Sheria za usalama barabarani

Sheria za usalama barabarani

Marire

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2012
Posts
12,333
Reaction score
5,292
Wakuu heshima kwenu.

Nilikuwa kwenye safari trafiki wakampiga faini dreva wetu wa bus pale kibaha stand kisa alipiga overtake kwenye msitari iliyochorwa barabarani inayokataza overtake.

Baada ya hapo tulivyoaendelea na safari niliiona misitari katikati ya barabara aina tofauti na abiria niliyekuwa naye ni kama mimi tu hajui chochote.

Kama kuna wadau wanajua embu toeni elimu kidogo.
 
Mstari mweupe ulioungana unakuzuia ku-overtake.

Mstari mweupe ulio katika vipande vipande unakuruhusu ku-overtake kama mbele ni salama.

Hayo ni machache ninayofahamu kuhusu mistari hiyo.
 
mstari mweupe then pembeni yake vipande vipande?
 
Hapo sikumbuki vizuri ngoja wanaofahamu zaidi waje watusaidie.

Katikati kukiwa na mistari miwili, mmoja umekatika na mwimgine haujakatika, basi yule alieko upande uliokatika anaruhusiwa ku over take, wa upande wa pili mstali haujakatika haruhusiwi ku over take, hii ipo sana baada ya kumaliza kona ya barabara.
 
mstari mweupe then pembeni yake vipande vipande?

vipande vikiwa upande wako unaruhusiwa ku-overtake......sehemu nyingine mstari upande wako umenyooka ila upande mwingine una vipande vipande wewe huruhusiwi ku-overtake ila wa upande mwingine anaruhusiwa.
 
Kwa kifupi ni kuwa ukiona mstari umeunganika ni kuwa huruhusiwi ku overtake..na kama umekatika katika basi unaruhusiwa ku overtake...kama iko miwili unaangalia ule mstari ulio upande wako (mstari wa ndani tuseme) unaonyesha nini..kama iilivyo hapo juu..

Na ukiona mistari meupe miwili haijakatika hapo ndo hata usifikirie ku overtake kabisa..kama yote miwili imakatika basi wote wawili (wa pande zote mbili wanaweza ku overtake)
 
Asanteni sana wakubwa nami nimeelimika.
 
~mistari ikiwa miwili imeunganika kumbe si ruhusa ku overtake nimeelemika leo
 
alafu kuna siku nilimuone trafiki akiendesha gari kasi na hakuwa amefunga mkanda nani anapaswa ampige faini?
 
Mh? Hapo pagumu ngoja tena tusubiri wenye kufahamu hilo jambo watuweke sawa.
 
alafu kuna siku nilimuone trafiki akiendesha gari kasi na hakuwa amefunga mkanda nani anapaswa ampige faini?

Magari mengi mabovumabovu (taxi na daladala) ukiulizia ni ya matrafiki/ ukiona daladala inavunja sheria sana ujue ni ya trafic, ukiona dereva wa daladala mjeuri sana ujue ni ya trafic, wao ndio wako msitari wa mbele ktk kulea uvunjaji wa sheria kwenye magari yao. Ukimuona dereva wa daladala amekamatwa halafu anapiga simu ujue anaongea na afande na mara utasikia "huyo ni kijana wangu mwachie". Hata baadhi ya askari wanakatishwa tamaa kutekeleza majukumu yao. Hii ndio TZ.
 
Katikati kukiwa na mistari miwili, mmoja umekatika na mwimgine haujakatika, basi yule alieko upande uliokatika anaruhusiwa ku over take, wa upande wa pili mstali haujakatika haruhusiwi ku over take, hii ipo sana baada ya kumaliza kona ya barabara.

Vilevile ipo kwenye miinamo na miinuko
 
Back
Top Bottom