Mungu ndiye chanzo cha yote[kwa wale wanaoamini] je ndio chanzo cha mbegu ya uasi wa shetani?
Mungu sio chanzo cha kila kitu/jambo, Mungu ni nafsi iliyokuwa.njema hivyo kila wema unatoka kwa Mungu na kila uovu unatoka kwa shetani hivyo mbegu ya uasi kwa binadamu imetoka kwa shetani.
Kwanini laana ya Mungu iendelee kutafuna vizazi hata vizazi kwa kosa lililofanywa na watuwawili waliombwa na Mungu mwenyewe?
Sio kweli kwamba laana ya Mungu inaendelea kutafuna vizazi na vizazi kwani Mungu ni Mwema na hakimu muadilifu hivyo hawezi kuangamiza mtu kwa kosa la mtu mwingine, ni hivi: kuna baadhi ya maandiko ya kiroho/Mungu yanahitaji ufafanuzi wa kiroho na sio ufafanuzi wa kimwili vinginevyo unaweza kupata tafsiri inayokwenda kinyume na "absolute justice and inconceivable meanings" katika hayo maandiko na pia kuna baadhi ya maandiko yametiwa mikono na watu katika zama za giza ili kupotosha maana halisi na kupata maana za matamanio ya nafsi zao, (Yeremia 8:8).
Kwa maana hiyo inahitaji uangalifu na uchambuzi wa kina kupata maana sahihi za baadhi ya Maandiko ya Mungu.
Kuna mahali kokote kwenye biblia pameonesha shetani aliko? Ni wapi kama hapajaoneshwa tunaanzaje kumchora shetani kama ndio chanzo cha haya maasi yote?
Mimi sijasoma sana Biblia hata hivyo sijui kama kuna mahali pameonyeshwa alipokuwepo shetani.
Labda nianze hivi; Neno shetani ni neno la asili ya kiarabu au nadhani (Semitic languages) lenye maana pana linalo maanisha kitu chochote kiovu, chenye kutenda uhalifu, madhara nk, kwa watu. Mfano mnyama mkali kama simba, chui, fisi , nyoka, mamba nk wanapodhuru watu lugha ya mfano (figurativelly) inayoweza kitumika kuitwa hao wanyama ni "shetani" kwasababu ya huo ubaya na madhara waliyosababisha kwa binadamu pia mtu muovu, mf, jambazi, Muongo, mzinzi, nk pia kutokana na huo uovu wake anaweza kuitwa Shetani kwa maana hiyo mtu akiwa shetani maana yake ndani ya moyo wake (in his mind) kuna Ushetani unaomshawishi afanye huo uovu, unaweza pia kulinganisha katika njia hii; Malaika wanawakilisha mambo yote mema na shetani anawakilisha mambo yote maovu hivyo Malaika ni sawa na Nuru na Shetani ni sawa na giza, nuru imeumbwa na giza halijaumbwa, hivyo Malaika waneumbwa na shetani hajaumbwa, ni sawa na kusema; Nuru inapoondoka giza huja ni hivyo hivyo wema/nuru inapoondoka ndani ya nafsi ya mtu ndipo ubaya, ushetani/ giza huingia ndani ya nafsi.
Hapo sasa ndipo linakuja somo.la falsafa ya kiroho kwamba Mungu akawatuma manabii na mitume wake ili tuwafuate na tuwatii ili wema/nuru za uungu ziingie mioyoni mwetu na giza/ushetani uondoke mioyoni mwetu, kifupi Mungu anapenda wema na kamwe Mungu hajaumba shetani huyo anayesemwa kwamba hupoteza watu.
Au shetani ni sisi wenyewe? Na hapa duniani ndio makao yetu?
Ndiyo shetani ni sisi wenyewe kwani ushetani umo ndani ya nafsi ya mtu mwenyewe, yaani mtu anapokataa kufuata njia ya wema maana yake mtu huyo kazima nuru ya wema ndani ya nafsi yake na hivyo anamkaribisha giza/ushetani--- na mtu huyo ataitwa Shetani.
Kumbuka mfanano huu; Malaika ni nuru na wema, Shetani ni giza na uovu.---- Nuru imeumbwa jinsi malaika alivyoumbwa kinyume chake giza halijaumbwa jinsi shetani hajaumbwa na Mungu.
🙏🏻🙏🏻🙏🏻