Sheria za ndoa!

Sheria za ndoa!

1800

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2010
Posts
2,215
Reaction score
604
Wadau naomba kujuzwa,nina utata kidogo juu ya sheria za ndoa,mfano mimi nikiwa mkristu na nimefunga ndoa ya kanisani,je nitaruhusiwa kisheria kufunga ndoa nyingine bomani(ya kiserikali)? na kama nina ruhusiwa je bomani naweza funga ndoa ngapi?kwa maana ya je kuna limitation yeyote ya idadi ya ndoa!naombeni mnifungue macho!asanteni
 
Ndoa ya kanisani ni ndoa ya mke mmoja. Hivyobasi,ikifungwa hairuhusiwi kwa mume au mke kufunga nyingine tena isipokuwa kama mke au mume amefariki au ndoa husika imevunjwa na mahakama
 
Asante mkuu,so kwa maana hiyo nikiwa tayari nina ndoa ya kanisa na nikataka kwenda kufunga nyingine ya bomani na mwanamke mwingine kisheria sitaruhusiwa kufanya hvyo?
 
Hautaruhusiwa Mkuu hadi:

(a) Kitokee kifo cha mmoja wa wanandoa

(b) Ndoa husika imevunjwa rasmi na Mahakama
 
Asante sana mkuu,sasa unanipa mwanga,na je kama ndoa yangu ya awali ilifungwa kiserikali/bomani na si kanisani,je itakua ni kikwazo pia kufunga ndoa ya pili,kwa maana ya je ndoa ya kiserikali/bomani inaruhusiwa wake wangapi?asante mkuu
 
Ndoa ya kiserikali yaweza kuwa kuwa ima ya mke mmoja au ya wake wengi. Hii yategemea makubaliano kati ya wanandoa na aina ya ndoa itakayoandikwa katika cheti husika cha ndoa hiyo. Ndoa ya Bomani yaweza kuwa ya wake wengi wanaoolewa siku moja au wengi wa siku tofauti.Au ya mke mmoja kama wanandoa walivyokubaliana.

Kikwazo pekee cha kufunga ndoa ya pili baada ya ile ya Bomani ni aina ya ndoa itakayoandikwa katika cheti. Cheti chaweza kuandikwa 'ndoa ya mke mmoja' au 'ndoa ya wake wengi'.Nisisitize kuwa aina hizo za ndoa hutegemea makubaliano ya awali ya wanandoa kabla ya kufunga ndoa hiyo.
 
Asante sana mkuu,hapo sasa umenipa mwanga wa kutosha juu ya aina na sheria za ndoa
 
Back
Top Bottom