Shibuda awashangaa wanaoogopa urais


Semilong,

Inaelekea kweli hujui siasa za UK au ni msomaji wa SUN na umbea wa mitaani unachukulia ndio ukweli.

Ni kweli David Millibabd alitoa speech yake ambayo watu walitafsiri kama mwanzo wa kampeni ya kuongoza chama (kumwangusha Brown). LAKINI, alipoulizwa alikataa kata kata na kusema yeye anaongelea renewal chini ya Brown.

Kumrudisha Mandelson sio kwa ajili ya upinzani ndani ya Labour, ni kwasababu popularity yake ilikuwa inatelemka na Conservative kuongezeka. Kamrudisha Mandelson kama njia ya kuboresha utendaji wa serikali yake na hivyo kuzuia kuanguka kwa Labour.

Pia speech ya Milband na kurudi kwa Mandelson kulikuwa hakuna uhusiano. Hayo mambo mawili yalitokea wakati tofauti kabisa.

Mtu aliyempinga Brown kwenye serikali yake ni junior minister mmoja mwanamke na siku hiyo hiyo aliachishwa kazi tena akaambiwa na mtu wa TV kwamba umekuwa sacked.

Kwa UK ni wazi kama wewe ni waziri huwezi kumpinga PM wazi wazi, ukifanya hivyo inabidi uachie ngazi na kuomba uchaguzi na kama una wabunge wa kutosha kukuunga mkono basi uchaguzi unaitishwa, vinginevyo ukikosa wa kukuunga mkono unaishia kuwa backbencher na ndio sahau hurudi tena serikalini.
 

Semilong,

Ndio maana nasema huenda ni msomaji wa SUN, lini Brown alikataa kumwonyesha Blair
budget? Nitafutie hata sehemu moja wanaposema hivyo.

Unachoongelea wewe ni kwamba Brown alikuwa na fiscal rules zake kali kiasi kwamba baadhi ya mambo ambayo Blair angetaka pesa zitolewe, Brown alikuwa anakataa kwasababu
ilikuwa inapinga na hizo fiscal rules. Hiyo ndio sababu alikuwa anatumia na wala sio kukataa kumwonyesha budget. Kwi kwi kwi!!

Kila mtu anajua hao watu walikuwa ni maadui, ninachotaka kukuambia ni kwamba hata siku moja hawakusemeana hovyo au kupingana kwenye kwenye public. magazeti yalijaribu kuandika na kuchochea lakini kila wakiitwa kila mtu alikuwa namuunga mkono mwenzake.
 

Kwa mantiki hiyo hiyo kuna wanaCCM hawataki Kikwete aendelee kwa kushindwa kupambana na mafisadi ndani ya CCM akina Chenge, Rostam, Lowassa, Mkapa na wengineo wengi. Siyo kweli kwamba Brown alifanya mambo yake kimya kimya na hiyo article niliyoiweka hapa ni uthibitisho wa hilo kwamba. Na hata kuna wakati akataka kumuondoa kama Waziri wa Fedha lakini akapingwa na wengi ndani ya chama kutokana na kazi nzuri ambayo Brown aliifanya.

Kama Brown asingemchallenge Blair aachia ngazi si ajabu hadi hii leo angekuwa madarakani lakini Waingereza walimchoka kutokana na kumuumga mkono Kichaka karibu katika kila issue pamoja na uvamizi wa Iran na opinion polls zilionyesha kwamba support yake ilikuwa ndogo sana. Na sisi Tanzania tunasikia vilio vya nchi kuyumba, nchi imetekwa na mafisadi, uchumi wetu uko mikononi mwa wageni. Hizi ni dalili tosha za kuonyesha vilio hivi ni kutokana na wananchi walio wengi kutoridhika na uongozi ulio madarakani ndiyo maana vinazidi kuongezeka kila kukicha. When you failed to deliver your promises, you should be kicked out of office. IT IS TIME FOR CHANGE, CHANGE THAT WE NEED FOR OUR BELOVED COUNTRY.
 
Shibuda, whatever his shortcomings, is a true maverick.

His unconventional dedication to principles and the CCM constitution pales the unfounded goon's chorus of common sense defying nepotism.
 

Bubu Ataka Kusema,

Any way lengo hapa sio kubishana, ila ukweli ni huo Brown hakufanya challenge yoyote publically au kwenye interview dhidi ya Blair.

Hata hiyo ya kutaka kumwondoa kuwa waziri wa fedha uko wrong. Wafuasi wa Blair walimshauri Blair amwondoe kwenye nafasi ya kuwa waziri wa fedha, lakini dakika ya mwisho Blair aligoma. Alihofia maasi kwenye chama na akachukua uamuzi wa busara kutokufanya hivyo. Brown alikuwa hana uwezo wa kikatiba kukataa anachofanya PM.

