofauti.Au ya mke mmoja kama wanandoa walivyokubaliana.
Kikwazo pekee cha kufunga ndoa ya pili baada ya ile ya Bomani ni aina ya ndoa itakayoandikwa katika cheti. Cheti chaweza kuandikwa 'ndoa ya mke mmoja' au 'ndoa ya wake wengi'.Nisisitize kuwa aina hizo za ndoa hutegemea makubaliano ya awali ya wanandoa kabla ya kufunga ndoa hiyo.
una plan kuwa na wake wangapi?Mkuu kutaka kujua sio kua ndio nataka funga ndoa,bali ni kutaka kujifunza tu!me ndoa bado mkuu