gordon brown(GB) alikua anatetemeshwa na DAVID MILLIBAND(DM), na DM akafanya interview ambayo ikaleta mizengwe sana labour ikashidwa glasgow kwa mara ya kwanza, GB alichofanya ni kumrudisha adui wake mkubwa LORD MANDELSON (AKA PRINCE OF DARKNESS) kutoka europe. Lord M alivyofika wale blairites wote ikabidi wanyamaze na ndio GB alipoponea.
Semilong,
Inaelekea kweli hujui siasa za UK au ni msomaji wa SUN na umbea wa mitaani unachukulia ndio ukweli.
Ni kweli David Millibabd alitoa speech yake ambayo watu walitafsiri kama mwanzo wa kampeni ya kuongoza chama (kumwangusha Brown). LAKINI, alipoulizwa alikataa kata kata na kusema yeye anaongelea renewal chini ya Brown.
Kumrudisha Mandelson sio kwa ajili ya upinzani ndani ya Labour, ni kwasababu popularity yake ilikuwa inatelemka na Conservative kuongezeka. Kamrudisha Mandelson kama njia ya kuboresha utendaji wa serikali yake na hivyo kuzuia kuanguka kwa Labour.
Pia speech ya Milband na kurudi kwa Mandelson kulikuwa hakuna uhusiano. Hayo mambo mawili yalitokea wakati tofauti kabisa.
Mtu aliyempinga Brown kwenye serikali yake ni junior minister mmoja mwanamke na siku hiyo hiyo aliachishwa kazi tena akaambiwa na mtu wa TV kwamba umekuwa sacked.
Kwa UK ni wazi kama wewe ni waziri huwezi kumpinga PM wazi wazi, ukifanya hivyo inabidi uachie ngazi na kuomba uchaguzi na kama una wabunge wa kutosha kukuunga mkono basi uchaguzi unaitishwa, vinginevyo ukikosa wa kukuunga mkono unaishia kuwa backbencher na ndio sahau hurudi tena serikalini.