Shetani ananifahamu, na Yesu anamjua, wewe je, shetani anakufahamu?

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
6,238
Reaction score
8,194
Mapepo, mashetani na wachawi wananifahamu sana kuwa nimeokoka na sina mchezo na dhambi.

Wiki iliyopita, walijaribu kunishambulia kama walivyomfanyia Ayubu. Mdomo wangu ulivimba ghafla ukawa mwekundu.

Kama kawaida, kimbilio langu la kwanza ni Jina la Yesu. Niliukemea uvimbe huo kwa Jina la Yesu, ukatoweka baada ya muda mfupi. Jana, mashetani yalikuja tena. Yakaniletea uchovu mwingi na ulegevu mwili wote. Mwanzoni nilifikiri ni uchovu tu kwa sababu wikiendi nilifanya sana kazi. Hivyo nikajilaza kitandani nipumzike. Nilipumzika ya kutosha, uchovu haukuisha. Nikajua ni mashetani. Nikayakemea kwa Jina la Yesu. Within seconds, uchovu wote, kwishney!

Dah, kwa kweli ni raha sana kukaa ndani ya Yesu. Mashetani yananifahamu kuwa mimi ni mtoto wa Mungu. Nikiyaamuru yatoke yanakimbia mbio. Hii ni mojawapo ya faida za kuokoka.

Kama hujaokoka, ukikemea mapepo hayawezi kutoka, maana yanafahamu vizuri wewe ni nani na kwamba huna mamlaka ya kuyakemea. Na usipoangalia yanaweza hata kukujeruhi.

Matendo 19:15
Yule pepo mchafu akawajibu, akawaambia, Yesu namjua na Paulo namfahamu, lakini ninyi ni nani? Na yule mtu aliyepagawa na pepo mchafu akawarukia wawili, akawaweza, akawashinda, hata wakatoka mbio katika nyumba ile wakiwa uchi na kujeruhiwa.
 
SAWA,Tuombee na sisi tuwe na Nguvu hizo!
 
samahan ivi kuokoka n nini?
 
Ukitaka kuwa na mamlaka ya kiroho juu ya mapepo, lazima uokoke na ukae ndani ya Yesu Kristo. Waliookoka wana mamlaka ya kufukuza mapepo kwa Jina la Yesu! Watu ambao hawajaokoka hawana mamlaka dhidi ya mashetani, kama ilivyokuwa kwa hao wana wa Skewa (Matendo 19:15-16).
 
Shetani huwa ni muongo
Akisema anamjua fulani huenda mtego huo!
Ni kweli shetani ni muongo, lakini anamjua Yesu, anamfahamu Paulo na mimi ananifahamu. Ndio sababu akija kwangu nikimkemea kwa Jina la Yesu anakimbia. Anajua kabisa nimepewa mamlaka ya kumfukuza.

Lk 9:1
Akawaita wale Thenashara, akawapa uwezo na mamlaka juu ya pepo wote na kuponya maradhi.

Kila mtu aliyeokoka ni mwanafunzi wa Yesu, hivyo amepewa mamlaka juu ya pepo wote na kuponya maradhi, kama hao Thenashara.
 
samahan ivi kuokoka n nini?
Bila samahan, soma kwa makini uzi huu👇, utajua maana ya kuokoka:
 
Ni kweli shetani ni muongo, lakini anamjua Yesu, anamfahamu Paulo na mimi ananifahamu. Ndio sababu akija kwangu nikimkemea kwa Jina la Yesu anakimbia. Anajua kabisa nimepewa mamlaka ya kumfukuza.

Lk 9:1
Akawaita wale Thenashara, akawapa uwezo na mamlaka juu ya pepo wote na kuponya maradhi.

Kila mtu aliyeokoka ni mwanafunzi wa Yesu, hivyo amepewa mamlaka juu ya pepo wote na kuponya maradhi, kama hao Thenashara.

Hakuna namna ya kuthibitisha kuwa anamjua Yesu. Maana kauli ya kinywa chake huwa ni uongo
 
Uthibitisho huu hapa:
Marko 1:23-24
‘Na palikuwa na mtu mwenye pepo mchafu ndani ya sinagogi lao, akapiga kelele, akisema, Ah! Tuna nini nawe, Yesu wa Nazareti? Je! Umekuja kutuangamiza? NAKUJUA WEWE NI NANI, MTAKATIFU WA MUNGU.’

