Shetani mpenda sala!

Shetani mpenda sala!

Dah Nimeelewa Hii inahitaji D mbili aisee..
Ni Code Ngumu sana..
Nimejitahidi Nimeelewa ni Maswala ya Kula Keki na Maziwa na asali kwenye Ile nchi ya Ahadi
Bado mzee 😁, hujaelewa endelea kunywa maji ya baridi kwa wingi huku ukitafakari !. Maana yawezekana maisha n mtazamo tu wala sio uhalisia !,nchi ya ahadi yenye maziwa na asali ilikuwepo toka nyakati za wana waisraeli lakini Miongoni Yohane mbatizaji alipendelea kula nzige na asali 😂 chakula pendwa sana ,bila kusahau mikate isiyotiwa chachu yaan kizazi hiki huiita mabumunda 😆
 
Sasa wewe huyo shetani umemtoa wapi?
Shetani ni nani??? Lugha ya picha ,ngoja nkupe clarification hapa mtaalam!!
1. Maandiko matakatifu mfano, Katika Biblia, shetani anaweza kuonekana kama mpinzani wa Mungu, akijaribu watu ili wakiuka maagizo ya Mungu.

2. Kwa lugha ya falsafa na itikadi za ki- falsafa za Nietzsche, shetani anaweza kuwa mfano wa ukosoaji wa maadili ya jadi, akionyesha upinzani dhidi ya imani zisizo na msingi.

3. Masimulizi ya kale na tamaduni nyingi, shetani au roho mbaya huwakilisha nguvu za giza zinazoshawishi watu kufanya maovu, kama vile Hades katika mytholojia ya Kigiriki.

4. Sanaa na fasihi inatunabaishakwamba, kazi kama "Faust" ya Goethe, shetani anaweza kuwakilisha tamaa za kibinadamu na matokeo ya kujiingiza katika maamuzi mabaya.

5. Jamii inatambua kuwa nyakati zingine, shetani anaweza kuwakilisha dhana za ubaguzi na chuki katika jamii, akionyesha maovu ya kibinadamu katika mifumo ya kijamii nk.
👉🏾lugha hio ya picha
 
Inashangaza sana
Sana sana !,hakuna visonzo vya kukusanya sadaka na matoleo ,tuna na majaba na mabeseni ya kujaza masurufu ya kwenye vipembu vya kanga na vitenge vya wajane na wahitaji kwa kukirimia utakaso na baraka
 
Shetani ni nani??? Lugha ya picha ,ngoja nkupe clarification hapa mtaalam!!
1. Maandiko matakatifu mfano, Katika Biblia, shetani anaweza kuonekana kama mpinzani wa Mungu, akijaribu watu ili wakiuka maagizo ya Mungu.
Hakuna cha maandiko matakatifu wala bibi yake utakatifu.

Hiyo Biblia ni hekaya kama ilivyo hekaya za Abunuwasi.
2. Kwa lugha ya falsafa na itikadi za ki- falsafa za Nietzsche, shetani anaweza kuwa mfano wa ukosoaji wa maadili ya jadi, akionyesha upinzani dhidi ya imani zisizo na msingi.
Shetani ni nini?

3. Masimulizi ya kale na tamaduni nyingi, shetani au roho mbaya huwakilisha nguvu za giza zinazoshawishi watu kufanya maovu, kama vile Hades katika mytholojia ya Kigiriki.
Ukishasema masimulizi hata hadithi za uwepo wa Dragons 🐉 watemao moto midomoni mwao zina ingia humo humo.

Masimulizi huweza kuwa hata ya uongo.

Lakini ili yawe ya ukweli, lazima uthibitishe masimulizi hayo kwa uthibitisho na ushahidi.

Kwa hivyo masimulizi ya uwepo wa shetani, roho ni masimulizi ya uongo tu.

Wala hakuna ushahidi, wala ukweli wa uwepo wa huyo shetani au roho.

4. Sanaa na fasihi inatunabaishakwamba, kazi kama "Faust" ya Goethe, shetani anaweza kuwakilisha tamaa za kibinadamu na matokeo ya kujiingiza katika maamuzi mabaya.

5. Jamii inatambua kuwa nyakati zingine, shetani anaweza kuwakilisha dhana za ubaguzi na chuki katika jamii, akionyesha maovu ya kibinadamu katika mifumo ya kijamii nk.
👉🏾lugha hio ya picha
Shetani ni illusion.

Shetani ni kichaka kinacho tumiwa na watu kukwepa matendo yao maovu.

Yani unafanya ubaya wewe mwenyewe kwa tamaa zako halafu unaunda dhana ya kufikirika iitwayo "shetani" ndio unasema imekufanya ufanye ubaya!!!
 
Bado mzee 😁, hujaelewa endelea kunywa maji ya baridi kwa wingi huku ukitafakari !. Maana yawezekana maisha n mtazamo tu wala sio uhalisia !,nchi ya ahadi yenye maziwa na asali ilikuwepo toka nyakati za wana waisraeli lakini Miongoni Yohane mbatizaji alipendelea kula nzige na asali 😂 chakula pendwa sana ,bila kusahau mikate isiyotiwa chachu yaan kizazi hiki huiita mabumunda 😆
Nimeelewa Sema Umetumia Lugha Tamu lakini wale wa unanijua Mimi ni nani wakikukamata
 
Watumishi wengi Sana wa shetani, wamejiingiza kwa Siri kwenye kundi la Watumishi wa Mungu, hivyo wanalarua kondoo bila ya huruma
Lakini siimeandikwa utafuteni kwanza ufalme wa Mungu na hayo mengine mtazidishiwa 😂, wacha wakombe maokoto
 
Back
Top Bottom