Shetani hana akili. Anafaidika nini nikizini?

Boss la DP World

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2021
Posts
2,318
Reaction score
8,464
Wakuu tangu niamue kuokoka nimepata changamoto kubwa sana, leo nimezini mara ya pili hata wiki haijaisha.

Yani ni kama kasi imeongezeka, halafu niliye zini naye leo ni demu aliye nipiga chenga muda mrefu sana nikakata tamaa nikaacha kumfukuzia.

Jana akanitafuta akaniambia yupo Moro nikamjibu poa. Asubuhi akanipigia akaniambia anaondoka kesho nikajiongeza nikaomba game bila kutongoza nikijua atakataa tu maana nilimtongoza sana kipindi cha nyuma akazingua.

Nilivyo omba game akauliza sure? Nikasema yes. Tukakutana tukagongana nikamsindikiza alipofikia, sasa nipo hapa car wash napiga hesabu nimetumia kama laki 1 na 12 kufanya tukio hili na ni short time maana ntalala nyumbani.

Najua tu huyu ni shetani, hii hela ningejaza mafuta yangenisukuma wiki nzima.
 
Ila shetani mnamsingizia vitu vingi sana.

Kwani bei gani kuacha uzinzi?

Jamani okokeni muone faida za kuwa na YESU ktk maisha.
 
Ila shetani mnamsingizia vitu vingi sana.

Kwani bei gani kuacha uzinzi?

Jamani okokeni muone faida za kuwa na YESU ktk maisha.
Hapo Shetani anahusika. Unadhani Ni Nani amemteka fikra na kuwakutanisha. Muda mrefu walikuwa wanazungushana lakini baada ya mmoja kuongoka ndiyo mwingine awe romantic
 
Si makubaliano ya watu wazima? Dhambi imetoka wapi? Ni mazoezi ya kawaida na kila mtu amekuwa mwepesi na kuchangamka. Akili iko poa.
 
Mkuu kama uliuza mechi soon jiandae kua mchangiaji kwenye ule uzi wa kusingiziwa mimba.
 
Aliyekudanganya kuwa shetani hana akili kakudanganya

Ni mjanja mjanja
 
Inakuwa ngumu kumshinda shetani kwa kuwa hatumjui na maandiko hayatufunzi vya kutosha kujua mbinu zake.

Mimi kuna wakati naonaga mambo najua huyu ni shetani kabisa ila hakuna sehemu niliwahi fundishwa kuwa ana uwezo wa kufanya hayo niliyoyashuhudia.
 
Wanaume tuko na maajabu sana wakati mwingine. Jamaa aliondoka mkoani kuelekea Dar kwa mkewe tangu Jumatano ya juma lililopita.

Amechakata kitumbua hadi jana, leo hii kafika tu huku mkoani moja kwa moja kafikia kuchakata kitumbua Cha mpango wa kando

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…