Hiyo kauli ina uongo?
Sasa pepo amjue Yesu, shetani ndo ashindwe kumjua?

Halafu, kumbuka Yesu ni Mungu. Shetani na mapepo yake kabla hawajatupwa duniani walikuwa mbinguni wakimsifu Mungu. Hivyo wanamjua sana Yesu.
 
Pepo likisema Sasa hivi mchana, Toka nje kachungulie ujihakikishie
 
Kwahiyo pepo huwaingia wenye kutenda dhambi tu?
Mapepo/mashetani hayaingii tu kwa wenye dhambi. Hata wasiotenda dhambi wanaweza kuvamiwa au kuingiwa na mapepo kama wameacha "milango" wazi au wasipokuwa macho.

Ushahidi wa Kibiblia:
Katika Luka 4:33 tunasoma kuhusu mtu aliyekuwa katika ibada lakini alikuwa na pepo
"Na katika sinagogi mlikuwamo mtu mwenye pepo mchafu; akalia kwa sauti kuu..."

Huyo mtu alikuwa katika jengo la ibada, sio bar!

Katika Mathayo 16:22–23 tunasoma tena kwamba Petro alishawishiwa na Shetani kunena kinyume na mapenzi ya Mungu.
Yesu akamwambia Petro: "Rudi nyuma yangu, Shetani!"

Hapo, Petro hakuwa ameingiwa na pepo wa namna ile ya kurusha mate au kupiga mateke na mayowe, bali alitumiwa kama chombo cha ushawishi wa kishetani.

Hii inaonyesha mtu anaweza kuwa mcha Mungu lakini akatumiwa na adui kwa muda – kama hayuko makini.

Ukisoma Luka 13:11–16 utaona habari za mwanamke aliyepindana miaka 18 kwa sababu ya pepo wa udhaifu. Huyu hatuambiwi kwamba alikuwa mzinzi wala kahaba. Alionewa tu na Ibilisi, Yesu akamhurumia akamfungua, pepo wakatoka.

Mfano mwingine ni wa Anania na Safira (Matendo 5:3)
"Petro akasema, Anania, kwa nini Shetani ameujaza moyo wako..."

Anania na Safira walikuwa waumini wa kanisa la kwanza. Lakini shetani aliweza kuingia katika nia zao kwa sababu ya tamaa yao ya pesa na uongo.

Katika Mathayo 12:43–45 tunasoma kwamba mapepo yanaweza kurudi tena yalipotoka.

Andiko hilo ni mfano wa mtu aliyeondolewa pepo, lakini hakukaa katika Neno, maombi, wala kujazwa na Roho Mtakatifu. Mtu wa namna hiyo anaweza kurudiwa na pepo wengi zaidi.

Hata hivyo, dhambi ndio mlango mkubwa unaowafanya watu waingiwe na mapepo.

Nafurahi sana jinsi unavyouliza maswali. Mungu akuwezeshe kumjua Yeye na mapenzi yake. Amen
 
Uthibitisho huu hapa:
Marko 1:23-24
‘Na palikuwa na mtu mwenye pepo mchafu ndani ya sinagogi lao, akapiga kelele, akisema, Ah! Tuna nini nawe, Yesu wa Nazareti? Je! Umekuja kutuangamiza? NAKUJUA WEWE NI NANI, MTAKATIFU WA MUNGU.’

Hiyo kauli ina uongo?
Sasa pepo amjue Yesu, shetani ndo ashindwe kumjua?

Halafu, kumbuka Yesu ni Mungu. Shetani na mapepo yake kabla hawajatupwa duniani walikuwa mbinguni wakimsifu Mungu. Hivyo wanamjua sana Yesu.
Kwanza tujue pepo nani?
Wapo wa aina ngapi na sifa zao.
Tujue pepo ndiyo shetani?
Kisha tuabgalie hao pepo walionena hayo ni shetani?
 
Back
Top Bottom