Hapa mimi simtetei JK , lakini ni muhimu kuweka records straight. Kama wanaompinga JK CCM wako wengi basi wagombee na kumwondoa. Kuongea kwa akima Malecela hakuzuii wao kugombea. Alichotoa Malecela na wengine ni maoni yao.

Kuna kipindi wafuasi wake wa Brown ambao sio mawaziri walijaribu kuandika barua, baadhi ya wakuu wa chama wakamwambia Brown kama watu wake wanataka kumwangusha Blair, yeye asahau kuwa PM. Ikabidi Brown mwenyewe awakane na zoezi hilo likafa.

Blair alikuwa sio mjinga, alikuwa anajua kusoma nyakati. Pia alikuwa anajua historia ya kuondolewa kwa Thatcher na akajua inaweza kuja kwake pia.

Wanachofanya hapa UK kuondoa kiongozi ambaye hawamtaki whether ni kwenye serikali au chama, wale watu wa chini wanaomuunga mkono kiongozi mmoja ndio wanaanzisha maasi. Wakifikisha idadi ya kura zinazotakiwa kufanya challenge basi kazi imeisha. Uchaguzi ukiitisha na kama watu wamekuchoka, kwenye kura ya siri unapigwa nje. Hicho ndicho kilichomtokea Thatcher. Tofauti tu kwa Thatcher, aliyeomba challenge alikuwa naibu wake. Ikaishia wote wawili wakakosa na Major akapata kuwa PM kirahisi.

Mimi wakati huo nilikuwa mshabiki wa Brown na nilikuwa nasubiri afanye kitu Blair aangushwa, lakini haikutokea mpaka Blair mwenyewe alipoona anakoenda ataangushwa kwa kura. Sio kawaida UK PM kuongoza zaidi ya miaka 10.
 

Utterly, he should have got the message here. Happy Easter
 
Huu ni ukweli ulio wazi, CCM siyo imechokwa, bali ilishachokwa tangu kitambo, tatizo hakuna altenative, bora CCM iendelee kutawala maisha, after all ni zimwi likujualo...!.
 
Huu ni ukweli ulio wazi, CCM siyo imechokwa, bali ilishachokwa tangu kitambo, tatizo hakuna altenative, bora CCM iendelee kutawala maisha, after all ni zimwi likujualo...!.
 
huyu atakuwa siyo shibuda tu.kuna watu wazito nyuma yake wanautaka urais 2010 baada ya kuona uwezekano wa kumuangusha kikwete upo kama watapata upenyo ndiyo mana hawa wazee wanajitahidi kwa nguvu zote kuwavunja nguvu maanake wakiacha italeta vurugu na hata kumuharibia kikwete na kumuweka katika wakati mgumu kama upinzani wataweka mgombea mzuri.
 

Kama sikosei, huyo Shibuda aligombea pia na MKapa, kama sio yeye nakumbuka kuna jamaa toka hiyo mikoa alichukua form wakati wa Mkapa. Jamaa anajiamini na kwenye siasa tunataka watu kama hao hata kama ni wachache lakini kuna principles wanaziamini.

Chaguzi za CCM zilivyo sio rahisi kumwondoa rais aliye madarakani. Maamuzi mengi yanafanywa na CC ambayo wajumbe wake wengi wanachaguliwa na huyo mwenyekiti wao ambaye pia ni rais. Hiyo ndio inachuja majina, wana uwezo wa kutupa majina kama walivyofanya kwa Malecela na huwezi kuwahoji.

Kama kuna nafasi ya kumwondoa JK ni kupitia upinzani, sahau hii ya CCM kumwondoa JK.

Tatizo la JF kuna watu ni vipofu na hawaoni kabisa ukweli mwingine wowote zaidi ya ule wanaouamini wao.
 

Kina Malecela walitoa maoni ama walisema ni utamaduni?
Nadhani ingekuwa maoni kama wangesema kuwa wanapendelea kuona rais akichaguliwa kugombea kwa mara nyingine kutokana na sababu hizi ama zile na si wazee wazima kuja na kusema eti ni "Utamaduni"
Mtanzani fikiria kwa makini na si tu kusema ni maoni yao,kwasababu maoni yao hayo yana malengo,sasa la kujiuliza ni kama malengo hayo yana manufaa kwa Taifa na si tu kuana mambo kwa mazoea. Ni muhimu sana kuleta mabadiliko kwenye siasa zetu kwasababu hao wazee wametufikisha hapa tulipo kwasababu ya tamaduni hizo hizo.
 

Utakuwa unajidanganya ukifikiri wanasiasa wanapofanya mambo yao, lengo namba moja ni manufaa kwa taifa. Namba moja ni manufaa kwao labda mbili ndio taifa.

Ukiwa na watu kama Chenge si ajabu taifa iko namba kumi.

