Sheria za Soka za FIFA: Ifahamu Sheria namba Moja ya FIFA inayohusu Uwanja wa Soka

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Kwa mujibu wa Sheria hizo za FIFA (Shirikisho la Soka Duniani) mwaka 2015/16, mechi inaweza kuchezwa kwenye Uwanja wenye nyasi asilia au za kutengeneza ila nyasi za kutengenza lazima ziwe za rangi ya Kijani

Uwanja wa kuchezea lazima uwe wa umbo la Msatili ukiwa umewekewa alama za mipaka kwa mistari. Mistari ya Upande mrefu inaitwa 'touch line' na upande mfupi inaitwa 'goal lines'

Uwanja umetengenishwa katika nusu mbili na mstari wa katikati uitwao 'halfway line' na alama ya katikati ya uwanja huwekwa katikati ya mstari wa 'halfway line' ambapo duara la Nusu Kipenyo cha Mita 9.15 huwekwa kuzunguka alama hiyo

Vipimo vya kawaida vya Urefu wa 'touch line' vinaweza kuwa kati ya Mita 90 hadi Mita 120 lakini kwa Mechi za Kimataifa urefu wa 'touch line' unakuwa kati ya Mita 100 na Mita 110

Vipimo vya kawaida vya urefu wa 'goal line' ni kati ya Mita 45 na Mita 90 na kwa mechi za Kimataifa urefu wa 'goal line' ni kati ya Mita 64 na Mita 75. Mistari hiyo ya mipaka inatakiwa kuwa na upana wa Sentimita 12

2.PNG

3.PNG

Kibendera kinachokaa katika kona za Uwanja kinakuwa na urefu wa usiopungua Mita 1.5 na kinachokaa mwishoni mwa 'halfway line' (sio lazima) ninatakiwa kuwa kuwa Mita moja kutoka 'touch line'

Robo Duara lenye nusu Kipenyo cha Mita 1 kutoka kona zote za kibendera hicho huchorwa ndani ya uwanja wa kuchezea

4.PNG

Goli linakuwa katikati ya mistari ya 'goal lines' na milingoti ya goli inaweza kutengenzwa kwa mbao, chuma au malighafi yoyote iliyothibitishwa. Upana wa goli ni Mita 7.32 na urefu ni Mita 2.44

Neti inaweza kuwekwa kwenye goli na ikagusa ardhi nyuma ya goli hilo ilimradi tu imewekwa kwa uzuri na haimsumbui Mlinda mlango

Milingoti ya goli na crossbar (Mwamba wa Juu) lazima viwe vya rangi nyeupe

Milingoti ya Goli inatakiwa kusimikwa vizuri ardhini ili kuimarisha usalama, magoli yanayoweza kuhamishika hutumika iwapo tu yatafikia viwango hivyo na kuwa sawa na yaliyosimikwa ardhini

5.PNG

NB:
Ambapo teknolojia ya mstari wa goli (Goal-Line Technology - GLT) inatumika, marekebisho kwa goli yanaweza kuruhusiwa lakini lazima iwe kulingana na maelezo yaliyoainishwa ndani Programu ya Ubora wa FIFA kwa GLT na kulingana na maelezo hapo juu ya Goli
 
Safi mkuu ukiweka nyingine nitag
 
Back
Top Bottom