Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 11,478
- 3,659
hapo Tanga kuna shamba moja la minazi lililopakana na usharika mmoja ambao una sehemu ya makaburi yaliyozungushiwa uzio na kuwekewa "mfano wa geti". getini yupo mlinzi mmoja mzee mchovu hivi akilinda watu kutovunja misalaba. usiku mmoja vibaka wawili wakaenda kwenye hilo shamba kuiba nazi. walipoangua za kutosha wakajaza kwenye gunia moja na fasta wakalikokota kuelekea kule makaburini. walijua mlinzi wa pale ni mchovu tu, wakavuka geti na nazi mbili zikaanguka pale. wakasikia mtu akikoroma usingizini hapo jirani. kwa hofu wakaziacha na kuzama ndani karibu kiasi na getini wakaanza kugawana nazi kila mtu na gunia lake. "hii yangu hii yako, hii yangu hii yako..." mlinzi akashtuka usingizini akasikia wakigawana ila asijue nini kinagawanywa. kwa hofu akatoka hadi nyumbani kwa mchungaji ambapo si mbali na kumweleza. mchungaji akawaza na kumwambia, "Ni mungu na shetani wanagawana roho. twende tukasikilize vizuri" hao hadi pale na kila mmoja akakaa upande wake wa geti. wakasikia wanavyogawana hadi wakamaliza, kisha mmoja wao akasema, "bado! kuna zile mbili pale getini." mlinzi kusikia vile akazirai pale pale na mchungaji haikujulikana kapitia wapi