sheria

sheria

ludevu junior

Member
Joined
Jul 31, 2013
Posts
7
Reaction score
1
Natamani kuwa mwanasheria lakini nina tatizo la kutetemeka ninapoamua kusimama ili niongee mbele za watu, je nifanyeje kuondokana na tatizo hili?
 
Vuta bangi kwanza thn changanya na viroba uone kama hilo tatizo litaendelea kuwepo.
 
Hiyo ni hofu tu...na isikufanye usitimize ndoto zako!!
 
Natamani kuwa mwanasheria lakini nina tatizo la kutetemeka ninapoamua kusimama ili niongee mbele za watu, je nifanyeje kuondokana na tatizo hili?

hahahaha jiamini tu mkuu utafanikiwa, jenga tabia ya kujiamini
 
lack of coffidence which facing you due to many reasons
like
bad/poor wearing/dressing
poor point planing before audience/pre presentation and so so so
but don't giveup knowing problem is half of solving it!
 
Naunga mkono hoja!!!
 
piga bia zako mbil then nenda kwny presentation m ninatatzo ilo lakn kuna jamaa kanishaur ivyo lakn ndio good way 4 me
 
Thanks a lot guys, nafikiri hilo la kunywa bia, huwa linanisaidia sana, japo sio mbili kama alivyoshauri ndugu Oil Sumu. Bado napokea comments
 
Natamani kuwa mwanasheria lakini nina tatizo la kutetemeka ninapoamua kusimama ili niongee mbele za watu, je nifanyeje kuondokana na tatizo hili?

hilo ni tatizo dogo sana,na kwakuwa umeshalitambua basi cha msingi anza kujizoeza kuzungumza na kuchangia hoja sehemu yoyote utakayokuwa aidha vijiweni,makongamano,mikutano,harusini,n.k hii itakusaidia kuondoa woga,hofu na kukufanya ujiamini zaidi,hata mm nilikuwa hivyohivyo ila kwa sasa sishikiki.
 
mm nikiingia chuo kama kuna representation napga bia zangu 2 tu
 
Natamani kuwa mwanasheria lakini nina tatizo la kutetemeka ninapoamua kusimama ili niongee mbele za watu, je nifanyeje kuondokana na tatizo hili?

1. Tambua kwamba kutetemeka siyo tatizo. It's just the way your body responds to eternal stimuli. Wewe unatetemeka, mwingine anatoka jasho au mwili unakuwa baridi. Hizi zote ni responses hakuna bora au mbaya kuliko nyingine.
2. Unaweza kabla ya kuongea mbele ya watu ufanye 'aerobic exercises' ili mapafu yapate hewa safi ya kutosha. Tafuta sehemu tambarare kama kitanda au sakafu - taratibu vuta hewa ndani mpaka hapo utakaposhindwa kuvuta zaidi. Kisha achia taratibu taratibu na vuta tena kama ulivyofanya awali na kuachia taratibu. Kuvuta na kuachia - hesabu hadi 50, lakini pia unaweza kufanya zaidi kama una nafasi. Zoezi hili linasaidia kulegeza misuli (linakufanya uwe relaxed) na ukiongea mbele ya watu kule kutetemeka kutapungua. Kama utalipatia vizuri, utaona kwamba mwishoe kutetemeka kutaisha kabisa.
3. Unaweza kujipangia ratiba yako kila siku - mfano, asubuhi, mchana, jioni na usiku. Ni zoezi pia linalofaa kwa ajili ya kupata peace of mind or concentration. Kama unasoma, unaweza kulitumia - mfano, dk 15 au zaidi kabla ya study time na kisha unaanza kujisomea. Kama umechaguliwa kusoma risala, fanya robo saa au dk 20 kabla ya kusoma risala. Unaweza pia kufanya taratibu ukiwa na wenzako hata kama umekaa au umesimama kuvuta hewa taratibu na kuiachia kwa muda bila wenzako kukugundua unachofanya. Hapa nasemea kama utahitaji katika mazingira kama hayo, lakini muda mzuri ni pale ukiwa peke yako. Ili upate concentration nzuri unaweza kufumba macho na unapovuta hela ndani (inhale) tumia pua na unapoiachia (exhale) tumia mdogo kwa kuufungua ili ipite na hakikisha unatoa hewa hadi pale utakaposhindwa kutoa zaidi. Zoezi hili unaweza kulifanya pia kama unaenda kukutana na mpenzi wako kwa mara ya kwanza, kwenda kuomba kazi/kufanya interview, kwenda kuhojiwa polisi au kutoa ushahidi/kujitetea mahakamani.
4. Jaribu kila siku na kila mara unapohitaji na utaniambia mafanikio yake. It's a relaxation exercise.
5. Na unajua kwa nini unatetemeka? Ni kwa sababu hutaki au unaogopa kukosea maana unataka kila kitu kifanyike vizuri. Matokeo yake, hali hiyo inakujengea hisia za kujiuliza maswali - Je, sitakosea? Wenzangu/watu watanifikiriaje? Nitaweza kweli etc? Asante!
 
Thanks a lot guys, nafikiri hilo la kunywa bia, huwa linanisaidia sana, japo sio mbili kama alivyoshauri ndugu Oil Sumu. Bado napokea comments

Mimi nakushauri usitumie bia kama suluhisho kwa hali hii. Ukizoea utakuwa 'addicted' (yaani bila kupiga bia hutaweza kuongea mbele ya watu). Kama unatumia bia, tumia tu kama kinywaji au interaction na wenzako. Kuna jamaa amezoea kunywa whisky au brandy (yeye ni mwalimu) na imetokea kwamba bila kuweka jamaa hawezi kufundisha na akishagusa tu anafanya vizuri ajabu. Kwa maneno mengine, asipokunywa whisky au brandy kabla ya kufundisha, anakuwa dull na wanafunzi wanaboeka. Lakini akitumia anakuwa mchangamfu sana na wanampenda. Kwa vile wanafahamu hivyo, wakiona kuna siku yuko dull wanamnunulia kitoti cha brandy au whysky ili awape lecture nzuri. Si, unaona ameshakuwa addicted huyo? Hivyo, achana na bia kama solution kwa tatizo hilo. Fuata zoezi nililoeza hapo juu.
 
Utakapoanza kusoma sheria utajenga confidence maana masomo yenyewe yanakujenga Kisakolojia kujiamini. Hata kama wewe ulikuwa si muongeaji utajikuta unajua kuongea kwa confidence na itakapokuja wakati wa masomo yako hizo presentation zitajenga. Sheria ni sawa na Mwanajeshi kujiamini

Vuta bangi kwanza thn changanya na viroba uone kama hilo tatizo litaendelea kuwepo.
 
Back
Top Bottom