Maneno ya Malecela hayajabadili katiba ya CCM. Kama Shibuda anataka kugombea na atagombea tu. Lakini kweli kwa akili yako unaamini ile CC ya CCM inaweza kupita jina lingine zaidi ya JK?

Uteuzi wa mwanzo ungelikuwa unafanywa na halmashauri kuu, ningeweza japo kuamini kwamba labda inawezekana, lakini CC zaidi ya nusu ya wajumbe wanawekwa na rais/mwenyekiti, unategemea nini toka kwa watu kama hao?

Hii dunia ni muhimu mno kuelewa the reality, vinginevyo utaishia kugonga ukuta. Kwa TZ kama mnataka kumwondoa JK nafasi pekee ni kupitia upinzani na uchaguzi mkuu. Haya mambo ndani ya CCM kwa mimi naona nafasi hakuna.
 


1. mimi sio msomaji wa sun, MIMI NASOMA FT, hehehehe...
2. SABABU YA YEYE KUKATAA NI ILI ASIAMBIWE ANA CAUSE UNREST IN THE PARTY.


KUSHUKA KWA POPULARITY GB NDIO SABABU YA BAADHI YA VIONGOZI KUTAKA AONDOLEWE NA AJE MILIBAND. LORD MANDELSON NDIO BLAIR RITES #1, NA AMEWANEUTRALISE BLAIR RITES WENZAKE, NIMTENDAJI WA KAZI MZURI PIA. NA SIO LORD MANDELSON TU AMERUDI HATA ALISTAIR CAMPBELL ANAMPA USHAURI NA HAWA NI MASWAIBA WAKUBWA TONY BLAIR.

Semilong,
Pia speech ya Milband na kurudi kwa Mandelson kulikuwa hakuna uhusiano. Hayo mambo mawili yalitokea wakati tofauti kabisa.
ANGEMRUDISHA PALE PALE INGEKUWA NI KNEE JERK REACTION AMBAYO WANASIASA WA ULAYA WANA AVOID.



swala la MILIBAND KUONGEA NA WAANDISHI HILO HALINA MJADALA, WABUNGE WA GB WALIKUWA WANAMUAMBIA AMU SACK MILIBAND, WATU WOTE WALIKUWA WANAMUAMBIA INC RAFIKI YAKE ALAN SUGAR, LAKINI HAKU SACK KWA AJILI NI SIGN ZA WABUNGE 71 TU ZINAHITAJIKA ILI ITOKEE LEADERSHIP CHALLENGE. NA LAZIMA
ANGEZIPATA SIGN 71, KWA AJILI KULIKUWA NA WABUNGE ZAIDI YA 90 WAKO TAYARI.


JAMANI MBONA LIPUMBA AMEKUA CHALLENGED, JE CUF INADEMOKRASIA KULIKO CCM?
 
Last edited:


Mkuu Mtanzania labda utanipa elimu zaidi hapa manake ninavyojua CC ya ccm ina wajumbe 35 hivi au hawazidi 40 na wote ni vingunge wa juu kabisa wa ccm/taifa na wanapochuja majina ya wagombea basi mgombea ambaye ni mwana CC haruhusiwi kuwapo.Kwa maana hiyo hata kama yeye Kikwete ni mwenyekiti lakini siku hiyo itabidi atoke nje.
sasa mkuu kwa nchi yetu ilipofikia hapa au niseme ccm ya sasa hii jinsi ilivyo na umaarufu wa kikwete ulivyoporomoka,mkuu huwezi kuweka guarantee kwamba kikwete atapitishwa tu hasa ukichukulia kwa mfano watokee wagombea wenye influence kubwa.ndiyo mana hawa wazee wa ccm vichwa vinawauma.mimi nadhani ingekuwa kama ni shibuda tu peke yake mwenye nia hiyo wala wasingepoteza muda wao na waandishi wa habari na kuanza kuweka mikwara mizitomizito.
 
Last edited:
Kuna watu wana compare siasa za Europe na Tanzania, wanafanya comparisona kati ya watu walio dunia ya kwanza na ya tatu! au watu walio karne ya 21 na karne ya 17!!
 

majina yatukuwa mengi tu pale itakapofika april 2010. Mtu kama ana nafasi ya uwaziri hataki kuipoteza mpaka 2010.
Potential candidate akitangaza sasa hivi kikwete anaweza hata kumzushia kesi. Na magazeti ya chama na maswaiba yataanza kumuandama.
Ndani ya ccm sasa hivi kuna muamko.
 

Mkuu,

Hawa watu hapa chini ndio unategemea wamgeuke JK? Labda kama tunaota ndoto.
2. Msekwa - Makamu Mwenyekiti
3. Ndugu Amani Abeid Amani Karume - Makamu Mwenyekiti(Zanzibar)


4. Ndugu Yussuf R. Makamba - Katibu Mkuu

5. Capt. (mst) George Huruma Mkuchika - Naibu Katibu Mkuu (Bara)
6. Ndugu Salehe Ramadhan Ferouz - Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar)
7. Dr. Ali Mohamed Shein - Mjumbe
8. Ndugu Edward Ngoyai Lowassa - Mjumbe
9. Ndugu Shamsi Vuai Nahodha - Mjumbe
10. Alhaj Ali Hassan Mwinyi - Mjumbe

11. Ndugu Benjamin William Mkapa - Mjumbe
12. Mzee Rashid Mfaume Kawawa - Mjumbe
13. Dr. Salmin Amour - Mjumbe

14. Ndugu John Samwel Malecela - Mjumbe

15. Capt. (mst) John Zefania Chiligati - Mjumbe
16. Ndugu Amos Gabriel Makala - Mjumbe

17. Ndugu Bernard Kamilius Membe - Mjumbe
18. Ndugu Kidawa Hamid Saleh - Mjumbe

19. Ndugu Samwel John Sitta - Mjumbe
20. Ndugu Pandu Ameir Kificho - Mjumbe
21. Ndugu Anna Abdallah - Mjumbe
22. Ndugu Rostum Aziz - Mjumbe

23.Dr. Mohamed Gharib Bilal - Mjumbe

24. Ndugu Pindi Hazara Chana - Mjumbe

25. Ndugu Andrew Chenge - Mjumbe

26. Dr. Maua Abeid Daftari - Mjumbe

27. Ndugu Samia Suluhu Hassan - Mjumbe
28. Ndugu Mohamed Seif Khatib - Mjumbe
29. Ndugu Haji Omar Kheri - Mjumbe
30 . Dr. Abdallah Omari Kigoda - Mjumbe
31 . Ndugu Abdurahman Kinana - Mjumbe
32 . Ndugu Anne Semamba Makinda - Mjumbe

33. Ndugu Fatuma Said Ali Mchumo - Mjumbe
34 . Ndugu Zakia Hamdan Meghji - Mjumbe

35. Ndugu Omar Yussuf Mzee - Mjumbe
36. Ndugu Emmanuel John Nchimbi - Mjumbe
37 . Ndugu Ali Ameir Mohamed - Mjumbe

38. Ndugu Yussuf Moh'd Yussuf - Mjumbe
 

Mtanzania, point yangu inabaki pale pale,kwamba ulisema ni maoni yao kina Malecela na yaheshimiwe,na mimi nikasema kutokana na migogoro iliyolikumba Taifa,ni muhimu maoni hayo yakatolewa kwa vigezo vya ufanisi wa kazi na si utamaduni....Mtanzania kwa viongozi wa kitaifa kuzungumza maneno kama hayo kwenye wakati kama huu wewe unaona ni kawaida? Hizo ni siasa za ndani za chama,lakini si ndio viongozi hao hao wa serikali?

Utamaduni wa kawaida kwa Taifa la watu wenye akili timamu ni kuchagua ama kupendekeza kioongozi kwa vigezo vya utendaji kazi na si utamaduni.

Na kama ni kweli kuna hatari ya ccm kuumbuliwa kwenye uchaguzi kwasababu ya ufisadi,then utamaduni hapo utakuwa questionable,tusubiri tuone,cha muhimu ni utendaji wake kupimwa kabla ya kukumbatia utamaduni.

Mtanzania nilisema niko neutral kwenye issue hii lakini nilitegemea maneno ya busara zaidi kutoka kwa viongozi wenye calibre ya Malecela na wenzake,kwamba vikao halali vya chama vitakaa kama taratibu zinavyosema,na katiba/kanuni za chama zitafuatwa wakati wa kumteua mgombea urais kwa tiketi ya ccm...Maneno kama hayo yangeonyesha kuwa tuna viongozi wenye busara,lakini kuja na kusema ni utamaduni kuteua mgombe urais mara mbili bila kupingwa ni kuonyesha less concern about the rality and the future of our nation.
 

Mkuu kwanini una uhakika wa 100% kwamba hawawezi kumgeuka?si wanasiasa hawa,sasa wanasiasa nao wana urafiki wa kudumu/uadui wa kudumu?wanasiasa siyo wakuwaamini mkuu na usikute kwenye hiyohiyo list kuna mtu keshajipanga tayari kushindana na kikwete!!
 
mimi sio msomaji wa sun, MIMI NASOMA FT, hehehehe...

Mkuu Semilong,

Kumbe ndio maana kwasababu FT hawaandiki siasa kwi kwi kwi!!!

Heri nikuache uhangaike na derivatives, futures, hedging, swaps, options, forwards!

Mimi nikisoma FT huwa nasinzia, too boring!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…